GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ni tukio la kusikitisha sana. Limetokea katika Kitongoji cha Bombani, kijiji cha Dumila Mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa watoa taarifa, mwili wa mtu aliyedaiwa kufa kifo cha ghafla, ulionekana ukitoka jasho na mapigo ya moyo kupiga kwa mbali. Waliotaka daktari aitwe aje athibitishe kama kweli kafariki hawakusikilizwa. Baba mtu alikataa kwa madai kuwa mwanaye kashaaga dunia.
Cha ajabu, waliitwa wataalamu wa mila! Kwa huko, pengine, waganga wa kienyeji wanaoaminika kuliko madaktari! Inasikitisha.
Najiuliza!
Wanakijiji walishindwa kumshinikiza huyo baba akubali
mtoto wake kupelekwa hospitalini?
Uongozi wa kijiji ulishindwa kuzuia mazishi ya huyo mtu baada ya kuwepo kwa huo utata?
Hakuna uwezekano kuwa pengine aliyezikwa hakuwa amekufa bali alikuwa amezimia tu?
Hayo yametokea kwa bahati mbaya au kuna agenda ya siri nyuma yake?
Kuna umuhimu wa hiyo taarifa kufuatiliwa na vyombo husika.