Kama Samatta kakwama huko England mashabiki tuambiwe ukweli

Kama Samatta kakwama huko England mashabiki tuambiwe ukweli

Kupata permit ya kufanya kazi England inakuwa ngumu wakati angekuwa mbelgiji hahitaji permit kufanya kazi England.

Atapata permit, next weekend atakuwa ndani ya uzi wa Aston Villa akiwasaidia wasishuke daraja.

Kila kitu kina taratibu zake, ukute angekuwa na hiyo dual citizenship asingepata hiyo nafasi.

Baada ya Liverpool FC, Aston Villa itakuwa timu yangu ya pili kuishabikia. I hope itabaki Premier.
 
Hizo points anazipata vipi ? Kwani Aston villa before wamu point walikua hawajajua hayo?
Inaandikwa na James Rushton tokea nchini Uingereza. Klabu ya Aston Villa inahitaji mshambuliaji na hadi sasa tetesi ni uhamisho wa dau la pauni 8.5 millioni kumpata mtanzania Mbwana Ally Samatta toka klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji limekwishakamilika.
Mshambuliaji huyu amekuwa akiishi na kufanya kazi nchini Ubelgiji tokea mwaka 2016.

Amefurahia muda wake katika soka la Ulaya tokea muda huo ila uhamisho kwenda England utamlazimu Samatta kupitia vigezo vingi ambavyo huombwa na watu wasio na pasi za Jumuiya ya Ulaya.

Kwa kuwa Tanzania haipo Jumuiya ya Ulaya Samatta itamlazimu kupata kibali cha kazi.

Samatta atapata vipi kibali cha kazi? Ofisi ya mambo ya ndani ya Uingereza huweka mfumo wa pointi na klabu husika hufanya maombi kwenye chama husika cha soka kuwasaidia kwa ofisi ya mambo ya ndani na chama cha soka cha England FA kuruhusu kibali kutolewa.

Mfumo wa pointi unamaanisha kibali cha kazi kutolewa ila hii ni kwa wachezaji ambao timu zao zinashika nafasi 10 za juu katika viwango vya FIFA. Huwezi kuiona Tanzania katika kundi hili, mara ya mwisho kwa timu hii kushika viwango vya juu vya FIFA ilikuwa ni mwaka 1995 iliposhika nafasi ya 70. Kwa sasa ni ya 134 hii ikimaanisha Samatta atahitaji kusanya pointi zaidi toka katika vipengele vingine kama ifuatavyo. LICHADI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kawaida huwa haichukui zaidi ya masaa 48 baada ya vipimo vya afya mchezaji kutambulishwa na klabu, fuatilieni sajili zote mtaona

lakini huyu ndugu yetu Samatta tokea tuskie yupo Uk akifanya vipimo vya afya tunaona kimya tu mpaka sasa, kama dili limebuma tuambiwe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha uchawi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Isije kuwa afya mgogoro. Ila deal likibuma wabongo kuna kitu mtajifunza. Kuacha kushadadia vitu kabla ya kuwa imehakikishwa.
Mbona ni kawaida tu hiyo, si huwa tunashangilia tangu mashambulizi yanapoelekea golini, "anakwenda Kagere..Kagere...kwake Chama...Chama...Chama..kwake Ajibu..Ajibuuuuuuuuugooooooooooo" akikosa basi tunashika vichwa, wa kutukana anatukana maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom