Kama ni mzima wa afya mshukuru Mungu, kuna watu wanateseka na maradhi

Kama ni mzima wa afya mshukuru Mungu, kuna watu wanateseka na maradhi

Pole mleta mada , Mungu ni mwema walao umekua na hali njema. Izidi kuwa kuwa hivyo kwa neema ya Mungu.

Nashukuru mada yako na comment zake nimezikua binafsi kwangu zimenipa changamoto usiku huu !

Naamini mwenyezi Mungu atakujalia neema ya kuwazuru wagonjwa na wenye mahitaji maalum .
 
Mm
Wasalaam ndg,

Nianze kwakusema kuna binadam wanateseka na magonjwa ile mbaya analazwa hospital hadi anazoeana na kila mfanyakazi wa hospital kuanzia walinzi, wafanya usafi, manesi na madaktari.

Iko hivi last month jumatatu tarehe 20 nilipata ajali maeneo ya Ngunja Mkuranga nikiwa na pikipiki nikitokea shambani Mkiu.

Nikiri kuwa niliponea chupuchupu kifo kwenye ajali ile maana nilizima na kuja kuzinduka nikiwa Mbagala hospital, huku na huku tiba ikashindikana pale kutokana n mvunjiko wa mfupa hivyo nikapewa rufaa ya kwenda MOI maana nilikuwa nimevunjika mara mbili (olecranon bone) mfupa wa kiwiko cha mkono wa kushoto, basi bana nikarudi home ili siku inayofuata niende MOI.

Basi siku iliyofuata nikaenda MOI nikaonana na wataalam nikafanya vipimo na kuambiwa tiba yangu ni kuwekewa chima hivyo nifanye malipo kwajili ya upasuaji.

Sio siri suala la kuwekewa chuma liliniwazisha sana na kuanza kutafuta tiba mbadala lakini at the end nikakubali nakalipia upasuaji na kupangiwa tarehe.

Tarehe ilipofika nikaenda MOI nikafanya kipimo cha damu kisha nikalazwa kwajili ya upasuaji wa kuwekewa chuma siku ya pili yake na nashkutu Mungu nilipata tiba fresh kabisaa na kulazwa kwa siku tano kisha nikaruhusiwa.

Sasa bana kipindi nipo hapo wodini aisee kuna watu wanaumwa kwa mateso sana unakuta mtu kavunjika nyonga, mguu, uti wa mgongo yaani hajiwezi kwa lolote na hana ndugu wala mtu yoyote yule wa kumuhudumia wala kumletea chakula.

Kuna wengine wamekaa muda mrefu hadi wamepatiwa vyeo vya mwenyekiti au katibu wa wodi.
Na mbaya zaidi wengi ni wazee watu wazima.

Aisee wenye ndugu au wazazi waliopo hospital kuweni serious kuwahudumia jamaa wanateseka na kudhalilika sana.

View attachment 2586502
Nimekaa wiki ikelu hospital kisa uvimbe aisee uliyo yaandika nimeya ona mwenyewe nikiwa nauguza mkono uliokuwa na uvimbe baada ya kufanyiwa operation .mm nikifika mahali manurse walikuwa ni marafiki zangu mana nilienda peke yangu kufanyiwa huo upasuaji ila uliyo yaandika ni ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom