KAMA NINGEKUWA MIMI.
Leo nazungumzia vijana na ajira kupitia Mikopo inayotolewa na serikali kwa vikundi vya vijana, akina mama na watu wenye Ulemavu. Utaratibu wa sasa ili kupata mkopo watu husika lazima wawe na kikundi kilichosajiliwa, baada ya hapo mchakato wa maombi ya mkopo tajwa huanza. Inapotokea kikundi kupata mkopo huo ni vikundi vichache sana vinautumia kwa malengo yaliyokusudiwa na hatimaye tija ya mkopo kutoonekana na kushindwa kurejesha mkopo huo kwa wakati.
JE, TATIZO LIKO WAPI?
JE, NINI KIFANYIKE?
Kwa Mtazamo wangu wahusika wabadilishe namna ya uendeshaji na utoaji wa mikopo hiyo kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa yaanzishwe “makambi ya Ujuzi” ya muda mfupi sana, ambayo yatatoa mafunzo kwa vitendo ya shughuli mbalimbali katika kila Wilaya ikiwezekana kata (mf kilimo, useremala, ufugaji, ujasiriamali, ushonaji, ufundi ujenzi, ufyatuaji tofali, udereva etc.) nje ya mfmo rasmi wa Veta.
Makambi haya yawe ni bure viendeshwe bila ada yoyote na iwe ni lazima kwa mtu yeyeote mwenye nguvu asiye na shughuli rasmi kwenda kujifunza ujizi mojawapo au Zaidi. Makambi haya yatoe mafunzo kupitia wataalamu wa serikali waliopo kwenye idara husika walioajiriwa na ambao wanalipwa na serkali (mf. Maafisa kilimo nk) ambao ndio watatumika kutoa ujuzi kwa vitendo kwa wanafunzi wa kambini hapo. Kutokana na uchache wa wakufunzi basi kila wilaya iwe na angalau kambi moja yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 200 kwa wakati mmoja kwa awamu moja.
JE, MAKAMBI HAYO YATAKUWA WAPI?
Kila wilaya itenge eneo lisilopungua ekari 100 kwa ajili ya kambi na eneo hilo liwe lina/liwekwe mahitaji muhimu kama maji, umeme na mahema(tents za kulala)
JE, MAFUNZO YATATOLEWA KWA MUDA GANI?
Mafunzo yatolewe kwa muda usiopungua miezi mitatu hivyo kwa mwaka kutakuwa na awamu tatu ambapo wanafunzi angalau 900 kila mwaka na kila wilaya watapata mafunzo.
JE, WANUFAIKA (WANAFUNZI) WA MAFUNZO WATAPATIKANAJE?
Kila kata itakuwa na majina ya watu wote wasio na shughuli rasmi ndani ya kata au wanashughulika lakini hawana ujuzi wa kutosha, halafu wanaundiwa makundi. Kila kundi kulingana na shughuli ya uzalishaji. Kila kundi litapangiwa muda wa kwenda kupata mafunzo. Mathalani kama ndani ya wilaya kuna kata 20, kila kata iwe na uwezo wa kupeleka makundi 2 yenye watu wa 5 kila kundi kwenye kambi ambapo awamu ya kwanza ya mafunzo ya miezi 3 kambi itakuwa na wanafunzi wasiopungua 200. Wanafunzi hao watafundishwa kambini kwa muda usiozidi miezi mitatu.
Pili, kwa wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati kabla ya kuondoka vyuon wajiunge vikundi na wasajiliwe na kulingana na ujuzi walioupata na wachague eneo la kwenda kufanyia shuguli hiyo halafu wakopeshwe ili waanze uzalishaji mara tu baada ya kuhitimu kabla hata ya kupata ajira popote. Na viongozi wa sererkali wa eneo husika wakabidhiwe makundi hayo kwa ajili ya uangalizi zaidi na support pale itakapohitajika.
JE, SASA MIKOPO MITOLEWE KWA NAMNA GANI?
Baada tu ya kuhitimu mafunzo ya ujuzi kambini serikali iwapatie mahitaji yote muhimu kulingana na shughuli ambalo kundi limejifunza ikiwa ni pamoja na eneo rasmi kule kijijin/katani wanakotoka la kufanyia shughuli pamoja na msimamizi wa kundi husika kutoka ktk idara husika(eg kilimo, biashara etc).
JE KAMBI HIZO ZITAENDESHWAJE?
Kambi zote ziwe na shughuli ya lazima ambayo ni kilimo hasa cha bustani, mboga na matunda ya muda mfupi, atakuwepo afisakilim/ougani ambaye atakiuwa kambini kwa ajili ya mafunzo ambapo mafunzo hayo yatakuwa kwa vitendo na wanafunzi watawexa kuzalisha chakula cha kutosha kulisha kambi kwa muda mfupi na baadaye kambi itakuwa na uwezo wa kujihudumia yenyewe. Hivyo gharama zitakuwa kwenye awamu ya kwanza tu ambapo ndo chakula kitakuwa bado hakijazalishwa. Baada ya hapo chakula kambini kitakuwepo cha kutosha na kingine kuuzwa kwa ajili ya huduma zingine za kambini.
NOTE
ANGALIA MHUTASARI HAPA CHINI

- Kwa mtazamo wangu:
- kuna tatizo la uelewa kwa makundi tajwa kuhusu mkopo huo.
- Vikundi vingi vinachukua mikopo bila kuwa na utaalamu wa kutosha kuhusu shughuli ambayo mkopo umekusudiwa kwenda kutumika.
- Hakuna usimamizi wa kutosha wa kitaalamu kwa shughuli za vikundi(Technical support)
- Ufuatiliaji wa mikopo hii umekuwa sio wenye tija hivyo mwanya huu kutumiwa na vikundi kutorejesha mikopo.
JE, NINI KIFANYIKE?
Kwa Mtazamo wangu wahusika wabadilishe namna ya uendeshaji na utoaji wa mikopo hiyo kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa yaanzishwe “makambi ya Ujuzi” ya muda mfupi sana, ambayo yatatoa mafunzo kwa vitendo ya shughuli mbalimbali katika kila Wilaya ikiwezekana kata (mf kilimo, useremala, ufugaji, ujasiriamali, ushonaji, ufundi ujenzi, ufyatuaji tofali, udereva etc.) nje ya mfmo rasmi wa Veta.
Makambi haya yawe ni bure viendeshwe bila ada yoyote na iwe ni lazima kwa mtu yeyeote mwenye nguvu asiye na shughuli rasmi kwenda kujifunza ujizi mojawapo au Zaidi. Makambi haya yatoe mafunzo kupitia wataalamu wa serikali waliopo kwenye idara husika walioajiriwa na ambao wanalipwa na serkali (mf. Maafisa kilimo nk) ambao ndio watatumika kutoa ujuzi kwa vitendo kwa wanafunzi wa kambini hapo. Kutokana na uchache wa wakufunzi basi kila wilaya iwe na angalau kambi moja yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 200 kwa wakati mmoja kwa awamu moja.
JE, MAKAMBI HAYO YATAKUWA WAPI?
Kila wilaya itenge eneo lisilopungua ekari 100 kwa ajili ya kambi na eneo hilo liwe lina/liwekwe mahitaji muhimu kama maji, umeme na mahema(tents za kulala)
JE, MAFUNZO YATATOLEWA KWA MUDA GANI?
Mafunzo yatolewe kwa muda usiopungua miezi mitatu hivyo kwa mwaka kutakuwa na awamu tatu ambapo wanafunzi angalau 900 kila mwaka na kila wilaya watapata mafunzo.
JE, WANUFAIKA (WANAFUNZI) WA MAFUNZO WATAPATIKANAJE?
Kila kata itakuwa na majina ya watu wote wasio na shughuli rasmi ndani ya kata au wanashughulika lakini hawana ujuzi wa kutosha, halafu wanaundiwa makundi. Kila kundi kulingana na shughuli ya uzalishaji. Kila kundi litapangiwa muda wa kwenda kupata mafunzo. Mathalani kama ndani ya wilaya kuna kata 20, kila kata iwe na uwezo wa kupeleka makundi 2 yenye watu wa 5 kila kundi kwenye kambi ambapo awamu ya kwanza ya mafunzo ya miezi 3 kambi itakuwa na wanafunzi wasiopungua 200. Wanafunzi hao watafundishwa kambini kwa muda usiozidi miezi mitatu.
Pili, kwa wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati kabla ya kuondoka vyuon wajiunge vikundi na wasajiliwe na kulingana na ujuzi walioupata na wachague eneo la kwenda kufanyia shuguli hiyo halafu wakopeshwe ili waanze uzalishaji mara tu baada ya kuhitimu kabla hata ya kupata ajira popote. Na viongozi wa sererkali wa eneo husika wakabidhiwe makundi hayo kwa ajili ya uangalizi zaidi na support pale itakapohitajika.
JE, SASA MIKOPO MITOLEWE KWA NAMNA GANI?
Baada tu ya kuhitimu mafunzo ya ujuzi kambini serikali iwapatie mahitaji yote muhimu kulingana na shughuli ambalo kundi limejifunza ikiwa ni pamoja na eneo rasmi kule kijijin/katani wanakotoka la kufanyia shughuli pamoja na msimamizi wa kundi husika kutoka ktk idara husika(eg kilimo, biashara etc).
JE KAMBI HIZO ZITAENDESHWAJE?
Kambi zote ziwe na shughuli ya lazima ambayo ni kilimo hasa cha bustani, mboga na matunda ya muda mfupi, atakuwepo afisakilim/ougani ambaye atakiuwa kambini kwa ajili ya mafunzo ambapo mafunzo hayo yatakuwa kwa vitendo na wanafunzi watawexa kuzalisha chakula cha kutosha kulisha kambi kwa muda mfupi na baadaye kambi itakuwa na uwezo wa kujihudumia yenyewe. Hivyo gharama zitakuwa kwenye awamu ya kwanza tu ambapo ndo chakula kitakuwa bado hakijazalishwa. Baada ya hapo chakula kambini kitakuwepo cha kutosha na kingine kuuzwa kwa ajili ya huduma zingine za kambini.
NOTE
- BAADA YA MAFUNZO (MIEZI 3) KILA KATA ITASAJILI KIKUNDI RASMI KWENYE MFUMO WA SERKALI NA KUOMBEWA ENEO NA MKOPO KWA AJILI YA KUANZA SHUGHULI RASMI CHINI YA USIMAMIZI WA HALMASHAURI NA KILA KUNDI LITAJIKITA KWENYE AINA MOJA TU YA ZAO WATAKALOCHAGUA ILI KURAHISISHA UHAKIKA WA SOKO
- MAZAO YA CHAKULA YALIYOMENGI YATAKUWA KWA AJILI YA CHAKULA KTK ENEO LA MAFUNZO ZIADA NDIYO ITAKAYOUZWA
- MAZAO YA BIASHARA KAMA PARACHICHI, ALZETI ETC AFISA BIASHARA NA MASOKO ATAPEWA JUKUMU LA KUTAFUTA WADAU WA KUINGIA NAPO MKATABA NA KUHUDUMIA VIKUNDI HUSIKA KUZALISHA KULINGANA NA UBORA UNAOHITAJIKA KWA KAMPUNI AU MFANYABIASHARA HUSIKA.
- HALMASHAURI PIA ITAANZISHA SUPERMARKET KWA AJILI YA KUUZIA BIDHAA ZITAKAZO KUWA ZIMEONGEZEWA THAMANI NA ZINAHITAJIKA KWA MATUMIZI YA WILAYA HUSIKA ILI KUUZWA HUMO, KUANZISHA VIWANDA KAMA CHA JUICE CHA HALMASHAURI AMBAPO MATUNDA YATAKAYOKUWA YANAZALISHWA YATAWEZA KUUZWA HAPO PAMOJA NA VIWANDA VINGINE KULINGANA NA SHUGHULI ZA VIKUNDI.
- KILA KIJANA NDANI YA WILAYA HUSIKA ASIYE NA SHUGHULI RASMI YENYE KUMUINGIZIA KIPATO LAZIMA APITIE MAFUNZO NA AWE NA ANAUWEZO WA KUZALISHA BIDHAA KULINGANA NA MAHITAJI YAKE
- KITUO KITAKUWA ENDELEVU NA BAADAE KINAWEZA KUENDEL NEZWA KWA KUWEKEWA MIUNDOMBINU YA KUDUMU NA KUONGEZA AINA ZINGINE ZA UJUZI KWA KADRI ITAKAVYOFAA
ANGALIA MHUTASARI HAPA CHINI
| WANUFAIKA WA MAKAMBI |
| ||||||||||||
| MSIMAMIZI MKUU WA KAMBI | MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA HUSIKA | ||||||||||||
| MRATIBU WA KAMBI | AFISA MAENDELEO YA JAMII WA WILAYA HUSIKA | ||||||||||||
| WAKUFUNZI WA KAMBI | WATAALAMU KUTOKA IDARA TOFAUTI ZA NDANI YA HALMASHAURI HUSIKA(KUTEGEMEANA NA SHUGHULI AMBAYO KITUO KINAJISHUGHULISHA) | ||||||||||||
| LENGO KUU LA KAMBI | Kuwezesha kila kijana awe na shughuli inayomuingizia kipato halali(yeye mwenyewe au ktk kikundi) hasa kwa vijana ambao hawana kipato cha kuendelezwa kielimu na wazazi wao au wanaopata changamoto mbalimbali katika safari ya mfumo rasmi wa masomo na hawako tayari kurudi shule kwa sababu ya umri na muda au hawana uwezo wa kumudu masomo ya darasani | ||||||||||||
| MALENGO MAHUSUSI | kutoa mafunzo /ujuzi kwa vitendo
| ||||||||||||
NA MWANDISHI WENU
HALAKEYE
HALAKEYE
Upvote
0