Elevat Kapela
JF-Expert Member
- Dec 9, 2017
- 631
- 1,837
Rais Magufuli anaweza kuwa na ndoto nyingi sana juu ya Taifa hili lkn naamini ameshindwa kabla ya kuanza.
Tuanze na hiki ninachokisikia mara kwa mara kikitamkwa na rais na watendaji wake Tanzania ya viwanda. Je Tanzania ya viwanda yaweza kufikiwa? Jibu ni Hapana.
Sababu ni zifuatazo:
1. Hakuna intelejensia ya uchumi inayohusika na suala hili. Kwa wasiojua, nchi yeyote unayoiona imeendelea kiviwanda ujue wana fanya kitu kinachoitwa "economic intelligence" ambayo kazi yake ni kutafuta taarifa, kuzichambua na kuja na jawabu wapi kijengwe kiwanda gani na kwa nini?
Pia kikundi cha majasusi wa kiuchumi wanatakiwa kukokotoa malighafi na zao la bidhaa linalozalishwa, pia huangalia masoko ya bidhaa hizo pamoja na ushindani wake.
Katika hili hufanya uchambuzi wa kitaalamu ambao utasaidia kuutazama ushindani wa bidhaa za nje na kutafuta namna ya kufanya fitna juu ya bidhaa za nje zisinunulike ndani kwa lengo la kulinda bidhaa za ndani. Likiliangalia jambo sioni kama serikali inalifanyia kazi lakini naona matamko tu yasiyokuwa na maana.
2. Teknolojia na wataalam. Nilimsikia waziri Jafo akiagiza kila mkoa unatakiwa uwe na viwanda 100. Kiukweli kama mchumi nilipigwa na butwaa. Swali la kujiuliza viwanda gani hivyo vinatakiwa kuwa 100?
Kwa wataalam gani walioandaliwa kufanya kazi kwenye viwanda hivyo? Kwa teknolojia ipi itasaidia viwanda hivyo vizalishe bidhaa bora kwa ushindani katika kizazi hili cha zama za taarifa?. Mathalani, chukulia mkoa wa Shinyanga wenye wilaya nne uwe na viwanda mia, kwa maana kila wilaya iwe na viwanda 25.
Sasa kwa mtu mwenye akili sawia ni malighafi ipi inapatikana Shinyanga vijijini inayoweza kuhimili viwanda 25? Kwa nguvu kazi ipi ipo Shinyanga vijijini kuhimili viwanda 25? Kwa nishati gani itatumika kuendesha hivyo viwanda 25? Ukijiuliza maswali haya utaona ndoto ya Tanzania ya viwanda kwa serikali hii haitatimia.
3. Serikali imeshindwa kufanya kazi kama timu. Nina imani wizara zote zilizoundwa hazina muunganiko wa kufikia dira moja. Katika nchi za Ki- Afrika kila waziri anapuyanga kivyake tu ili mradi aonekane kwenye luninga akisisitiza jambo au akitoa maelekezo. Mathalani waziri wa Kilimo ndani ya nchi anaweza kuwa hana mawasiliano na waziri wa nishati kwa kudhani hakuna wanapokutana kidhamira.
Usishangae DAS akiongea lake na DED akiwa na lake ndani ya wilaya moja. Omba MUNGU akupe muda mrefu wa kuishi uone ukweli huu kuwa kwa serikali hii ya ccm hakuna Tanzania ya viwanda Bali Kuna maneno tu yasikuwa na Mipango mikakati.
4. Wizi wa teknolojia. Naamini kama nchi hakuna tulikopeleka vijana wetu wakaibe teknolojia baadaye warudi. Naaminisha kuwa tunaweza kupeleka vijana wetu China na wakaajiriwa huko kama wafanyakazi kumbe nyuma ya pazia wajue wameenda kujifunza teknolojia ambayo tunahitajika waifanyie kazi hapa nchi kwa kuiboresha zaidi.
5. Fedha za kuendesha na kuboresha viwanda hazipo. Ukweli usiopingika kwa hali hii ya nchi sioni mwale wa matumaini juu ya viwanda, labda kama ni viwanda vya cherehani kama alivyosema waziri twaweza kujikongoja lakini kama tunataka na sisi tuzalishe pikipiki na magari bado tuko mbali sana.
WanaJF kama kuna mtu anaamini kwa serikali hii ya mwendokasi twaweza kupata viwanda naomba anipe facts lakini kwangu mimi kama mchumi na mtaalamu wa mipango naona safari bado ni ndefu sana haya unayoyaona ni maigizo.