Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Inahitaji tamko moja tu kwa Raisi Samia kukomesha uteaji na uuaji wa raisa wa Tanzania. Anachotakiwa kufanya ni kutoa tamko hili kama Amiri Jeshi Mkuu;
"Kwa kipindi hiki tukitafuta suluhisho la kudumu kokomesha utekaji na uuaji, ieleweke wazi kwa raia na wakazi wote hapa Tanzania kwamba kuanzia sasa hakuna chombo chochote cha usalama nchini, zaidi ya Jeshi la Polisi, ambacho kina mamlaka ya kukamata watu (kufanya arrest). Na ukamataji wowote utakaofanywa na Polisi, ni lazima ufanyike askari wa polisi wakiwa na uniform zao na vitambulisho, na wakitumia magari yenye utambulisho wa alama za polisi na pamoja na registration number.
Na ni jukumu la vyombo vingine vyote vya usalama, kutia ndani Usalama wa Taifa TISS na Takukuru, kama wana sababu za kumkamata au kufanya arrest ya mtu yeyote ndani ya Tanzania, watafanya hivyo kwa kupitia na kuwatumia Jeshi la Polisi, na Polisi watamkamata huyo mtu kwa utaratibu niliousema hapo juu.
Hivyo basi, na iwe wazi kwa raia wote wa Tanzania kwamba ukamataji wowote wa mtu ndani ya Tanzania, awe raia au mgeni, ukifanyika nje ya utaratibu huu, huo si ukamataji halali, na Jeshi la Polisi na raia wote kwa ujumla wanakuwa na wajibu wa kuzuia ukamataji huo usifanyike, kutia ndani kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi"
Sasa, kama ni kweli Raisi Samia ana nia na yeye binafsi au serikali yake haihusiki, au chama chake CCM hakinufaiki na utekaji huu na mauaji yanayofanyika, hili tamko litakomesha huu utekaji mara moja. Swali ni kwamba, je huu utekaji hauna baraka za serikali, au chama cha CCM? Kama una hizo baraka, basi tusitarajie kama Raisi Samia atatoa tamko hili, kwa sababu atakuwa anajua kinachoendelea na menginne yote anayosema kuhusu utekaji yanakuwa ni maigizo tu.