Hata hayo maswali ndo mimi na jiuliza, na kama endapo evolution ilikua labda sio wote tuwe binadamu ni kwanini ndugu zetu nyani tuwaache / wasibadilike?
Kwanza kabisa hatukuwaacha nyani ambao hawakubadilika.
Watu wengi wanafanya makosa ya kufikiri kuwa evolution inasema zamani tulikuwa sawa na hawa nyani wa sasa, sisi tumebadilika wao hawajabadilika.
Hivyo si evolution inavyosema. Wote tumebadilika. Ila tulikuwa na a common ancestor ambaye alikuwa more ape like, maana yake sisi tumebadilika zaidi.
Kwa mujibu wa evolution.
Evolution inakwenda kwa natural selection. Kuna mazingira fulani yanafanya species fulani zife, nyingine ziendelee kuwapo, nyingine zibadilike.
Kwa mfano, kwenye mazingira ya misitu, wanyama wanaofanana na misitu ile wanaweza kupata advantage ya kuwa camouflaged wakaendelea kuwapo, na wasio na rangi ya hiyo misitu kuwindwa kirahisi na kutoweka, matokeo yake baada ya vizazi vingi wanyama wenye rangi isiyo na advantage ya camouflage watatoweka na wale wanaofanana na msitu wataongezeka na kuwa ndiyo watawala.
Kitu kingine ambacho ni kigumu kuelewa ni kuwa, kwa mujibu wa theory ya evolution, evolution inatokea katika mamilioni na malaki ya miaka, mabadiliko madogo madogo yanalimbikizana na kusababisha mabadiliko makubwa.
Sasa watu wengi wanaohoji evolution wanahoji kama vike wanataka kuona mabadiliko katika umri wao, miaka 30, miaka 50.
Ukitaka kuona evolution katika muda nfupi usiangakie wanyama wakubwa kama sokwe, nyani au watu. Ukitaka kuangalia evolution katika muda nfupi angalia vidudu kama bacteria, virus.
Angalia kitu kinaitwa anti-biotic resistance na jinsi bacteria wanavyojenga resistance dhidi ya dawa.
Unajua kwa nini hospitali hawatumii tetracycline tena? Unajua kwa nini madawa ya zamani ya malaria hayatibu tena malaria inabidi tutumie madawa mapya?
Hiyo ni evolution. Vidudu vimejipanga kuweza kujikinga na dawa, vime evolve.
Ukitaka kuelewa evolution usiangakie nyani na watu, angalia jinsi bactwria na microorganism nyingine zinavyojenga resistance dhidi ya dawa, na kwa nini tunahitaji dawa mpya, kwa nini zamani magonjwa kama gono yalikuwa yanatibiwa na tetracycline lakini siku hizi kuna gononsugu halisikii dawa.
Vidudu vya gono vimefanya evolution.