KAMA NI KWELI MUSA NDO MWANDISHI WA VITABU VITANO VYA BIBLIA KUNA SEHEMU KUNAYUMBA

Unasema unasoma vitabu vingi na tofauti tofauti ila vile unavyokuja kupendekeza hapa watu wakavisome ni vile tu ambavyo vinaendana na misimamo yako au tuseme vinaonesha mapungufu ya imani za dini au Mungu.

Wewe unavyovisoma hivyo vitabu na unavyovichukulia usifikiri na wengine na wengine watavichukulia kama wewe,nimeeleza kuwa kuna watu waliyokuwa na misimamo ya kuwa hakuna Mungu na baadaye wakaja kuamini Mungu,si kwamba hawakuwa na hoja kama hizo walikuwa nazo.

Ukichunguza vizuri hili suala la kuamini au kutoamini Mungu ni zaidi ya sababu tunazofikiri ndio chanzo cha kuamini au kutoamini,ndio maana nikakwambia wewe endelea kusoma pengine utakuja kupata majibu ya hoja zako au kuona tatizo la msingi katika hizo hoja.
 
Ninachojua in 5000 yes to come hizi dini zitafutika zitakuja dini nyingine.. Maana huo wakati binadamu wataweza kupambana na uzee na kifo sasa utamwambia nini kuhusu afterlife sana sana zitakuja dini Mpya kulingana na shida zisizokuwa na majibu enzi hizo
 
Kamwambie ukweli magu kua anaenda vibaya kiuongozi uone itakua vipi
Tukimzungumzia Magu haitasaidia,maana hata huyo Magu ameshawatumbua sana waliyokuwa wakifanya udanganyifu,sasa hapo utasemaje?
 
Hata sababu ya kuja kwa mitume kwenye hizo dini ni kwa sababu watu walikuwa wameacha au kusahau mafundisho,sasa toka hizi dini zianze hadi leo kuna changamoto ngapi lakini hadi leo bado dini zipo?
 
Hata sababu ya kuja kwa mitume kwenye hizo dini ni kwa sababu watu walikuwa wameacha au kusahau mafundisho,sasa toka hizi dini zianze hadi leo kuna changamoto ngapi lakini hadi leo bado dini zipo?
mafundisho yapi huvu unajua duniani kulikua na specie nyingine ya mwanadamu sema imefutika sasa nani alikua wa kwanza kuumbwa sisi au wao... dini ni imagination na hiyo imagination inatufanya tuachive vitu vikubwa sisi binadamu
 
mafundisho yapi huvu unajua duniani kulikua na specie nyingine ya mwanadamu sema imefutika sasa nani alikua wa kwanza kuumbwa sisi au wao... dini ni imagination na hiyo imagination inatufanya tuachive vitu vikubwa sisi binadamu
Sijakupata vizuri mkuu.
 
Musa hajawai kuandika kitabu hata kimoja..


Nitakuja na maelezo

Sawa Mkuu, ukipata muda njoo na maelezo ili tubadilishane ujuzi ; Kwa jinsi ninavyo elewa Musa aliandika Vitabu 4 vilivyokamilika na 1 aliandika nusu, nusu nyingine ikamaliziwa na Joshua.
Vitabu viinne ni Mwanzo,Kutoka ,Mambo ya Walawi na Hesabu. Kitabu alichoandika kikaishia katikati ni Kumbukumbu ya Torati .

- Tuanza na kitabu cha hesabu,
Hesabu 33:2 Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.

2: Kumbukumbu la Totati
-Kumbukumbu la Torati 31:9 Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la agano la BWANA, na wazee wote wa Israeli.

3: Kutoka
-Kutoka 24:4 Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli,

-Kut 34:27 BWANA akamwambia Musa, Andika maneno haya; kwa kuwa mimi nimefanya agano nawe, na pamoja na Israeli, kwa mujibu wa maneno haya.

4: Bwana Yesu Kristo wa Nazareth alithibitisha Musa kuandika Torati.
-Luka 24:44 Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika TORATI ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.

Yohana 5:46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye ALIANDIKA habari zangu.
Yohana 5:47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?

- Ukisoma kifungu hiki pua utaona Musa aliandika Torati.
Yohana 1:45 Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye ALIYEANDIKWA na MUSA KATIKA TORATI, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.
 
bible stories are nothing but a copy and paste from the egyptian book of the dead
 
Mkuu Kiranga unayo soft copy ya hiki kitabu unisogezee
 
Mkuu kitabu cha mwanzo kimeandikwa 600 BC wakati Mussa ameishi miaka zaida ya 1490 BC.... Wanatheolojia wanakubali kuwa mussa amechangia data kwenye hizo pentateuch lakini yeye kama yye hakuandika ni sawa tu na kitabu cha Isaya au barua za paulo sura nyingi ziliongezwa ama kuandikwa na wafuasi wao ila majina ya vitabu walipewa wao maana ndio walikuwa wana credibility kuliko hao wafuasi. Pia kuhusu Yesu kusema Mussa aliandika sio necessarily lazima iwe Vitabu vya kwenye biblia huenda aliandika tu machapisho ambayo ndio wayahudi miaka ya 600BC wakatumia kucompile vitabu vile 5 vya kwanza vya biblia. Tafiti zaidi kuhusu mosaic authorship utagundua kitu flani hapa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…