Rais hateui jaji moja kwa moja bali tume ya utumishi wa mahakama (JSC) ndiyo huteua na kupendekeza majina matatu kutoka miongoni mwa majaji wa rufani na kuwasilisha kwa Rais kwa ajili ya kuidhinisha jina moja kati ya hayo aliyowasilishiwa.Kama kuna mhimili wa dola unaodharaulika, kutumiwa vibaya na kudhoofishwa basi mhimili wa mahakama ndio kinara.
Sijaona mantiki kwa nchi yenye mihimili rasmi ya dola mitatu inayojitegemea, yaani Rais (serikali), bunge na mahakama, halafu Rais kwa mamlaka yake awe ndio anayeteua mkuu wa mhimili wa mahakama, yaani Jaji Mkuu.
Ni kwanini mhimili wa mahakama usiwe na utaratibu wake wa kumchagua kiongozi wake mkuu, yaani Jaji Mkuu?
Kwanini nafasi ya jaji mkuu isigombewe na kupigiwa kura na majaji wenyewe?
Huo ndo ukweli, Watawala wengi huwaweka wanasheria mfukoni ili watawale vizuri bila kelele, Magufuli alikaa na huyu jaji miezi 8 bila kumthibitisha eti anakaimu, wakati nafasi ya Jaji Mkuu haikaimishwi, ulikua udhaifu wa kudharau Mhimili wa Mahakama, sulaa la bandari ,viongozi waandamizi walipanga sana , Hangaya akaanza kuwala vichwa watumishi wa Ikulu, akatafuta wanasheria wake wapindeshe sheria mkataba ukapitishwa chapu warabu wakachukua chao.Yes, kuna baadhi ya nchi, kabla hajatajwa hadharani, taasisi zote za usalama na kimadili zinapaswa kum-clear then inabaki mjadala kati ya raisi na uongozi wa juu wa Bunge, endapo mmoja wao atapinga na akawa na hoja yenye mashiko, raisi hawezi kulazimisha, anarudi ubaoni kutafuta mwingine.
Kwetu, si ajabu akateuliwa hata graduate, kisha masaa kadhaa kabla ya kuapishwa akatenguliwa.
Wewe unajielewa sana! Duniani mahakama zilizo huru jaji mkuu huchaguliwa na majaji wa mahakama ya rufaa! Ila ccm eti rais anateua jaji mkuu, kwa nini mhimili mwingine utawale mhimili mwingine? Upuuzi mkubwa sana!Kama kuna mhimili wa dola unaodharaulika, kutumiwa vibaya na kudhoofishwa basi mhimili wa mahakama ndio kinara.
Sijaona mantiki kwa nchi yenye mihimili rasmi ya dola mitatu inayojitegemea, yaani Rais (serikali), bunge na mahakama, halafu Rais kwa mamlaka yake awe ndio anayeteua mkuu wa mhimili wa mahakama, yaani Jaji Mkuu.
Ni kwanini mhimili wa mahakama usiwe na utaratibu wake wa kumchagua kiongozi wake mkuu, yaani Jaji Mkuu?
Kwanini nafasi ya jaji mkuu isigombewe na kupigiwa kura na majaji wenyewe?
Waza tofauti pia.Utaratibu huu una hatari kwa sababu itapunguza impartiality ya Majaji na kuunda makundi. Ukinipa kura nakupa hiki, na kuna uwezekano siasa nje ya muhimili zikaingia na kuivuruga mahakama
Umemsikia juzi Rais Samia alivyozungumza kuhusu kutokutaka kumuongezea muda jaji mkuu wa sasa baada ya jaji wa sasa kufikia umri wa kustaafu?Rais hana mamlaka ya kuteua Jaji Mkuu isipokuwa ataidhinisha jina moja miongoni mwa majina ya Majaji wa mahakama ya rufani aliyopelekewa.
Marekani kwa baba wa demokrasia, Rais anateua Jaji MkuuWaza tofauti pia.
Rais kukaa chini chumbani na mkewe/mumewe na kututeulia Jaji mkuu kuna faida gani kwa mhimili wa mahakama ikiwa atateua jaji yoyote kwa utashi wake kuwa jaji mkuu kuliko majaji wenyewe kuamua kwa kura nani awe jaji mkuu.
Huyo mteule wa Rais atawajibikaje kwa mhimili wa mahakama ikiwa hakuwa chaguo lao.
Uhuru wa mhimili wa mahakama unatokeaje ikiwa mkuu wa huo mhimili anateuliwana na mkuu wa mhimili mwingine?
Huo ni uoga tuUtaratibu huu una hatari kwa sababu itapunguza impartiality ya Majaji na kuunda makundi. Ukinipa kura nakupa hiki, na kuna uwezekano siasa nje ya muhimili zikaingia na kuivuruga mahakama
Ila hawajibiki kwa rais!Marekani kwa baba wa demokrasia, Rais anateua Jaji Mkuu
Ata spika anachaguliwa na Rais..wabunge wanasherehesha tuu...hii fact anaijua vizuri Job NdugaiUna hoja nzuri
Ila nahisi huu utaratibu wa Rais kuchagua Jaji upo katika nchi zote.
Nchi gani anawajibika kwa Rais?Ila hawajibiki kwa rais!
Mkuu, Rais alisema hataki kumuongezea muda Jaji Mkuu asije (Rais) akagombana na majaji kwa kuwa huyu aliyepo umri wa kustaafu ulifika mwaka 2023 na akaongezewa na Rais miaka miwili ya kuendelea kufanya kazi, Jaji Stella Mugasha akaandika waraka kuwa Rais amevunja Katiba na Jaji Mkuu amekubali uvunjwaji wa Katiba kwa kuwa hakustahili kuongezewa muda. Rais anaweza kuongeza muda wa kustaafu kwa Jaji wa Mahakama Kuu au ya Rufani lakini sio muda wa Jaji Mkuu.Umemsikia juzi Rais Samia alivyozungumza kuhusu kutokutaka kumuongezea muda jaji mkuu wa sasa baada ya jaji wa sasa kufikia umri wa kustaafu?
Huyu mama alisema katiba ni kakijitabu tuMkuu, Rais alisema hataki kumuongezea muda Jaji Mkuu asije (Rais) akagombana na majaji kwa kuwa huyu aliyepo umri wa kustaafu ulifika mwaka 2023 na akaongezewa na Rais miaka miwili ya kuendelea kufanya kazi, Jaji Stella Mugasha akaandika waraka kuwa Rais amevunja Katiba na Jaji Mkuu amekubali uvunjwaji wa Katiba kwa kuwa hakustahili kuongezewa muda. Rais anaweza kuongeza muda wa kustaafu kwa Jaji wa Mahakama Kuu au ya Rufani lakini sio muda wa Jaji Mkuu.