Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,072
- Thread starter
- #21
Wanatekeleza majukumu kinafiki na uogauoga.Haiwezekani ueleze kwamba mtumishi aliyejaa hofu,kutoielewa kesho,kunyanyaswa na Viongozi wa CCM,kipato duni,masimango na kila aina ya kadhia akuletee tija.Kama unaamini anakupa tija,basi ni kwa kiwango duni ambacho nacho kinaitwa kiwango.
Watumishi wengi hasa wa mahospitali, taasisi na ofisi nyingine za umma walikuwa wanatekeleza majukumu ili kulinda vibarua vyao, na hiyo ilihusisha kutoa huduma stahiki kwa wananchi. Au unaongelea wanasiasa?