Kama pesa ya Mwanamke hainihusu, kampeni ya kataa ndoa ni halali sababu inakuwa utapeli

Kama pesa ya Mwanamke hainihusu, kampeni ya kataa ndoa ni halali sababu inakuwa utapeli

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Huu upuuzi Kila siku naukataa,kama Pesa ya Mwanamke Hainihusu yupo hapo Kwa Ajili ya nini hasa?

Hicho kinachoitwa ndoa ni Cha maana gani ikiwa kinaleta unyonyaji Kwa Mwanamke? Si Bora niwe nahonga na kula mzigo Kwa kununua kuliko huu ujinga unatetewa hapa?

======
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Njombe Wilferdy Willa ameitaka Jamii Mkoani humo hususani Wanaume kutambua kuwa fedha inayotafutwa na Mwanamke aliye kwenye ndoa ni ya kwake binafsi lakini fedha inayotafutwa na Mwanaume ni ya Familia jambo ambalo litasaidia kutatua migogoro ya ndoa.

Willa amesema hayo katika semina kwa Viongozi iliyoratibiwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Njombe ambapo amesema ni vema Wanaume wakatambua majukumu yao katika Familia kama inavyoeleza sheria ya ndoa kwakuwa itasaidia kupunguza migogoro kwenye ndoa.

Willa amesema Wanaume wengi kwenye ndoa hudhani pesa inayotafutwa na Mwanamke ndani ya ndoa ni ya Familia (wote) jambo ambalo sio sahihi kwa mujibu wa sheria ya ndoa badala yake Mwanamke ana wajibu wa kuwajibika kupitia fedha yake endapo tu Baba hayupo, amefariki au hawezi kutekeleza majukumu kwa wakati huo.

"Mwanaume au Mwanamke ukijua majukumu yako kwenye Familia hakutakuwa na kelele, ukisoma sheria ya ndoa inasema Baba atawajibika kuhakikisha Familia yake inakuwa na ustawi na Mwanamke atafanya majukumu ya Baba kama Baba hayupo au hana uwezo wa kutekeleza majukumu kwa wakati huo, kwahiyo fedha inayotafutwa na Mwananke ni ya kwake na inayotafutwa na Mwanaume ni ya Familia"
 
Huu upuuzi Kila siku naukataa,kama Pesa ya Mwanamke Hainihusu yupo hapo Kwa Ajili ya nini hasa?

Hicho kinachoitwa ndoa ni Cha maana gani ikiwa kinaleta unyonyaji Kwa Mwanamke? Si Bora niwe nahonga na kula mzigo Kwa kununua kuliko huu ujinga unatetewa hapa?

Hayo ni maoni yake sio sheria. Sheria,inasema mali iliyochumwa ndani ya ndoa itagawanywa kwa wawili hao. Sema wanaume wanapopelekwa mahakamani jwa talaka huwa hawang' ang'anii mali ya mke igawanywe lakini sheria inaruhusu hilo.
 
Ni ujinga Sasa Kwa nini zako zigawanywe harafu za mwanamke uziache? Mimi sio tayari kama ninajua ni za Mwanamke..

Lakini Mali ya Mwanamke ikindikwa Kwa jina lake inakuaje hapo?
 
Huu upuuzi Kila siku naukataa,kama Pesa ya Mwanamke Hainihusu yupo hapo Kwa Ajili ya nini hasa?

Hicho kinachoitwa ndoa ni Cha maana gani ikiwa kinaleta unyonyaji Kwa Mwanamke? Si Bora niwe nahonga na kula mzigo Kwa kununua kuliko huu ujinga unatetewa hapa?

Katibu wa Chama cha KATAA NDOA nakukaribisha chamani Kwa niaba ya mwenyekiti wetu Liverpool vpn
 
Ni ujinga Sasa Kwa nini zako zigawanywe harafu za mwanamke uziache? Mimi sio tayari kama ninajua ni za Mwanamke..

Lakini Mali ya Mwanamke ikindikwa Kwa jina lake inakuaje hapo?
Ni popoma pekee ndiye ataruhusu upumbavu huo wa kuandika mali kwa jina la Ke.

Achraf Hakimi hajakuwa tu case study kwenu ninyi Wavulana?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom