Kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mzee mbona unataka kutulazimisha kuamini vitu Ambazo siyo.....
Yaani ikiambiwa useme Russia, china ni nchi za kijamaa. Utataja Duh!!! Aibu kubwa sana...
Mkuu sitaki porojo nataka ushaidi wa SERA za nchi hizo ili tujue kama ni za kijamaa au kibepari.
 
Naona porojo zimekua nyingi.Mimi ninachohitaji ni SERA.Ujamaa ni mfumo mpana ndio maana kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa historia utaona katika sera ujamaa kila nchi ilikua na siasa ya namna yake mfano Tanganyika ni ujamaa na kujitegemea, harambee-kenya,humanism -Zambia n.k

Ukweli ni kwamba sisi Waafrika tulishindwa kupanga kimakati ya kimaendeleo kupitia ujamaa.Ndio maana Tanzania ujamaa ulikufa tangu enzi za Mwinyi japokua katiba inasema ujamaa ila hii nchi inaongozwa kibepari.

China na Russia ni nchi zilizopitia masaibu ya ujamaa na hatimaye zikafikia malengo yake ya kimkakati ya kimaendeleo kupitia ujamaa.

Tatizo hapa hamjui ujamaa ni nini.Ujamaa sio constant kama ubepari bali ujamaa unajidhihirisha kulingana na sera za serikali husika katika kufikisha mahitaji ya wananchi wake huku wananchi wakinufaika zaidi kupitia hizo huduma.

Ushaidi ni huu kuhusu kitengo cha afya cha Urusi na China,angalia ni kwa asilimia ngapi wananchi wanapata matibabu bure alafu linganisha na Marekani ambayo huduma za afya ni most expensive na japokua Kuna hospitali za serikali,ni lazima kulipia.Vilevile linganisha na Tanzania kama matibabu ni bure,je kuna huduma bora?Kuna vifaa?Lakini angalia hospitali binafsi zinavyotoa huduma bora kuizidi serikali.Ndio ujue Tanzania hakuna ujamaa.

Vilevile pitia historia katika kitengo hiko cha afya kwa nchi zote mbili utaona kua wakati USSR inakufa baada ya muda kidogo Urusi ilipokea privatization policy katika kitengo cha afya.Je hiyo policy ilidumu?Kwa nini haikudumu?Kwa nini mpaka sasa mwaka 2022 hapo Urusi kuna hospitali binafsi(ambazo ni chache) lakini serikali bado inatoa huduma nzuri za kiafya ambazo ni bure na bora .Ndio utajua hujui Ujamaa ni nini.

Vilevile angalia na China na katika kitengo cha afya.NDIPO UTAKAPOGUNDUA UJAMAA UNANGUVU YA KUMSAIDIA MWANANCHI MASIKINI TATIZO NI SISI WAAFRIKA TUSIO NA AKILI NA MAARIFA YA KUBUNI MIFUMO CHINI YA UJAMAA.USISINGIZIE UJAMAA WAKATI HAUNA AKILI YA KULETA MAENDELEO.HUKO CHINA NA URUSI KUNA TAASISI BINAFSI LAKINI WANUFAIKA WAKUBWA NI WANANCHI WENYEWE LAKINI SISI HUKU TUNANYONYWA KILA KUKICHA KUPITIA UBEPARI.KWANZA NINYI NYOTE MNAOSEMA TANZANIA INAONGOZWA KWA SERA YA UJAMAA NI WAJINGA TU,HAMJUI UJAMAA NI NINI.SIKATAI KATIBA INASEMA NCHI IPO CHINI YA UJAMAA,JE UNAFUATWA?ACHENI KUA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU.
 

Attachments

Wewe una miaka 17 tu, haya mambo yako juu ya uwezo wako, jikite na shule kwanza kwa sasa ukifikisha miaka 22 ndio urudi hapa
 
Mleta uzi ni mtoto wa miaka 17
 
Mleta uzi ni mtoto wa miaka 17
Mkuu umri sio kipimo cha akili ya mtu.Kuna wazee hawana busara na kuna vijana wana hekima.Miaka ni namba tu,Marekani mtu akifikisha 16 tayari mkubwa hapa Tanzania mpaka 18,sababu nini?Akili au kujitambua hakuendani na miaka as long as nishabalehe na nina uwezo wa kumtungisha mwanamke mimba ubongo umetanuka kwa kufiria mambo ya msingi.
 
Ndio nyie ambao mkiwa viongozi hamtaki kushauriwa na vijana mkidhani vijana hawana wanachojua.Alisikika ... akimuambia Furaha,mjomba wake"wewe kijana niletee mambo kuhusu ukemia nitakuelekeza lakini haya mambo ya siasa..."
 
Mkuu kuna kitu kimoja unashindwa kuelewa Sera zote ujamaa au ubeapari ni nzuri-issue kubwa ni ngoma inachezwa kipindi kipi?.

Kumbuka kabla USA hajawa superpower Russia ndio alikuwa superpower,sasa ulitaka USA baada ya kiwa super power aendelee na sera ya Ujamaa ambayo ilikuwa ya mtangulizi wake (USSR)??,it is obviously lazima aanzishe mfumo wake wa uchumi na utawala.

Ndio maana walikaa chini na kuanzisha mifimo hiyo ili kuhakikisha wanaendelea kuwepo katika nafasi hiyo.

Maono yako yanawezekana kama Tanzania ingekuwa Taifa kubwa kama Urusi au China na upo next kuchukua nafasi ya USA kama superpower wa Dunia.

Kwa Nchi kama yetu ambayo Mifumo ya uchumi na siasa,ya magharibi tupo katika makwapa huwezi kuchomoka ukiwa peke yako.

Njia pekee ya kuondokana na mfumo huo ungewezekana kama Africa nzima ingeungana na kuwa Tiafa mmoja-Nyerere alilona hilo na ndio alijaribu kulipigania mpaka anakufa halikuwezekana,sababu kubwa ni kqamba hao western kwa njia yoyote wanahakikidha hilo haliyokei.

Kama unataka kutekeleza hayo maono yako,anza kwanza na kuiunganisha Afrika yote.
 
Umeongea kwa utimamu mkuu.Hoja nzuri 👏🏽.
 
Urusi na China sio nchi za kijamaa, Korea Kaskazini ni nchi ya ujamaa uchwara ambayo Kiduku na kikundi chake kidogo wanatumia mkono wa chuma kunyonya jasho la raia watawaliwa waliobaki mafukara na skelton tupu.
Cuba
 
Sijawahi kufika na wala sijui lolote lakini nasikia marekani kuna hadi chakula cha bure kwa wasiojiweza. Kama hilo wanalifanya, wataacha huduma ya afya kwa wazee kweli?!!! Halafu vp kuhusu hili la maeneo maalumu ya kutunza wazee?!!!!!
 
Nje ya mada, kwanini wachina wengi wanakimbilia ulaya na marekani?!!!!
 
Nje ya mada, kwanini wachina wengi wanakimbilia ulaya na marekani?!!!!
Toa ushaidi.Unaandika pasipo any attachments unategemea nikuone great thinker without vivid explanations.
 
Sijawahi kufika na wala sijui lolote lakini nasikia marekani kuna hadi chakula cha bure kwa wasiojiweza. Kama hilo wanalifanya, wataacha huduma ya afya kwa wazee kweli?!!! Halafu vp kuhusu hili la maeneo maalumu ya kutunza wazee?!!!!!
Fuatilia.
 
Rubbish,kama unataka ujamaa mbona hauufanyi hapo mtaani kwako?

Kwani kuwa mjamaa kunahitaji hadi uwe Rais? Acha kukariri makaratasi wewe kiazi..

Walioasisi ujamaa uliwashinda,walipiga kama akina Nyerere uliwashinda ndio uje kuweza wewe maskini wa huko nanjilinji?

Ujamaa ni Imani kama Imani zingine na lazima uishi hivyo wala haotegemei hadi uwe Rais.
 
Ukiandika kama great thinker nitakujibu.
 
Mvua zimeanza, nenda kaoteshe mahindi upate tiba ya kuwalisha wanao na kuwasomesha!
Achana na hadithi zako za abunuwasi, hata M.kiti wa kitongoji sio rahisi wewe kupata!
 
Njoo upime wazo lako kwenye Game hii ya president simulator

Game hii ina Kupa Fursa ya kuendesha inch
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…