Kama Rais Samia anaifungua nchi ni nani aliifunga? CCM iombe Radhi

Kama Rais Samia anaifungua nchi ni nani aliifunga? CCM iombe Radhi

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Siku mia moja za Rais Samia ni pongezi kila kona bila kukoma lakini kuna baadhi ya hiana. CCM inafanya hiana kwa Watanzania na baadhi ya washauri wa Rais wasije kutufanyia hiana.

Mama tunamuheshimu sana na kwa kweli kaanza vyema. Tunampongeza kwa hatua alizofanya kwa sasa na hatutonyamaza kumkosoa pale atakapokengeuka. Mungu amsaidie.

Turudi kwenye mada. Vyombo vya habari vingi vikiwemo vile vilivyokuwa vinasifu na kuabudu yaliyofanywa na awamu ya tano sasa viko mstari wa mbele vikieleza umahiri wa Mama wa kufungua demokrasia, kufungua uchumi na Diplomasia yetu.

Tunajiuliza kama mama anafungua Nchi kwani ni nani aliifunga? kumbe CCM na jumuiya zake mlitufanyia hiana sana Watanzania.

Leo mnathubutu kutwambia Mama anafungua nchi na miezi kadhaa nyuma mlisifia matendo ya Awamu ya tano yaliyolalamikiwa kila kona ndani na nje ya Nchi?

Tulisema sana kuhusu kuminywa kwa Demokrasia, kuonewa watu, wafanyabiashara kubambikiziwa kesi za uhujumu uchumi, wanasiasa kuteswa n.k. mlibeza na kushupaza shingo na mkawa madalali wa watesaji wa watanzania wenzenu?

Kwa nini kama mambo yalikuwa shwari leo hii ni kama Mama anaanza upya kwa nini?

CCM IOMBE RADHI
Kuna mambo hayawezi kurudi nyuma ikiwemo dhuluma za Chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa 2020. Kuna Mateso na mauaji mengi. Hakuna namna ya kulipwa watu waliodhulumiwa na kupotezewa muda wao hata kama wameachwa huru kwa makosa ya kubambikiza. Katika hali hio CCM kama chama kilichoshika Dola na kuendelea kusimamia yote hayo kufanyika basi walau ituombe Radhi Watanzania na kufidia wahanga kwa yale baadhi yanayowezekana.

CCM na wenye dhamana, watuombe radhi na kuahidi kutojirudia tena haya. Mama yetu asipotezwe kwa ushauri mbaya na Chama kiwe na Timu Maalumu ya kusimamia Umoja wa Kitaifa.

Miaka 5 ya dhoruba chini ya Utawala wa CCM ile ile kufurahia utendaji wa Mama leo bila ya kuomba radhi yaliyofanywa na CCM ile ile miaka mitano nyuma ni hiana na kukosa utu. CCM ni watu, wana hisia na wanafahamu machungu yaliyowapata watanzania hebu chama kijitokeze kiombe radhi.

Hii ni rai yangu ili mumsaidie Mama kulibeba dubwanasha la kivuli cha wasiojulikana na dubawanasha la chuki iliyojificha.

Tanzania ni kubwa na zaidi ya CCM.

Siku zote maslahi ya Taifa na umoja wa Watanzia utangulizwe.

Katiba Mpya haiepukiki.


Kishada.
 
Wana CCM walimpompiga mzee Warioba waliwaomba msamaha.

Neno chama dume huwa unaelewa?
 
Nchi inaangamia kwa sababu ya CCM.
Walau mama sasa anateua watu wasio wanaCCM. Ila katiba mpya ni lazima.
 
Back
Top Bottom