Kama ni wewe ni graduate na bado hujapata ajira, basi fanya shughuli zifuatazo

Kama ni wewe ni graduate na bado hujapata ajira, basi fanya shughuli zifuatazo

Imagine umemaliza chuo kikuu,unavojifunza ufundi wa board hata kukata mbao square huwezi ,mafundi wanakuzarau sana ,vipimo unakosea kila muda,badae wanaulizana umemtoa wap huyu baada aseme sehemu flani anasema huyu humkumbuki kamaliza chuo kwahiyo yupo tu kitaa.
 
Kimbia kajifunze ufundi wa ku-design gypsum boards, tv show case outlook, outlook ya kisasa ya maduka na interior design nyingine kwa pamoja.

Kimbia kajifunze mji ulivyo, zunguka utafute nyumba, acha vipeperushi vya namba yako kuwa wewe ni dalali, kaa kitaa na wana upate dili za viwanja na vyumba, then fungua ka-ofisi mshenzi ka udalali, ukiwashirikisha na wana wengine waaminifu.

Ingia kitaa tafuta shuguli zinazofanyika, wape offer ya kuwa MC wa shughuli yao bure bila kukulipa chochote, graduation za la saba, form 4, we fanya bure , huku mwisho wa sherehe gawa vipeperushi vya namba yako na jina lako, jitangaze katika sherehe hio, then ndani ya mwaka miaka miwili ushakuwa MC wa kulipwa.

Tofauti na hapo utampelekea sana shemeji yako maji ya kuoga
Mbona unanikatisha tamaa? Yaani nirudi darasani wakati hiki nilichosomea hata sijaanza kukifaidi? Hii dunia haiko sawa kabisa
 
Mwambie Kaka ako bado tuna kinyongo.
1735736272200.jpg
 
Kimbia kajifunze ufundi wa ku-design gypsum boards, tv show case outlook, outlook ya kisasa ya maduka na interior design nyingine kwa pamoja.

Kimbia kajifunze mji ulivyo, zunguka utafute nyumba, acha vipeperushi vya namba yako kuwa wewe ni dalali, kaa kitaa na wana upate dili za viwanja na vyumba, then fungua ka-ofisi mshenzi ka udalali, ukiwashirikisha na wana wengine waaminifu.

Ingia kitaa tafuta shuguli zinazofanyika, wape offer ya kuwa MC wa shughuli yao bure bila kukulipa chochote, graduation za la saba, form 4, we fanya bure , huku mwisho wa sherehe gawa vipeperushi vya namba yako na jina lako, jitangaze katika sherehe hio, then ndani ya mwaka miaka miwili ushakuwa MC wa kulipwa.

Tofauti na hapo utampelekea sana shemeji yako maji ya kuoga
Hamna kazi hapo
 
Hali imebadilika sio kama zamani graduate walikuwa ni wachache na hawatoshi kuajiriwa. Siku hizi graduete ni wengi. Siku hizi ukisoma usitegemee kuajiriwa tu unatakiwa usome vitu hata nje ya masomo rasmi. Unasoma uchumi, sheria, udaktari, ualimu na kozi zingine lakini pia ni bora ukajifunza mambo mengine ya ujuzi hata kama hayako kwenye mfumo rasmi ili uki graduate usika idol huna shughuli ya kufanya. Graduate hutakiwi kukosa shughuli za kufanya, ziko nyingi na hazina gharama za kujifunza
Tatizo tunajifungia sana mijini na hatutaki kutoka na kwenda kutafuta. Ila hii nchi ina fursa kila sehemu. Watu tunakuwaje na ardhi alafu tukose chakufanya kweliii?.

Kuna vijiji ardhi hekari moja ni elfu 60 na bado hakuna watu wanaojilipua kwenda kutengeneza miji huko.

Hapo usiongelee utalii ndio kabisaa hii nchi ina neema sana aisee, ni vile tu tunataka vya haraka na waoga kujaribu mambo mapya. Laptop za graduates ni zakuangalia series na bando.zetu ni zakuangalia trends tiktok.
 
Napata shaka na elimu ufunguo wa maisha.Classmate wako aliishia la saba kisha akajichanganya mtaani hivi sasa ni nguli wa fani fulani.Sasa graduate ndiyo unaingia chimbo,huoni kwamba ulitapeliwa pesa kwa kupewa makaratasi yasiyokunufaisha?
 
Duuh inasikitisha
 
Back
Top Bottom