Kama Rais Samia ataacha Katiba Mpya basi itatupatia picha kuwa uongozi ni akili na siyo nguvu

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Yaani huyu Mama naona anaenda kuwa Rais was pili ukimtoa Baba wa Taifa, maana Kama atatupatia katiba Mpya Basi Legacy yake itakuwa kubwa Sana.

Nilichogundua Uongozi ni akili. Legacy sio kujenga barabarani mbovu zenye mashimo na ujanja ujanja.

Mama akiacha katiba Basi peponi moja kwa moja.
 
Hayo ya peponi, hatuweza kuyanenea, lakini lililikubwa na wazi, hakika ataweka legacy ya vizazi vya sasa na vingi vijavyo. Kama ulivyosema, atakuwa Rais wa pili baada ya Mwalimu kulumbukwa daima.

Marais pekee kule Marekani wanaopewa heshima kubwa ni George Washington (Baba wa Taifa) na Abraham Lincon (Baba wa demokrasia). Huenda na sisi tutampata Lincon wetu.
 
Dr. Samia suluhu hassan, anakwenda kuweka legacy ya kipekee, kujenga legacy si kwa njia ya mabavu, ubabe, ushenzi, unyangau, kuijenga legacy ni akili pevu, hekima, busara, mama anaivaa nafasi yake haswaa, mashalaah.
 
Peponi hakuuhusiani na katiba mpya. Atimize wajabu tusubiri kama maandiko yalivyosema.

Kikubwa akuze uchumi. Kupunguza gharama ya maisha. Kuongeza kipato cha kila mtanzania. Iko ndio bado tunamdai.

Anakwenda vizuri
 
Yaani huyu Mama naona anaenda kuwa Rais was pili ukimtoa Baba wa Taifa, maana Kama atatupatia katiba Mpya Basi Legacy yake itakuwa kubwa Sana.

Nilichogundua Uongozi ni akili. Legacy sio kujenga barabarani mbovu zenye mashimo na ujanja ujanja.

Mama akiacha katiba Basi peponi moja kwa moja.
Na Kuna uwezekano mkubwa wa Hilo kufanyika, nadhani JK aliyejaribu ku push wakati ule na kutishwa ,this time around anataka ku push kwa mgongo wa Samia ambae kimisimamo wanaendana..

Na wakifanya hivyo CCM watashinda tuu uchaguzi japo kwa margin ndogo Sana.

Mwisho wawe na kipengele Cha Serikali ya mseto Kama Vyama vimepata Asilimia fulani ya kura za Urais na Ubunge.
 
Na wakifanya hivyo CCM watashinda tuu uchaguzi japo kwa margin ndogo Sana.
Tusijidanganye, uchaguzi ukiwa fair ccm wanaweza kupata wingi kwenye ubunge. Kwenye urais hawawezi kupenya.

Chama kimechokwa, na bahati mbaya sana wapiga kura hawaangalii tukiitoa ccm huyu anayeingia atakuwa na hali gani.
 
True Ccm hipo ICU
 
Nitaamini kuwa aliye vuruga rasimu ya Warioba ni yule aliyewatuma DAB na genge lake Ubungo Plazza
Mimi naona afadhali ule mchakato ulivurugika ili tupate katiba bora.

Ile rasimu, ukiondoa kuwa na serikali tatu, mengine karibia yote ilikuwa copy and paste ya hii katiba mbovu tunayolalamikia.

Hatuwezi kupata katiba nzuri kama itaandikwa na wanasiasa au wengine wowote ambao ni wanufaika wa katiba hiyo.
 
Dr. Samia suluhu hassan, anakwenda kuweka legacy ya kipekee, kujenga legacy si kwa njia ya mabavu, ubabe, ushenzi, unyangau, kuijenga legacy ni akili pevu, hekima, busara, mama anaivaa nafasi yake haswaa, mashalaah.
Kwa hili nimependa mno mno na ninam support 100%
Pia ataweka sawa kwenye historia kwamba women are never power mongers,

Thanks a lot mama HE Dr. Samia Suluhu Hassan!
 
Tusijidanganye, uchaguzi ukiwa fair ccm wanaweza kupata wingi kwenye ubunge. Kwenye urais hawawezi kupenya.

Chama kimechokwa, na bahati mbaya sana wapiga kura hawaangalii tukiitoa ccm huyu anayeingia atakuwa na hali gani.

Hata ubunge wana hali ngumu sana kila kona hakuna walichofanya 2025 wajipange sana watapoteza viti vingi sana.
 
Hatuwezi kupata katiba nzuri kama itaandikwa na wanasiasa au wengine wowote ambao ni wanufaika wa katiba hiyo.
Sijui think tank yake ni akina nani kwenye hili
 
Hata ubunge wana hali ngumu sana kila kona hakuna walichofanya 2025 wajipange sana watapoteza viti vingi sana.
Kura halali hawawezi pata zaidi ya 30% kwenye urais. Hata huko vijijini walikokuwa na support base kubwa ya kinamama wamechokwa.

Bungeni bado watatawala hata kama ni kwa wingi mdogo.
 
Back
Top Bottom