Kama Rais ni mtetezi wa wanyonge na mtumbuaji majipu maarufu, kwanini hajamtumbua Said Lugumi?

Kama Rais ni mtetezi wa wanyonge na mtumbuaji majipu maarufu, kwanini hajamtumbua Said Lugumi?

Masikini Tanzania,
serikali iliyoamininika hapo awali leo imegeuka na kuwa waficha maovu na watetezi wa Mafisadi.

Mkataba wa Lugumi ni mtarimbo ulioiganda serikali ya CCM.
CCM ndiyo chama dume,na Magufuri ndiye rais wa Tanzania.Ndugai ni mbunge wa Kongwa na ni mwana CCM na ndiye spika wa Bunge la Tanzania a.k.a bosi wa Mbowe,Lema,Lissu na Miungu wako wote waliopo Bungeni unaowafahamu ww.Km hutaki,fanya hayo yanaweza kukusaidia-ama jinyonge,hama nchi,jitupe bahari na mengine mengi fanani na hayo.Na yakupasa utambuye,CCM ndiyo chama TAWALA hadi mwisho wa kinyongo chako.
 
CCM ndiyo chama dume,na Magufuri ndiye rais wa Tanzania.Ndugai ni mbunge wa Kongwa na ni mwana CCM na ndiye spika wa Bunge la Tanzania a.k.a bosi wa Mbowe,Lema,Lissu na Miungu wako wote waliopo Bungeni unaowafahamu ww.Km hutaki,fanya hayo yanaweza kukusaidia-ama jinyonge,hama nchi,jitupe bahari na mengine mengi fanani na hayo.Na yakupasa utambuye,CCM ndiyo chama TAWALA hadi mwisho wa kinyongo chako.
wewe umepanic.
 
You must see a psychiatrist kwani una shida kkubwa upstairs. Uliambiwa ni vitu 14 tu na 10 hazifanyi kazi. Wakati mwingine acheni kujipendekeza hadi kwa shetani kulikopitiliza. Tangulizeni utaifa kwanza na siyo matumbo yenu.
Hayo Ni maneno yenu tu....ukweli ndo huo ndo maaana unaona hata mtumbua majipu yupo kimya kashajua Ni maunafiki ya Wa upande Wa pili.......
 
Baada ya kuwasilishwa Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ndani ya Bunge la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, ilitakiwa kuwasilishwa Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ikitakiwa kuwasilishwa na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika Wizara hiyo, Mhe. Godbless Jonathan Lema (MB) Kuhusu makadirio ya Mapato na matumizi ya fedha ya Wizara hiyo.

Katika hali isiyo ya kawaida Hotuba hiyo ya Kambi Rasmi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyokuwa iwasilishwe leo Jumatatu 16/5/2016 Bungeni mjini Dodoma iliahirishwa kwa kile kilichosemekana Hotuba hiyo inatakiwa ikapitiwe upya na Kamati ya Maadili ya Bunge.

Katika hali ya kawaida, inaonyesha kuna mam bo ambayo wasingependa viwemo kwenye Hotuba hiyo hili hali mambo hayo yana tija kwa mustakabali wa Taifa letu.

Hapo ndipo unapogundua ya kuwa Serikali hii ya awamu ya 5 imejawa hofu na inataka kuficha madhambi mengi huku ikiwaadaa wananchi na mambo mbalimbali kama wanavyoita utumbuaji majipu, huku majipu ambayo ni hatari zaidi yakiendelea kuachwa na kutakwa kufichwa na kuumiza Taifa.

Serikali ya awamu 5 imeshaonyesha viashiria vya wazi wazi ya kuwa ni Serikali yenye hofu na ya Kidikteta na isiyopenda kukoselewa katika hali yeyote mfano, kukataza kuonyeshwa moja kwa moja kwa vikao vya Bunge ili waweze kuficha mambo yao machafu, kuchukua mambo ya msingi ambayo wananchi wangependa kuyajua na kuwapa uelewa na kujua ni kipi wawakilishi wao wanakifanya ndani ya Bunge, hali yao ya Kikatiba imeminywa wazi wazi(In a daylight).

Sheria kandamizi kwa vyombo vya habari, kufungia vyombo mbalimbali vya habari, hivi ni viashiria tosha ya kuwa Serikali hii haitaki kukosolewa na kutaka kuendesha nchi inavyotaka huku Katiba, Sheria,Taratibu mbalimbali za nchi.

Katika hili la kutowasilishwa kwa Hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inaonekana kuna mkono mrefu wa Rais mstaafu wa awamu ya 4 Mhe. Jakaya Kikwete akizuia na kutaka hotuba hiyo is iwasilishwe Bungeni kwani inamgusa kwa hali moja ama nyingine, Hotuba hiyo imetakiwa kupitia na na Kamati ya Maadili ya Bunge ili waweze kuondoa mambo mambo mbalimbali ambayo wasingependa yawasilishwe mbele ya Bunge letu tukufu la Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, katika Hotuba hiyo anaingizwa IGP Mstaafu Saidi Mwema ambaye ni ndugu yake.

Said Mwema ndiye aliyekuwa IGP na kuingia mikataba na Lugumi Enterprises ambaye amemuoa mtoto wa Said Mwema IGP huyo mstaafu.

Kikubwa ambacho kinatakiwa kufichwa kuacha mengine mengi ni Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyohoji utekelezaji wa mkataba wenye utata wa vifaa vya mfumo wa alama za vidole (AFIS) ulioingiwa Kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Kuna malumbano yaliyojaa sintofahamu na inatakiwa sintofahamu hii imalizike bila shaka, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka Serikali kutoa majibu kwa maswali yafuatayo:

1. Kwa kuwa mikataba ya Serikali kwa mujibu wa Sheria lazima ufuate Sheria za manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),Je utaratibu huu ulifuatwa?

Kingine cha muhimu kujua ni kwamba, Je Mkataba wa Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi umetekelezwa ama haukutekelezwa na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikuwa na tatizo la utekelezaji, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?

Yote kwa yote, swali la msingi, Kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa Kampuni ya INFOSYS inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS), kwanini C.A.G katika ukaguzi alioufanya hakuhoji suala la uhalali na kulinganisha thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa vile?


Akiwa ni Rais mtetezi wa wawanyonge kama anavyojinadi na mtumbuaji majibu maarufu, kwanini hajatumbua jipu la Said Lugumi na aliyekuwa IGP Said Mwema na Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kuwasimamisha kazi wote wanaondelea na kazi lakini kwa hali moja au nyingine wamehusika na mkataba tata wa Lugumi?

Elimu naamini bado. Na Watanzania bado wapo usingizi tunachagua viongozi wanajua Panadol za kutuliza machungu ya matatizo. Panadol huwa haitibu ninvyofahamu bali inatuliza maumivu. Kwa Akiri zao wananchi maskini sasa hivi wanagaiwa panadol, hii inadhihilishwa wazi na supports na shangwe viongozi wanapoonekana wakitumbua majipu hadharani. Taratibu Watanzania wataanza kuzinduka. Lakini I'll kufikia Hatua Elimu kubwa inahitajika.
Sio Siri badala nafuu ya maisha kwa sasa maisha yamezidi kuwa magumu.
 
Akiwa ni Rais mtetezi wa wawanyonge kama anavyojinadi na mtumbuaji majibu maarufu, kwanini hajatumbua jipu la Said Lugumi na aliyekuwa IGP Said Mwema na Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na kuwasimamisha kazi wote wanaondelea na kazi lakini kwa hali moja au nyingine wamehusika na mkataba tata wa Lugumi?

Mkuu, Magufuli hawezi kutumbua na kuingilia kati kazi inayofanywa na kamati ya Bunge. Ingekuwa hili suala limefika mezani kwake bila kuhusisha kamati ya Bunge, watu wangekuwa wametumbuliwa siku nyingi!
 
Baadhi ya comments za kujipendekeza kokote kule sio nzuri. Nadhani hata hao wakubwa wakisoma hizo comment wanawadharau. Sijui kwanini watu wanajitoa ufahamu. Mtoa madaraka hawezi kumpa madaraka mtu ambae hawezi ku- reason. Hata ushabiki wa simba na yanga ungekua namna hii, timu hizi zingekufa
 
Ccm haijawah kosea, mkiwa mnaisemasema ccm natamani kulia
 
Kama ni msomaji magazeti yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni mambo ya magazetini hamna jipya hata moja.NAKUAPIA.Alichofanya ni kukusanya habari za magazetini na kuziandikia hotuba!!! AIbu kuiita ile eti ni hotuba ya upinzani bungeni ni aibu.

Wee umekazana habari za magazeti. Kwani magazeti yanachukua wapi habari?? Utafikiri unajibu watotot wadogo. Ulishasuikia kuna gazeti hata moja limefungiwa na TCRA kwa kuandika LUGUMI au mamabo ya Zanzibar. Nyie ndio mnakisononesha Chama kwea utetezi hafifu hafifu kisa uumini. Kama huna hoja kaa kimya watu wajadili ova!
 
hivi kuna watu hawafuatiliii vyombo vya habari then wanajidai kutoa comment nadhani ndicho kilimzuia leo lema kuendelea kusoma bajet yake SAKATA LA LUGUMI mlitaka iundwe kamati huru ya bunge kuchunguza na ipelekwe report serekalini ili hatua ichukuliwe walipewa mwezi na mwezi huo haujaisha sasa mnataka nn?subirini report ifike mambo ya ainishwe watu walale nao mbele .
 
Ishu ni source au content.....??? Source yaweza kuwa ya kijinga lakini content yake ni heavy, by the way Rais mwenyewe ameshayatumia magazeti hayohayo unayoyadharau kufanya maamuzi nyeti kabisa rejea JAMHURI VS TPA, so sidhani kama tunaweza kujustify kuzuiwa kwa hotuba ya lema eti kisa ame quote magazeti vinginevyo kama tunakubaliana magazeti siyo reliable news/information source.

Argue, don't shout................
Kama ni msomaji magazeti yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni mambo ya magazetini hamna jipya hata moja.NAKUAPIA.Alichofanya ni kukusanya habari za magazetini na kuziandikia hotuba!!! AIbu kuiita ile eti ni hotuba ya upinzani bungeni ni aibu.
 
Niki-comment Mods wataondoa comment yangu. Ngoja ni kae kimya kwanza.
 
Hayo Ni maneno yenu tu....ukweli ndo huo ndo maaana unaona hata mtumbua majipu yupo kimya kashajua Ni maunafiki ya Wa upande Wa pili.......
Huna tofauti na jirani anyeshangilia jirani kuunguliwa nyumba moto ilihali nyumba zao zimeshikana! Cha kukufanya ufikiri ni kelele za upande wa pili ni nini? Kamati iliyoibua uozo inaongozwa na ccm, cag ni ccm na serikali ni ya ccm. Aibu hii kwa wanaccm mnaificha kupitia tv live siyo? Ingeibuliwa na kina Zitto mngekuwa na majibu rahisi kama haya. Mwambieni cag awe anafichia siri.
 
Kama ni msomaji magazeti yaliyomo kwenye hiyo hotuba ni mambo ya magazetini hamna jipya hata moja.NAKUAPIA.Alichofanya ni kukusanya habari za magazetini na kuziandikia hotuba!!! AIbu kuiita ile eti ni hotuba ya upinzani bungeni ni aibu.
unaandikaga nini wewe?unaapa kwa jina LA Nani? fb wanakumiss kule.
 
Yaani huyo JK asizuie mijadala kibao ambayo ilikuwa inahatarisha hata kuporomosha kwa serikali yake leno hii aje kuzuia wa mjadala wa Mambo ya Ndani kwa ajili ya kumlinda shemeji yake!!
 
Watu hadi mnatia kinyaa. Yaan mna mahaba na vyama utazani tuko.kwenye kampeni
 
JPM kuhusu Lugumi ameshikwa pabaya.Ohhh,huu ni mwiba mchungu na umeganda.Pole Ngosha.
Masikini Tanzania,
serikali iliyoamininika hapo awali leo imegeuka na kuwa waficha maovu na watetezi wa Mafisadi.

Mkataba wa Lugumi ni mtarimbo ulioiganda serikali ya CCM.
 
5.1 Mkataba tata wa Lugumi na Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali , ilihoji utekelezaji wa mkataba wenye utata wa vifaa vya Mfumo wa Alama za Vidole (AFIS) ulioingiwa kati ya Jeshi la Polisi Tanzania na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Mheshimiwa Spika, kumetokea majibishano na malumbano mengi kwenye vyombo vya habari na miongoni mwa wabunge wa Bunge lako tukufu, hasa pale walipoanza kuhoji utekelezaji wa mkataba huo hasa kuhoji juu endapo vifaa hivyo vinafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, Kufuatia majibishano na malumbano yaliyojaa utata ambao lazima upatiwe majibu yasiyo na shaka yoyote, hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali kutoa majibu ya moja kwa moja bila kupepesa macho. Tunataka Maswali yafuatayo yajibiwe hapa bungeni;

Mheshimiwa Spika,

1) Kwa kuwa mikataba ya serikali kwa mujibu wa sheria lazima ufuate sheria za manunuzi na kuthibitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Je, Utaratibu huu ulifuatwa? 2) Je Mkataba huu wa LUGUMI ENTERPRISES na JESHI LA POLISI umetekelezwa ama haukutelezwa, na kama ulitekelezwa ni kwa kiwango gani, na ikiwa kulikua na tatizo la utekelezaji, Je, Jeshi la Polisi lilichukua hatua zipi?3) Je, ni kampuni ngapi ambazo zinahusika na hatua za utekelezaji wa Mkataba kati ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, kwa kuwa kampuni ya INFOSYS ambayo mmoja wa wamiliki wake ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga inatajwa kufunga vifaa hivyo (AFIS). 4) Ni kwanini C.A.G katika ukaguzi wake hakuhoji kuhusu uhalali na ulinganishi wa thamani ya pesa ya manunuzi na faida ya vifaa hivyo?5) Kampuni ya INFOSYS (inayomilikiwa na Mhe. Kitwanga) imedai kulipwa na Jeshi la Polisi, takribani Dolla za Marekani 74,000, Je fedha hizi Kampuni ya Mhe. Kitwanga ililipwa kwa kazi ipi iliyofanya na Jeshi la Polisi? 6) Ni kwanini mpaka sasa , Rais Magufili hajachukua hatua dhidi Said Lugumi, na aliyekuwa IGP Said Mwema / Emmanuel Nchimbi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na kuwasimamisha kazi wale wote ambao bado wako kazini juu ya mkataba tata wa Lugumi ?7) Tunamtaka Rais , kutengua mara moja uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na kumrudisha nchini mara moja , kwani alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Ndani na ni imani ya Kambi rasmi kuwa alijua mambo yote yanayoendelea ya mkataba wa Lugumi


Mheshimiwa Spika , Ni imani ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuwa Mhe.Waziri Charles Kitwanga, anazo taarifa za Mkataba huu na utekelezaji wake aidha kutoka kwenye Kampuni yake ambaye yeye ni Share holder ( Mbia ) ambayo ilifunga vifaa hivi au anazo taarifa ya utekelezaji wa Mkataba huu kutoka Jeshi la Polisi ambalo liko chini yake kwa kiwango chote kuhusu mambo yote ya Mkataba huu.

Mheshimiwa Spika, Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) , alinukuliwa na vyombo vya habari pale alipoulizwa kuhusu sakata la Lugumi na Mikataba yake na Jeshi la Polisi kutotekelezwa, alijibu majibu mafupi Katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 27/04/2016 namnukuu “siyo kweli, watu wana ugomvi wao kibiashara, lakini nakueleza wazi kwamba, tembelea vituo vyote tulivyokubaliana, utakuta mashine zipo. Inawezekana zingine hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa internet” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, kulingana na maswali ambayo tumeuliza hapo juu na uchambuzi wetu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Spika,

1. Kwa vile Waziri wa Mambo ya Ndani anahusika kwa karibu katika Mkataba huu kupitia Kampuni yake ya INFOSYS na vile vile Jeshi la Polisi liko chini yake , je ? haoni kuwa ni busara kwa yeye kujiuzulu ili kutoa nafasi ya Uchunguzi kuepusha mgongano wa maslahi ndani ya Jeshi la Polisi na kwenye Kampuni ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki ?

Mheshimiwa Spika,

2. kwa vile inaonekana kupitia vyombo vya habari na kauli za viongozi mbali mbali kuwa upo uwezekano wa Polisi kuwa wametapeliwa na vifaa hivyo havijafungwa, Kambi ya Upinzani Bungeni inautaka uongozi wote wa juu wa Jeshi la Polisi kujiuzulu mara moja, kwani kama wao wameshindwa kujua ukweli wa vifaa vilivyofungwa kwenye vituo vyao vya Polisi ama vipo au havipo, watawezaje kuchunga na kulinda mali na usalama wa raia wengine?

Mheshimiwa Spika,

3. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inataka majibu yote yanayohusu Mkataba wa Lugumi na Jeshi la Polisi kuhusu utekelezaji wake uwekwe wazi hapa bungeni na wizara husika.
 
Back
Top Bottom