Kama sababu ni dawa za kulevya, kwanini Rais wa China hajatekwa mpaka sasa kama Maduro?

Kama sababu ni dawa za kulevya, kwanini Rais wa China hajatekwa mpaka sasa kama Maduro?

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,406
Reaction score
12,736
Kama sababu ya Maduro kutekwa na Marekani ni madawa ya kulevya? Kwanini mlalamikiwa mkubwa kuhusu athari za madawa ya kulevya Marekani ambaye ni China Rais wao Xi Jinping mpaka sasa hajatekwa kwenda U.S kujibia mashitaka yake?
 
Vifaranga wa kuku na swala vyote ni vitoweo, kwa nn mwewe aache swala achukue vifaranga wa kuku!!? Jibu lako lipo hapa.
 
Kama sababu ya Maduro kutekwa na Marekani ni madawa ya kulevya? Kwanini mlalamikiwa mkubwa kuhusu athari za madawa ya kulevya Marekani ambaye ni China Rais wao Xi Jinping mpaka sasa hajatekwa kwenda U.S kujibia mashitaka yake?
Kwa hiyo unataka wote wakamatwe kwa wakati mmoja au kushughulikiwa kwa njia moja tu?Huko ndiko kupangiana sasa.
 
Mwewe hawezi kubeba swala
ndio mwewe ananyakua vyepesi anavyoweza kuvimudu kubeba, swala ni mzito hamwezi ndio China iyo sasa!, hata katika maisha yetu ya kawaida jitahidi sana kuwa mzito kama swala ili usifikiwe sana kiwepesi na maadui pamoja na walimwengu wakuogope hawakawii kukupindua miguu juu!, si unajua msaliti hana alama.
 
Xi ye akae zake uko china pale venezuela imeshachukuliwa na baba yake, hakuna tn mchina wala urusi pale venezuela yny mafuta ya kutosha kbs akiba nzto, lengo la marekani ni kubeba mafuta na kushusha bei ya mafuta duniani ili shoga ake na xi bwana putin akose pesa ya kutosha ya kuuza mafuta uchumi uporomoke zaidi, swali kwako kwann china na urusi hawakupeleka jeshi kumsaidia mshirika wao? Je wajua meli ya mafuta ya urusi imedakwa jana na majeshi ya marekani? Kama china anajiamin apeleke usengerema wake kwasasa pale venezuela au avamie taiwan..
 
Back
Top Bottom