Kama Rais Magufuli ameweza kukuza pato la taifa kutoka sh trilioni 53 alizoacha Kikwete hadi sh trilioni 120, Mungu atupe nini tena?!

Kama Rais Magufuli ameweza kukuza pato la taifa kutoka sh trilioni 53 alizoacha Kikwete hadi sh trilioni 120, Mungu atupe nini tena?!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli hizi data zimenitia moyo zaidi na kunifanya nizidi kutembea kifua mbele.

Ukuaji wa pato la taifa kutoka sh trilioni 53 mwaka 2015 hadi sh trilioni zaidi ya 120 mwaka huu wa 2020 ni jambo la kujivunia ambalo ni lazima tulienzi kwa kumpa Dr Magufuli mitano tena.

Tundu Lisu atapewa kazi pale ofisi ya Mwanasheria mkuu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Ulikopata hizo taarifa bila shaka kuna na za ukuaji wa deni la taifa. Naziomba tafadhali. Kama zipo na ukuaji au uporomokaji wa pato la mtu mmoja mmoja naziomba tafadhali.
Deni la taifa ni 27% ya pato la taifa.

Deni ni himilivu sana kwa sababu ukomo wa kukopa ni 70% ya pato la taifa!
 
Kiukweli hizi data zimenitia moyo zaidi na kunifanya nizidi kutembea kifua mbele.

Ukuaji wa pato la taifa kutoka sh trilioni 53 mwaka 2015 hadi sh trilioni zaidi ya 120 mwaka huu wa 2020 ni jambo la kujivunia ambalo ni lazima tulienzi kwa kumpa Dr Magufuli mitano tena.

Tundu Lisu atapewa kazi pale ofisi ya Mwanasheria mkuu.

Maendeleo hayana vyama!
Umenena vyema Mkuuu hahahahahaa
 
Ccm mmekaa kihongo hongo tu mmeshataka kumpa hongo Tundu Lisu kwa ahadi ya uteuzi.
 
Tundu Lissu kwa heshima anapewa ubunge maalum ili aingie bungeni kuwapa amsha amsha wabunge wengine waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
 
  • Kicheko
Reactions: Ole
Kama pato la trillion 53 maisha yalikuwa mazuri kwawananchi kuliko hilo ongezeko is trillion 120 unayosema unadhani sasa tatizo litakuwa wapi kama sio hizo takwimu sio sahihi?matarajio ni kuwa kungekuwa na ongezeko la unafuu katika maisha kama kupabdishwa mishahara ajira mpya zakutosha kuongezeka mazingira mazuri yakufanya biashara nk
 
Tupo uchumi Wa kati Tuliaaa dawa ikuingie Kwani uliwahi hata mpigia kura kikwete wewe mpka utuulize maswali
Kweli mahaba sio kitu kizuri. Siamini kama hata unajua nini maana ya uchumi wa kati? Implication yake ni nini kwa maisha ya mtu mmoja mmoja?
 
Haupo sahihi ndugu, pato la taifa mwaka 2015 kwa mujibu wa benki ya dunia lilifika 47.3bil ambayo ni sawa na shilingi trilion 110
1601048172139.png

Gepu la pato la taifa kati ya kenya na Tz ilikuwa ni 17bilion lakini hili gepu limeongezeka zaidi ya mara na kufikia dola 38 bil kwenye kipindi cha miaka mitano iliyopita, kumekuwa na ukuaji wa kusuasua kwenye uchumi wa tz tangu 2016. kazi kubwa na misingi ya uchumi wa nchi ilifanywa sana na kikwete na mkapa.

NB: sina chama ila nimekuja kusahihisha. Unapotoa taarifa za uchumi ni vizuri kuwa na ushahidi wa data toka vyanzo sahihi.
 
Back
Top Bottom