Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jibu maswali kwanza kwa sababu inawezekana umelikuza sana hili swala la "Tanzania ya viwanda" Kiasi cha kuona haliwezekani. Sasa kwa kuwa wewe umesema ni mtaalam, ungetujulisha hilo kwanza ili tuendelee.Unajibu hoja zangu au unaniuliza maswali ? Jibu hoja?
Umetokwa mapovu tu hakuna la maana uliloongea. Argument zako zote hazina nukuu yeyote ya kitaalam, je inchi za kwanza kuanzisha viwanda vilifanya uchunguzi toka nchi zipi? Industrial revolution ilifanyika wapi hiyo intelijensia ya uchumi? Hayo ni mawazo ya Kichadema hayana nafasi kwa Tanzania ya leo.Rais Magufuli anaweza kuwa na ndoto nyingi sana juu ya Taifa hili lkn naamini ameshindwa kabla ya kuanza.
Tuanze na hiki ninachokisikia mara kwa mara kikitamkwa na rais na watendaji wake Tanzania ya viwanda. Je Tanzania ya viwanda yaweza kufikiwa? Jibu ni Hapana.
Sababu ni zifuatazo.
1. Hakuna intelejensia ya uchumi inayohusika na suala hili. Kwa wasiojua, nchi yeyote unayoiona imeendelea kiviwanda ujue wana fanya kitu kinachoitwa "economic intelligence" ambayo kazi yake ni kutafuta taarifa, kuzichambua na kuja na jawabu wapi kijengwe kiwanda gani na kwa nini?.
Pia kikundi cha majasusi wa kiuchumi wanatakiwa kukokotoa malighafi na zao la bidhaa linalozalishwa, pia huangalia masoko ya bidhaa hizo pamoja na ushindani wake.
Katika hili hufanya uchambuzi wa kitaalamu ambao utasaidia kuutazama ushindani wa bidhaa za nje na kutafuta namna ya kufanya fitna juu ya bidhaa za nje zisinunulike ndani kwa lengo la kulinda bidhaa za ndani. Likiliangalia jambo sioni kama serikali inalifanyia kazi lakini naona matamko tu yasiyokuwa na maana.
2. Teknolojia na wataalam. Nilimsikia waziri Jafo akiagiza kila mkoa unatakiwa uwe na viwanda 100. Kiukweli kama mchumi nilipigwa na butwaa. Swali la kujiuliza viwanda gani hivyo vinatakiwa kuwa 100?
Kwa wataalam gani walioandaliwa kufanya kazi kwenye viwanda hivyo? Kwa teknolojia ipi itasaidia viwanda hivyo vizalishe bidhaa bora kwa ushindani katika kizazi hili cha zama za taarifa?. Mathalani, chukulia mkoa wa Shinyanga wenye wilaya nne uwe na viwanda mia, kwa maana kila wilaya iwe na viwanda 25.
Sasa kwa mtu mwenye akili sawia ni malighafi ipi inapatikana Shinyanga vijijini inayoweza kuhimili viwanda 25? Kwa nguvu kazi ipi ipo Shinyanga vijijini kuhimili viwanda 25? Kwa nishati gani itatumika kuendesha hivyo viwanda 25? Ukijiuliza maswali haya utaona ndoto ya Tanzania ya viwanda kwa serikali hii haitatimia.
3. Serikali imeshindwa kufanya kazi kama timu. Nina imani wizara zote zilizoundwa hazina muunganiko wa kufikia dira moja. Katika nchi za Ki- Afrika kila waziri anapuyanga kivyake tu ili mradi aonekane kwenye luninga akisisitiza jambo au akitoa maelekezo. Mathalani waziri wa Kilimo ndani ya nchi anaweza kuwa hana mawasiliano na waziri wa nishati kwa kudhani hakuna wanapokutana kidhamira.
Usishangae DAS akiongea lake na DED akiwa na lake ndani ya wilaya moja. Omba MUNGU akupe muda mrefu wa kuishi uone ukweli huu kuwa kwa serikali hii ya ccm hakuna Tanzania ya viwanda Bali Kuna maneno tu yasikuwa na Mipango mikakati.
4. Wizi wa teknolojia. Naamini kama nchi hakuna tulikopeleka vijana wetu wakaibe teknolojia baadaye warudi. Naaminisha kuwa tunaweza kupeleka vijana wetu China na wakaajiriwa huko kama wafanyakazi kumbe nyuma ya pazia wajue wameenda kujifunza teknolojia ambayo tunahitajika waifanyie kazi hapa nchi kwa kuiboresha zaidi.
5. Fedha za kuendesha na kuboresha viwanda hazipo. Ukweli usiopingika kwa hali hii ya nchi sioni mwale wa matumaini juu ya viwanda, labda kama ni viwanda vya cherehani kama alivyosema waziri twaweza kujikongoja lakini kama tunataka na sisi tuzalishe pikipiki na magari bado tuko mbali sana.
WanaJF kama kuna mtu anaamini kwa serikali hii ya mwendokasi twaweza kupata viwanda naomba anipe facts lakini kwangu mimi kama mchumi na mtaalamu wa mipango naona safari bado ni ndefu sana haya unayoyaona ni maigizo.
Hapa kumbuka mpango ni kila mkoa viwanda 100. Maana yake, Shinyanga 100, Tabora 100 vivyo hivyo na mikoa mingine yote 34 Tanzania nzima....Shinyanga haitazamwi kuwa soko pekee la viwanda hivyo 25, bali Tanzania yote na nne yake, mwekezaji anajua hilo
Mimi sijaona kama kalikuza ama kalifanya dogo...Jibu maswali kwanza kwa sababu inawezekana umelikuza sana hili swala la "Tanzania ya viwanda" Kiasi cha kuona haliwezekani. Sasa kwa kuwa wewe umesema ni mtaalam, ungetujulisha hilo kwanza ili tuendelee.
Maswali Ni sehemi mojawapo ya mjadala.Mimi sijaona kama kalikuza ama kalifanya dogo...
Alichofanya ni kueleza jinsi sera ya ujenzi wa viwanda ilivyo ngumu kutekelezeka kwa mtazamo na vigezo vyake kwa elimu yake ya uchumi aliyonayo...
Kwa maana hiyo, kama kuna mahali unataka kum - challenge, fanya hivyo kwa kukosoa hoja zake na kuweka zako ili wengine tuendelee kujifunza...
Nadhani hii ndiyo maana ya mijadala, au siyo bwana?
Pu mbavu badala kujibu hoja unaleta ushabiki wa vyama, muwe mnatumia akili za kichwani na sio za makalio.Umetokwa mapovu tu hakuna la maana uliloongea. Argument zako zote hazina nukuu yeyote ya kitaalam, je inchi za kwanza kuanzisha viwanda vilifanya uchunguzi toka nchi zipi? Industrial revolution ilifanyika wapi hiyo intelijensia ya uchumi? Hayo ni mawazo ya Kichadema hayana nafasi kwa Tanzania ya leo.
Haijalishi, mradi tu tunatimka. Chezea wenye mbio wee!Wanachanja mbuga kuelekea wapi?
Maswali Ni sehemi mojawapo ya mjadala.
Tanzania ya viwanda inawezekana Sana, bila intelligence au kuiba technology Kama anavyodai mleta mada.
Viwanda kuwepo Tanzania ndiyo kutachochea technology transfer. Unaleta viwanda, na viwanda vinakuletea technology. Wataendesha wageni kwanza, lakini hatimaye sooner or later wazawa watajifunza technology hiyo.
Haya mambo Ni time-consuming na siyo ya kesho au keshokutwa.
Ndiyo maana nikauliza mleta mada unaipimaje nchi kuwa ya viwanda?
Kutokana na data za UNIDO, 2017 Tanzania Ni nchi mojawapo Africa inayo industrialize fast. Hasa enzi za Kikwete manufacturing was growing really fast.
Inawezekana Tanzania kuwa an industrial economy, mbona Bangladesh, Cambodia Ni industrial economies?
Guatemala Ina Manufacturing Value Addition kubwa kuliko East Africa yote na Ina umeme kidogo kuliko Tanzania. Unajua Hilo?
Tusilalamike serikali tu, what about us? Are we manufacturing minded?
Kwa hiyo maswali yangu yapo very valid. Ni kwamba tu hili jukwaa linatumika for bashing the government kwa masuala ya kisiasa. Ukiwa na mawazo tofauti, utatukanwa na kupingwa.
WEKA NAMBA 4 NDIO IWE YA KWANZA.Asante mtaalamu Kapela! Kiukweli hata dhamira ya kuwa na viwanda nchi hii haipo. Kilichopo ni kampeni za uraisi 2020. Ulichoandika ni facts kuhusu ndoto hizi za mchana na wachumi wengi humu JF tumelisemea sana hili jambo ambalo halihitaji degree ya uchumi kuelewa kuwa kwa uongozi uliopo litabakia kuwa ndoto.
Watu wanafikiri viwanda vinaanzishwa kwa matamko na kukua kama uyoga. Bila ya kuwa na mikakati iliyokwenda shule tusahau kabisa.
Kwa maoni yangu, tulipaswa kuwa na:
1. Mapinduzi ya kilimo kwanza; mifumo ya umwagiliaji ingejengwa kwa wingi huku ikibidi kuleta wawekezaji wa nje kulima kibiashara.
2. Kuingeza thamani ya mile kinachozalishwa shambani, kiasi cha kuuza nje.
3. Kuboresha diplomasia na intelegensia ya uchumi.
4. Kuboresha elimu katika ngazi zote katika namna ambayo itaongeza human capital inayohitajika sana katika mapinduzi ya viwanda.
5. Nishati ya umeme ya uhakika. Tuna gesi, makaa ya mawe na maji mengi, upepo mwingi na mwanga wa jua wa kutosha.
I DO NOT believe in miracles!
Rais Magufuli anaweza kuwa na ndoto nyingi sana juu ya Taifa hili lkn naamini ameshindwa kabla ya kuanza.