instagramer
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 215
- 492
Habari Wadau Wa Jukwaa Hili...
Kuweka kumbukumbu sawa, Mimi ni mmoja wa vijana wa kitanzania niliyesoma katika shule za Serikali kuanzia elimu ya msingi, sekondari mpaka chuo, hivyo mawazo nitakayotoa hapa yasiyafsirike kupinga shule za Serikali.
Kwa muda mrefu nimekua nikiwaza namna ya kufikisha ushauri wangu huu kwa Serikali. Kwa kuzingatia mahitaji na ukuaji wa Jiji letu la Dar es salaam Kiuchumi.
Hivi Serikali yetu Haioni umuhimu kwa Sasa wa kubomoa shule zake zote za msingi na hata sekondari ambazo zipo katikati ya Jiji??? Hizo shule nyingi zimekua kongwe na za kizamani Sana, na siamini kama zinaachwa kwa ajili ya kutunza historia.
Serikali izivunje ili maeneo hayo yajengwe maghorofa ya Kisasa kwa ajili ya shughuli za kibiashara. Kwa maana wakati shule hizi zinajengwa miaka ya zamani, basi maeneo hayo walikaa watu wa kipato Cha chini au Cha kawaida, ambao ndio wanufaika wa shule hizo. Ila watu hao kwa Sasa wapo nje ya Jiji na sio katikati tena kama zamani. Mfano, shule ya msingi Mtendeni, zamani wanafunzi walikua ni wakazi wa Kariakoo ambao kwa Sasa wanaoishi maeneo hayo asilimia kubwa ni matajiri ambao watoto wao Wanasoma shule zenye ma'bus.
Hivyo kwa mfano huo wa Mtendeni Pekee, unaweza Kuta wanafunzi wake wanatoka maeneo ya mbali kabisa ambapo wanakumbana na changamoto ya usafiri na suluba za hapa na Pale wakati huko huko walipo Kikwete alishapeleka shule nyingi tu za kata.
Je kwa mawazo haya, Serikali Haioni umuhimu wa kuvunja shule zote hizo na kubadili matumizi ya ardhi????
CC: Waziri wa elimu
Waziri wa ardhi
Spika wa Bunge