ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 937
Hivi iki kiapo cha uaminifu kwa viongozi wetu wakiwa wameshikilia vitabu vya dini zao mikononi au kutamka maneno yanayofaa kuchukuliwa kama "kiapo cha uamninifu" kina maana yeyote kwetu au ni mambo ya mapokeo na ambayo yamejaa kwa waliotoa dhamana?
Ikiwa ukiapa kanisani kwa kushika/ kuiinua juu Msaafu au Biblia na badae ukatenda dhambi ya kushindwa kutekeleza yale uliyoapa, unapaswa kumrejea Mungu na kumwaomba huruma zake, na ikiwa kwa Serikali viongozi wanaapa kwa kushika Vitabu vya Dini na Katiba ya Nchi mbele ya Watanzania, inakuwaje mtu akitenda uovu unaokiuka kiapo cha uaminifu aishie kusema "nimejihudhuru / nimeachia ngazi" tu na kama alikuwa Waziri basi ataendelea na nafsi yake ya ubunge ambao pia una kiapo cha uaminifu kwa mujibu wa Katiba?
Je, ikiwa kiongozi amevunja kiapo cha uaminifu na ameendelea kuwepo ndani ya mmoja ya mihimili ya Serikali , kuna sababu yeyote ya kuwa na kiapo cha uaminifu ikiwa kiutendaji ioanekana kama hakiheshimiwi kabisa?
Ikiwa kukiri kosa ni pamoja na kusema "najihudhuru/naachia ngazi" ikimaanisha kushindwa kuendelea na dhamana ile uliyopewa aua umehusika moja kwa moja na tuhuma zinazodaiwa dhidi yako au watendaji waliochini yako, Je, ipo haja tena ya mtu ambaye alikiri kushindwa kutekeleza kiapo cha uaminifu kwa kwa staili ya "kujihudhuru wadhifa fulani" kuendelea kupewa madaraka mengine Serikalini pasipo kutakiwa kuapa upya kiapo cha uaminifu au hata kufikishwa mbele ya Mahakama ili ikamsafishe kwa dhambi ambazo anatuhumiwa nazo?
Ikiwa kiongozi aliyekula kiapo cha uaminifu na kwa makusudi au kwa kutokujali anashindwa kutimiza wajibu chini ya kiapo kwa kutowachukulia hatua stahiki wale ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi na oovu wa kurejesha nyuma maendeleo ya nchi, Je, tuna haja ya kuendelea kuwa na hiki kiapo cha uaminifu katika taratibu zetu.?
Na ikiwa kiongozi anaweza kuthibutu kudanganya mali zake chini ya kiapo cha uaminifu, ipo sababu yeyote ya kukiamini "kiapo cha uaminifu?" au tubadili sheria zetu ili kama mtu aliwahi kukiuka kiapo cha uaminifu asiruhusiwe tena kushika wazifa wowote wa kisherikali au kisiasa?

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA YA MWAKA 1977
Ibara ya 42(5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais, kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Ibara ya 49. Makamu wa Rais, kabla ya kushika madaraka yake ataapishwa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Ibara ya 51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.
Iabra ya 56. Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Iabara ya 68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.
Ibara ya 84 (9) Mtu yeyote ambaye si Mbunge atakayechaguliwa kuwa Spika, atatakiwa, kabla ya kuanza kutekeleza madaraka yake, kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu.
Ibara ya 103 (2) Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanizibar kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika na kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na Katiba ya Zanzibar, 1984.
Iabra ya 111. Jaji wa Mahakama Kuu hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapishwa kwanza kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungw na Bunge.
Iabara ya 121. Jaji wa Mahakama ya Rufani hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapishwa kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.
Tafsiri:
Iabra ya 151.-(1) "kiapo" maana yake itabidi ifahamike kwa maana ya kawaida ya
neno hilo na ni pamoja na tamko rasmi la namna yoyote linaloruhusiwa kisheria kutumiwa badala ya kiapo;
"kiapo cha uaminifu" maana yake ni kiapo cha kuwa mwaminifu kwa nchi na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.