Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Jana nilimsikia Prof Lipumba akisema yeye ameanza kuswalia nyumbani ili kuepuka misongamano inayoweza kusababisha maambukizi ya Covid 19.

Binafsi nikawa nimemwelewa vilivyo.

Ndipo nikaanza kutafakari, kama Waislamu kule Saudia wanaswalia nyumbani Bakwata wanashindwa nini?

Kama Wakristo kule Vatican, UK na Germany wanasalia majumbani hawa Katoliki, Anglican na KKKT wanafeli wapi?

Kama Walokole huko USA wanasalia majumbani hawa kina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mwingira wanashindwa nini?

Kuna wakati yatupasa kutumia busara hata kama mamlaka za juu zimewaachia hiyo fursa bado mnatakiwa kutumia hekima ya Mungu kutenda jambo sahihi.
Serikali haiwezi kuwakataza directly lakini nyie mmebarikiwa macho ya rohoni na mwilini na hata hao wagonjwa 88 waliotangazwa hadi sasa ni waumini wenu.

Hekima ya Mungu wa mbinguni na iwe juu yenu!
..... hongera kwa darasa makini
 
Unajua ukishakiri kua yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yako unakua umetangaza vita na shetani, na shetani atajaribu kufanya kila njama za kukuporomosha hapo juu ulipo

Unajua kwamba shetani kapewa mamlaka ya kumjaribu binadamu na katika hili shetani kaamua kutumia huu ugonjwa kama jaribio ili kuwateka watu?

Unajua kukubali kusalia nyumbani kwa kuogopa maambukizi ambayo yamepangwa na shetani ni ishara kwamba shetani amekushinda nguvu na umekosa imani ya kupambana naye?

Unaelewa kwamba namna pekee ya kumshinda huyu shetani ilitakiwa yeyote yule ambaye amemkiri yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yake ajitokeze katika wodi za wagonjwa wa corona kwa lengo la kuwafanyia sala ya toba kwa kuwashika vichwani?

Mnakumbuka kua ukiwa na yesu hakuna lishindikanalo maana amewaahidi kutengeneza njia mahala pasipo na njia?
We kiumbe una ugonjwa mmoja hatar sana hadi nimekuhurumia. Na ukute unamaanisha! Itoshe kusema licha ya kuaminishwa ishirikishe akili yako hata kidogo bas.
 
Hoja hii inachukiza na kuudhi mno!! HAIWEZEKANI!! Tumekuwa wajinga namna hii? Vatican na Ujerumani zinahusika vipi na imani ya watanzania. Hivi nikisema kwa kuwa Ulaya na marekani wameridhia ushoga basi nasi tufuate nitakuwa sahihi?

Inakera sana!! Ni heri kama mtu anatoa mfano na afanye hivyo lakini si kwa kuonyesha kwamba imani za watanzania zinaratibiwa Roma. Tujibidiishe ujifunza misingi ya imani, sio kukariri.

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
Maaskofu wa Katoliki wanateuliwa wapi?

Usilete kuchamba kwingi bwashee!
 
Maaskofu wa Katoliki wanateuliwa wapi?

Usilete kuchamba kwingi bwashee!
Hoja yako imeongelea maaskofu Katoliki? Kwa hiyo ukatoliki ulianzia Vatican? Pitia upya historia yako

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Hoja yako imeongelea maaskofu Katoliki? Kwa hiyo ukatoliki ulianzia Vatican? Pitia upya historia yako

Sent from my SM-A720F using Tapatalk

Ukatoliki ulianzishwa na Warumi wa Italia ndiyo maana hata jina lake ni Roman Catholic.
 
Back
Top Bottom