Punguza Makasiliko, Hii vita Yanga wamepigana kwa strategy ya hali ya juu sana.
Kwanza wali mmbana bodi ya ligi asifurukute, walipo hakikisha hafurukuti aka anzishiwa zengwe mtoa maamuzi Tff.
Baada ya Tff kuona moto umemshinda kakimbilia BMT/Wizarani kwa Mwana FA ,Maana mzee Kabudi yeye Tangu alipo gundua boss wake mkuu wa Mawaziri kahusika kutoboa mtumbwi alishajitoa kwenye usuluhishi, Maana ripoti ya Uchunguzi ili muanika Boss wake.
Mzee Kabudi baada ya kuona lisimuangukie Jumba bovu, Kaamua kumweleza Mama kilakitu.
Mama baada ya kuona Mambo yamesha haribika na kelele za wapiga kura zimeshakua nyingi aka amua atumie kofia yake ya Amiri Jeshi mkuu.
Kilichofuata ni kuitwa maboss wenye ushawishi mkubwa wa hizi timu na kutoa maelekezo.
Yule Boss anaye ishi Dubai alikua mbali maana wito ni wa ghafla aka agizwa atume wawakilishi wenye sauti waje wapokee maelekezo ya Amiri Jeshi na kuyatekeleza.
Tff/ bodi ya ligi lakwao nafikiri lina chemka, linasubiriwa ili la Derby lipite mwisho wa msimu utekelezaji wa maelekezo ya Amiri Jeshi juu ya tabia zao za hovyo waanze kuwajibishana.