Kama ombi la Profesa Kabudi litakubaliwa huko UNESCO basi tarehe 07 Julai kila mwaka itakuwa ni Siku ya Kiswahili Duniani

Kama ombi la Profesa Kabudi litakubaliwa huko UNESCO basi tarehe 07 Julai kila mwaka itakuwa ni Siku ya Kiswahili Duniani

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi ameiomba UNESCO kukitambua rasmi Kiswahili kama lugha ya mawasiliano duniani na kwamba itangaze tarehe 07 Julai ya kila mwaka kuwa ni Siku ya Kiswahili Duniani.

Hili ni jambo jema, tuombe Mungu alibariki ombi hili.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Mara utasikia Prof. Kabudi ameenda UNESCO kuomba chato iingizwe kwenye "URITHI WA DUNIA". Hii nchi watu wana changanyikiwa uzeeni.

Badala viongozi wakae na kushauriana jinsi ya kuokoa roho za raia wao kwenye hili janga la Covid. Raia wanakufa kila siku, Raia kila siku wanaugua na kukimbizana hospital, Raia wanapoteza watu muhimu katika familia zao. Viongozi wanakaa kushauriana upuuzi upuuzi tu.

Nchi za wenzetu maambukizi yanashuka asilimia kila week, kwasababu ya kutilia mkazo tahadhari za kisayansi. Sisi ndio kwanza yanaongezeka, mpaka tukifikia peak ya maambukizi nchini wenzetu watakua wameitokomeza Covid. Halafu watakaa kututazama tu tuki tapa tapa kama kondoo waliopotea zizi.
 
Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi ameiomba UNESCO kukitambua rasmi Kiswahili kama lugha ya mawasiliano duniani na kwamba itangaze tarehe 07 July ya kila mwaka kuwa ni Siku ya Kiswahili Duniani.

Hili ni jambo jema, tuombe Mungu alibariki ombi hili.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Saba saba tumuachie nani?
 
Mataga mlivyowajinga hapo mnaona kiswahili ni Mali ya CCM
Siku ya kuzaliwa TANU, Julai 7 baadaye ikageuzwa siku ya wakulima Tanzania ndio wanataka iwe siku ya Kiswahili duniani.

Wanaharakati duniani kote pingeni ujinga huu. Kiswahili sio mali ya CCM; ni mali ya dunia itafutwe siku huru isiyomtukuza shetani.
 
Waziri wa mambo ya nje Prof Kabudi ameiomba UNESCO kukitambua rasmi Kiswahili kama lugha ya mawasiliano duniani na kwamba itangaze tarehe 07 July ya kila mwaka kuwa ni Siku ya Kiswahili Duniani.

Hili ni jambo jema, tuombe Mungu alibariki ombi hili.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Kwa hiyo tutakuwa tunaadhimisha siku ya Kiswahili Duniani? Au tutabaki kusherehekea kwenye maonesho ya Kilele cha Biashara?
 
Yani Mambo ya kijingajinga ndio mnayamudu 😪😫😫😒😒😏
His Excellence alikua anasisitiza matumizi ya kiswahili kwa kutumia huno hunmo na maneno ya kiingeereza, stupidity at its best
 
Hilo upo Sawa ila wangapi mnaofahamiana wanaokijua kichina?
Wote wenye interest na maslahi ya biashara, elimu, tiba au sanaa ambao nawajua kama hawakijui basi wanajifunza au hata wanatamani kukijua

Kwa maana wanathubutu hata kujaribujaribu kujifunza semi muhimu kama salam, maulizo, kama vile kuomba msaada wa njia au maelekezo mablimbali
 
Back
Top Bottom