Mkuu mimi simuumini wa ubaguzi , na kwaimani yangu sikuwahi kufundishwa faida za ubaguzi ila tuuseme ukweli mkuu hata ukiingia tu huko mitandaoni tena hata kabla ya hili halijatokea katika watu ambao walikuwa watetezi wakubwa wa Mama basi ni hiyo jamii (narudia tena sorry) maana sinufaiki na kitu kwa kuwaweka kwenye kundi ovu lakini ukweli uko hivyo , na siyo wao tu ,kimsingi CCM walitutangulia kwa kutupandikizia mbegu ya udini na ndiyo iliyokuwa imeota , watetezi wakubwa wa Mama walikuwa watu wenye imani ya kiislam (nadhani pengine ndiyo eneo kundi la watu wa Zanzibar lilipoingilia)
More over, ukitaka kuelewa naongea nini jirudishe nyuma kisha uangalie maeneo yaliyokutana na hii kadhia , utagundua kuwa maeneo yenye waislaam wengi kama Tanga , Mtwara Pwani Mtwara na Lindi nimiongoni mwa maeneo ambayo raia wake hawajakutana kabisa na hiyo kadhia ,kwanini? Kwasababu ilipandwa mbegu ya udini na ikamea .
Issue ya Uzanzibar hiyo haiepukiki na siyo dhambi kwa mtu kujisikia furaha kwa mtu wa kwao kuwa kwenye nafasi fulani ,hiyo ni tabia ya asili ila pia kwenye kujisikia furaha kwa kilichotokea Bara hilo nalo nilakawaida kabisa siunajua tena maumivu ya msiba wa jirani na wakwako maumivu hutofautiana .
Kuhusu Zanzibar kupeleka msaada GAZA ,hilo nilakawaida kabisa kwa watu wanaoshabihiana kiimani na siyo kipimo cha watu waliyojaaliwa na mioyo ya upendo na haki .
Ubaguzi upo na hauwezi kuisha ila kwenye haya hatupaswi kuyaonea haya TUUNGANE KUYAKEMEA , tusimame kwa pamoja kama Taifa, ni mambo yasiyo na afya kwenye jamii zetu .