Kama Rais Samia ana nia ya kukomesha mara moja watu kutekwa na kuuawa, atoe tamko hili


Tatizo kasema ni kiziwi
 
Unacho fanya ni sawa na kumfuata muaji na kumwomba atusaidie kumtafta muwaji ambaye ni yeye mwenyewe
 
Hatari kweli kweli ...
 
Hana nia hiyo na hajawahi kuwa nayo
 
Hivi wasiojulikana wa wakati wa magufuli inawezekana bado wanafanya ile kazi ya wakati ule ya kuteka watu?
 
Hathubutu kusema hivyo sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani kunategemea moja kwa moja hao wahalifu.
 
Hathubutu kusema hivyo sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani kunategemea moja kwa moja hao wahalifu.
Hatari sana. Hivi unawezaje kujiita kiongozi wa watu ikiwa ili uwaongoze hao watu unaona lazima uwaue?
 

Huu utekaji unaoendelea Ccm, serekalo na Samia wanajua kila kitu na wanamaslahi na huu utekaji. Usitegemee hatua zozote serious. Anataka watu waingie uoga, kisha ajifiche ndani ya 4r.
 
Inachukua muda mrefu sana kufuta sheria. Hadi ifutwe tunaweza kupoteza watu wengine
Tamko la Rais lina nguvu kuliko unavyodhani.Kwa kuwa Mh.Rais Samia amesema kitu na umeanza kusikia matamko mengine ya kujilazimisha,basi wewe kama Mwananchi muombe sana Mungu ili pasitokee jambo lingine la kijinga litakalowaondoa wa Tanzania katika hoja ya msingi..yaani hoja ya mauaji chini ya kivuli cha Sheria ya Usalama wa Taifa.
MUNGU HALALI KAMA BINADAMU..MATOKEO YA HUU UTEKAJI NA MAUAJI NDIO MLANGO WA KUIPONYA NCHI DHIDI YA MADHILA YA KUPANGWA!
 
Utekaji na utesaji na Kuwaua waalifu bila kuwapeleka wahusika mahakamani ni mifumo ya falier state, nchi kama nchi imeshindwa kutengeneza mifumo bora ya maisha ya watu wake kwahiyo wanadhani utaweza kuwamaliza watu wanaokwenda kinhume na sheria, kinyume chamifump ya watawala, kinyums nawanavyotaka wao nchi iendde.. kwa mfano wimbi la panya Road solution ilikuwa siyo kuwauwa, wimbi la panya Road linatokana na umaskini, kwani utaona vijana wengi waliokamatwa kwenye operation ya Panya Road wanatoka mitaa ya Tandika, Mbagala, Chanika, vingunguti, Gongo la mboto, kwampalange, yale maeneo ambayo umaskini umetamalaki, Sasa serikali makini isingetumia POLISI peke yake kumaliza tatizo hilo. Ingeangalia ni jinsi gani wangeweza kupunguza wimbi la vijana wasiyo na kazi maeneo hayo, Wangepeleka vyuo vya VETA maeneo hayo na kwakuwa asilimia kubwa ni watoto wa maskini, wangetengeza mazingira wasome bure na chakula cha mchana na baada ya mafunzo wanawapeleka katika kazi za kujitolea sehemu mbali mbali ili kuwajengea uwezo wa fani walizo nazo baada ya hapo wanawaacha, wangeza kupunguza panya Road kwa asilimia 80.Ila viongozi wetu siyo wabunifu wanawekeza fedha nyingi kwenye magari ya washa washa na magari ya Anasa huku wananchi wakiishi katika umaskini wakupitiliza.
 
Fact
 
Nchi huwa inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni na taratibu.
Nchi haiendeshwi kutokana na matamko tu ya watawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…