Kama Rais anachaguliwa na wananchi, Spika wa bunge anachaguliwa na wabunge, kwanini Jaji mkuu asichaguliwe na majaji?

Kama Rais anachaguliwa na wananchi, Spika wa bunge anachaguliwa na wabunge, kwanini Jaji mkuu asichaguliwe na majaji?

Hii nchi katiba yetu haieleweki. Vi vyeo juu ya vyeo na kuteuana tu. Yaani tuna makamu wa Rais halafu tuna waziri mkuu na naibu waziri mkuu. Kule Zanzibar wana makamu wa kwanza na wa pili wa Rais. Ujinga mtupu
 
Tume ya utumishi wa mahakama ndio inapendekeza majina kwa Rais , nae anateua katika wale alioletewa.

Hajiteulii tu mwenyewe anavyojisikia.
 
Kama kuna mhimili wa dola unaodharaulika, kutumiwa vibaya na kudhoofishwa basi mhimili wa mahakama ndio kinara.

Sijaona mantiki kwa nchi yenye mihimili rasmi ya dola mitatu inayojitegemea, yaani Rais (serikali), bunge na mahakama, halafu Rais kwa mamlaka yake awe ndio anayeteua mkuu wa mhimili wa mahakama, yaani Jaji Mkuu.

Ni kwanini mhimili wa mahakama usiwe na utaratibu wake wa kumchagua kiongozi wake mkuu, yaani Jaji Mkuu?
Kwanini nafasi ya jaji mkuu isigombewe na kupigiwa kura na majaji wenyewe?
Rais hateui jaji moja kwa moja bali tume ya utumishi wa mahakama (JSC) ndiyo huteua na kupendekeza majina matatu kutoka miongoni mwa majaji wa rufani na kuwasilisha kwa Rais kwa ajili ya kuidhinisha jina moja kati ya hayo aliyowasilishiwa.

Nitajie nchi moja tu unayoijua wewe ambayo jaji mkuu hateuliwi na Rais.
 
Yes, kuna baadhi ya nchi, kabla hajatajwa hadharani, taasisi zote za usalama na kimadili zinapaswa kum-clear then inabaki mjadala kati ya raisi na uongozi wa juu wa Bunge, endapo mmoja wao atapinga na akawa na hoja yenye mashiko, raisi hawezi kulazimisha, anarudi ubaoni kutafuta mwingine.

Kwetu, si ajabu akateuliwa hata graduate, kisha masaa kadhaa kabla ya kuapishwa akatenguliwa.
Huo ndo ukweli, Watawala wengi huwaweka wanasheria mfukoni ili watawale vizuri bila kelele, Magufuli alikaa na huyu jaji miezi 8 bila kumthibitisha eti anakaimu, wakati nafasi ya Jaji Mkuu haikaimishwi, ulikua udhaifu wa kudharau Mhimili wa Mahakama, sulaa la bandari ,viongozi waandamizi walipanga sana , Hangaya akaanza kuwala vichwa watumishi wa Ikulu, akatafuta wanasheria wake wapindeshe sheria mkataba ukapitishwa chapu warabu wakachukua chao.

Hii mihimili ikiwa na balance sawa hata suala la katiba mpya ,masuala ya uchaguzi yangekua yamepata ufumbuzi.

Kinga ya majaji ni kuwa hawatumbiliwi kirahisi kama viongozi wengine
 
Rais hana mamlaka ya kuteua Jaji Mkuu isipokuwa ataidhinisha jina moja miongoni mwa majina ya Majaji wa mahakama ya rufani aliyopelekewa.
 
Kama kuna mhimili wa dola unaodharaulika, kutumiwa vibaya na kudhoofishwa basi mhimili wa mahakama ndio kinara.

Sijaona mantiki kwa nchi yenye mihimili rasmi ya dola mitatu inayojitegemea, yaani Rais (serikali), bunge na mahakama, halafu Rais kwa mamlaka yake awe ndio anayeteua mkuu wa mhimili wa mahakama, yaani Jaji Mkuu.

Ni kwanini mhimili wa mahakama usiwe na utaratibu wake wa kumchagua kiongozi wake mkuu, yaani Jaji Mkuu?
Kwanini nafasi ya jaji mkuu isigombewe na kupigiwa kura na majaji wenyewe?
Wewe unajielewa sana! Duniani mahakama zilizo huru jaji mkuu huchaguliwa na majaji wa mahakama ya rufaa! Ila ccm eti rais anateua jaji mkuu, kwa nini mhimili mwingine utawale mhimili mwingine? Upuuzi mkubwa sana!
 
Utaratibu huu una hatari kwa sababu itapunguza impartiality ya Majaji na kuunda makundi. Ukinipa kura nakupa hiki, na kuna uwezekano siasa nje ya muhimili zikaingia na kuivuruga mahakama
Waza tofauti pia.
Rais kukaa chini chumbani na mkewe/mumewe na kututeulia Jaji mkuu kuna faida gani kwa mhimili wa mahakama ikiwa atateua jaji yoyote kwa utashi wake kuwa jaji mkuu kuliko majaji wenyewe kuamua kwa kura nani awe jaji mkuu.

Huyo mteule wa Rais atawajibikaje kwa mhimili wa mahakama ikiwa hakuwa chaguo lao.
Uhuru wa mhimili wa mahakama unatokeaje ikiwa mkuu wa huo mhimili anateuliwana na mkuu wa mhimili mwingine?
 
Rais hana mamlaka ya kuteua Jaji Mkuu isipokuwa ataidhinisha jina moja miongoni mwa majina ya Majaji wa mahakama ya rufani aliyopelekewa.
Umemsikia juzi Rais Samia alivyozungumza kuhusu kutokutaka kumuongezea muda jaji mkuu wa sasa baada ya jaji wa sasa kufikia umri wa kustaafu?

Unakumbuka Kikwete alivyomuongezea muda Jaji Othman Chande baada ya kustaafu?

Wewe fahamu tu, jaji mkuu anateuliwa na Rais, na akiteuliwa na Rais hakuna mamlaka nyingine yoyote inaweza kuhoji, kupinga au kutengua.
 
Waza tofauti pia.
Rais kukaa chini chumbani na mkewe/mumewe na kututeulia Jaji mkuu kuna faida gani kwa mhimili wa mahakama ikiwa atateua jaji yoyote kwa utashi wake kuwa jaji mkuu kuliko majaji wenyewe kuamua kwa kura nani awe jaji mkuu.

Huyo mteule wa Rais atawajibikaje kwa mhimili wa mahakama ikiwa hakuwa chaguo lao.
Uhuru wa mhimili wa mahakama unatokeaje ikiwa mkuu wa huo mhimili anateuliwana na mkuu wa mhimili mwingine?
Marekani kwa baba wa demokrasia, Rais anateua Jaji Mkuu
 
Utaratibu huu una hatari kwa sababu itapunguza impartiality ya Majaji na kuunda makundi. Ukinipa kura nakupa hiki, na kuna uwezekano siasa nje ya muhimili zikaingia na kuivuruga mahakama
Huo ni uoga tu
Mhimili wenye misingi ya kimaadili kama huo huwezi kuleta mgongano wa kimaslahi hata kidogo, kumbe Kenya inawezekana, Uganda inawezekama

Uganda Jaji Mkuu au Jaji Mkuu Msaidizi anapendekezw na Tume ya Mahakama
then Bunge linaidhinisha na mwisho Rais anateua.

Kenya Pia Tume ya Mahakama inateua then Bunge hlf mwisho Rais anateua,
Hapa Tz Tume ya Mahakama inapeleka jina kwa Rais, Rais anateua , Jaji hathibitishwi popote. Sauti ya Maamuzi hana...Mahakama ilitakiwa ijitegemee kibajeti kama ilivyo Bunge na Serikali, Mahakama kuwa ombaomba kwa Serikali ndo maana inadharaulika
 
Ata Spika anachaguliwa na Rais, wabunge wanasherehesha tuu...hii fact anaijua vizuri Job Ndugai.
 
Umemsikia juzi Rais Samia alivyozungumza kuhusu kutokutaka kumuongezea muda jaji mkuu wa sasa baada ya jaji wa sasa kufikia umri wa kustaafu?
Mkuu, Rais alisema hataki kumuongezea muda Jaji Mkuu asije (Rais) akagombana na majaji kwa kuwa huyu aliyepo umri wa kustaafu ulifika mwaka 2023 na akaongezewa na Rais miaka miwili ya kuendelea kufanya kazi, Jaji Stella Mugasha akaandika waraka kuwa Rais amevunja Katiba na Jaji Mkuu amekubali uvunjwaji wa Katiba kwa kuwa hakustahili kuongezewa muda. Rais anaweza kuongeza muda wa kustaafu kwa Jaji wa Mahakama Kuu au ya Rufani lakini sio muda wa Jaji Mkuu.
 
Huyu mama alisema katiba ni kakijitabu tu
 
Back
Top Bottom