Kama ni kweli Ma - DED zaidi ya 100 watapandishwa kizimbani na TAKUKURU kwa Ufisadi basi mfumo wa MagufulI kuteua Makada wa CCM Umefeli

Bado tunasafari ndefu sana, sheria zipo, watu wanafanya blunders na bado wenye mamlaka wanasita kuwawajibisha.
 
Acha uwongo,Makada wa CCM wanateuliwa tangu enzi za JK,Tena kwa JK ndiyo ilikuwa balaa,Kuna watu TAMISEMI walikuwa wanapiga Hela za rushwa za watu wanaotaka Ukurugenzi wa Wilaya,ukihitaji U-DED unanunua kwa pesa yako.Jiwe ndiyo alikuja kuwaondoa hao Wahuni.
 
Miaka yote kabla ya jiwe ilikuwa DED anateuliwa kutoka miongoni mwa watumishi wa serikali wenye uzoefu wa muda mrefu. Jiwe akaleta ukadda, ukanda na ukabila kwenye uteuzi wa maDED.

Jiwe!!! Bora afe tena huko aliko.
Je hiyo hali ilibadilika?
 
Haya
 
Hiyo ya wakuu wa Idara wote kuwa wahasibu hapana.
Namaanisha mkuu wa idara ya fedha (mtunza hazina) lazima awe CPA similar kwa internal audit head lazima awe CPA na certified internal auditor
 
Hiyo ripoti si ya 2021/2022 kipenzi cha watanzania alishatangulia
 
Miaka yote kabla ya jiwe ilikuwa DED anateuliwa kutoka miongoni mwa watumishi wa serikali wenye uzoefu wa muda mrefu. Jiwe akaleta ukadda, ukanda na ukabila kwenye uteuzi wa maDED.

Jiwe!!! Bora afe tena huko aliko.
Utaratibu wa kuteua MADED kutoka kwq watumishi wenye uzoefu ulikuwq bora sana maana hata ghiriba na hila za madiwqni walizijua yeye akauondoa bora amekufa chizi yule
 
Kufuru au kufeli kwa mtu au serikali unategemea itikadi inayokuongoza.

Itikadi ndio chanzo cha sheria, sera, kanuni na utamaduni wa mtu au serikali.

Tumeamua kuikubali itikadi ya serikali kutokuwa na dini. Hiki ndio chanzo kikuu cha mazingaombwe ya watendaji serikalini.

Serikali kutokuwa na dini ina maana zaidi ya tano. Hapa nitawatajia maana mbili.

1. Unapoingia ktk majukumu ya kuserikali acha dini yako nje ya shughuli hizo.

Hapa usihoji kwanini watendaji haina. Kwani itikadi yao wamejengwa kuwa hawatokuja kilipwa kwa matendo yao.

2. Kazi kubwa ya dini ni kumjenga mwanadamu ktk upendo, huruma, utu nk. Na serikali si majengo au katiba. Serikali ni watendaji.

Kutokuwa na dini ni kukosa mambo hayo. Ukitaka kujua serikali haina dini. Nenda muhimbili. Kuna mateso wagonjwa wanayapata kwa kuwa watumishi hasa ustawi wa jamii kwa kukosa utu, huruma na upendo.

Tunahitaji kwanza kubadili itikadi ya serikali. Tunahitaji chama kitachounda serikali ya DINI ZOTE
 

Dhalimu alikuwa anajua sana tabia za wañaccm wenzake, lakini ili kusaka sifa za kijinga eti CCM chini yake iligeuka imara, ndio kulifanya afanye hayo. Usitegemee mtu ambaye sio muadilifu kwenye chaguzi, atakuwa muadilifu kwenye utendaji.
 
Hao maafisa mipango si ndiyo wezi wenyewe uko Halmashauri!
 
Ukicheleweshewa posho unakuwaga na akili sn
 
Hao maafisa mipango si ndiyo wezi wenyewe uko Halmashauri!
Hapana hao siyo wezi, wizi kwa sehemu kubwa upo orchestrated na wakurugenzi kwa kuchepusha matumizi ingawa sehemu kubwa wanaochangia mawaziri yaani unakuta Waziri anatembelea mfano Geita anajua kuna madini anataka hela au anaenda Simanjiro anajua kuna tanzanite anataka apewe hela, hilo nalo Mh Rais alijue, hata hao waliopata hati safi wengi ni rushwa wanawaandalia wakaguzi wanawake malaya na kuwalipia hotel etc, yaani wengi ambao hawakutoa ndiyo hati chafu, kwa ufupi kuna mambo mengi sana Mh Rais akiamua kufuatilia
 
Hao ni CHAWA wanajifariji.

Ni miaka 2 sasa na tumempongeza mama. Tumuombe atimue makada wote. Ateue senior Officers wanaoujua vizuri Utumishi wa umma.
Wale wanaofanya over invoicing hawajui vizuri Utumishi wa Umma?
Hapa haijalishi ni kada au siyo kinachotakiwa ni adhabu kali kama kifungo miaka 30 au kutaifishwa Mali za muhalifu.
 
Kwa mujibu wa katiba, watumishi wa uma na vyombo vya ulinzi na usalama, hawatakiwi kuonesha uhusiano wa wazi, ushabiki au upendeleo kwa chama chochote cha siasa.
Kuteua makada ni uvunjifu wa wazi wa katiba.
Wapo watumishi wengi sana wa uma wenye weledi na sifa ambao hawajihusishi na siasa wanafaa kuteuliwa.
 
Mimi nadhani kuwa Kada siyo tatizo tatizo ni kukosa maadili na kutokuheshimu Mali za Umma,jambo lingine jamii imekumbwa na mmomonyoko wa maadili kwa vile tuliamua kuwaweka kando viongozi wa kimila ambao kwa nyati zile waliheshimika katika jamii kwa kusimamia miiko mira na dastuli lakini kwa sasa tumepoteza mwelekeo ndiyo matokeo ya kuona haya ya viongozi kutokuheshimu nyazifa wanazo pewa.
Nishauri mpango wa Mama yetu Rais wetu Dr.samia Suluhu Hassani kuwarejesha viongozi wa kimila tuuone kama njia bora ya kutafuta kurejesha maadili katika jamii yetu asante.
 
Mkuu ungeandaa uzi kabisa ili hoja yako ikae vizuri maana unaongea mambo mazito ambayo sidhani kama Mama anayajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…