Kama ni kweli ninapinga kwa Papi Ousmane Sakho 'Kutemwa' Simba SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
GENTAMYCINE sijawahi Kukosea nikimpenda na Kumkubali Mtu kwani nina Jicho la Uhakika na la Kuona mbali pamoja na Ubora wa Mtu / Kitu.

Simba SC koseeni kote ila msithubutu Kumuacha (Kumtema) Mchezaji Raia wa Senegal Ousmane Papi Sakho kwani mtakuja Kujuta na Kunikumbuka hadi Kumkubuka na Yeye pia.

Sakho ni Mshambuliaji na Winga aliyekamilika karibia 90% ya Mtu ambaye Simba SC inamuhitaji ila tu Majeruhi na 'Miba' anayopigwa na Wachezaji Wawili Wazawa ndiyo vinamtesa na Kumkwamisha kutupa kile ambacho Wadau na 'Scouts' tulikiona Kwake.

Chonde Chonde Uongozi wangu wa Simba SC msimteme (msimuache) huyu Sakho bali mpeni mwaka Mmoja zaidi wa kuwa nae na naamini mtakuja kunipigia 'Salute' GENTAMYCINE hapa JamiiForums.

Huyu Sakho ni zaidi ya Jose Luis Miquissone ndiyo maana hata wakati anakuja Simba SC 'African Football Pundits' wengi waliipongeza Simba SC kwa Kumsajili kwani tayari alikuwa njiani kuelekea nchini Ufaransa kusajiliwa na moja ya Vilabu Shindani katika Ligi Daraja la Pili huko.

Ninasisitiza Ousmane Sakho asiachwe!!!
 
Nikimwangalia Pape ousmane sakho aina yake ya uchezaji na spirit ya upambanaji anapokua uwanjani, inanijia taswira ya Jose Luis miquissone. Simba wasifanye makosa ya kumuacha huyu mwamba anahitaji muda kidogo tu kuprove uwezo wake.
 
Wachezaji wa kigeni pale kuondoka labda wawe,Duncan,Wawa alafu aletwe beki mmoja kijana asimame na inonga,kagere umri umeenda aletwe staraika wa nje mzuri, wakati huo iangaliwe fomu ya mugalu kama bado majeruhi itabidi dirisha kubwa ampishe mtu,hakuna kiungo mkabaji pale lwanga majeruhi mengi,nafasi yake inahitaji mtu japo sio kumuacha lwanga,
 
Naunga hoja sakho na Banda wale Ni hazina kwa Simba ,hata wanaosema atemwe Banda hawana jicho la mbali ,hao wote wawil Ni talented pia umri wao unaruhusu Sana ,wapewe muda wa kutosha watatusaidia mbelen , hata Duncan sio mchezaj wa kuachwa kizembe.

Wakutemwa hapa Ni Hawa
Wawa
Kagere
Hawa Ni kimataifa .
Kibongo bongo wakutemwa Ni
Bocco
Nyoni
Gadiel
Kakolanya

Hao ndio hawana msaada kwa Simba ya Sasa yenye malengo ya kimataifa ,wengine wote wako fresh kabisa isipokua Kibu apewe program maalum kumfanyia councelling apunguze pupa akipata mpira awe mtulivu ,hii program imhusu na Mugalu pia.

Bench la ufundi toa yule Mrundi Hitmana maana anakula pesa ya bure tu pale msimbazi.
Wahamasishaji toa Mwijaku Tena akae mbali na Simba kabisa.
Msemaji wa Timu atafutwe mwenye Busara Simba ya Sasa sio ya kuwa na msemaji dizain ya manara ,mchukueni hata Masaubwire yule bro Ana busara Sana .
Upande wa viongoz ,Mangungu apewe semina ya Nini maana ya kiongoz mkubwa kwenye club kubwa Kama Simba ,apunguze kuharisha hovyo hovyo mbele ya kamera pia aache habar za kuwawazia wapinzan pind anapofafanua Jambo.
Kwa Leo Ni hayo tu
 
Naunga hoja sakho na Banda wale Ni hazina kwa Simba ,hata wanaosema atemwe Banda hawana jicho la mbali ,hao wote wawil Ni talented pia umri wao unaruhusu Sana ,wapewe muda wa kutosha watatusaidia mbelen , hata Duncan sio mchezaj wa kuachwa kizembe...
Nahunga mkono mawazo yako hila nasisitiza Banda na Sakho wabaki,
 
Genta nunakuunga mkono.
Simba wasifanye makosa ya kumtema Sakho.
Viongozi kama wapo mnaopitia mada za humu, wekeni akilini juu ya mada hii na kuifanyia kazi.
 
Kocha amewaona wote. Anajua pia uwezo wa wanaokuja na namna atakavyowatumia.

Usajili wa Simba unamalengo ya michuano ya Africa, sio ligi ya Bongo.
Tuliaminishwa hivyo wakati wa usajiri lakini mpka sahizi nahisi unaona kinachoendelea kutukuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…