Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

onesha ushahidi ambao wakati wa uteuzi wake aliagiza nyaraka za dini yoyote ndo tuanzie hapo.
 
Naona unazidi kuendekeza unafiki wako, Kwann akiteuliwa Muislam inakuwa issue sana na kila mtu ataimba udini, akiteuliwa mkristo mnalazimisha watu wanyamaze...

Serikali Haina dini ila ratio ya 90% kwa 10% kwenye uteuzi is merely unacceptable.
umeambiwa weka takwimu ya umahiri. sasa povu la nini tena. kulalamika hakusaidii
 
Mkuu kula nguruwe au kunywa pombe au kufanya lolote lile lililokatazwa na allah hakukufanyi kutoka ktk uislam huo ni uasi tu na kuhitaji kusilim upya pindi unapo amua kuacha maasi hayo.
Kwahiyo hiyo imani yako kuwa mislam akila nguruwe au kunywa pombe nk ndio katoka ktk uislam sio sahihi.
Nahiyo mikoa uliyo sema ina waislam wengu ongeza mingine kama mikoa ya znz na mingine ya bara nadhani hujafanya tafiti pana upo ktk hisia tu.
Kumbuka kama waislam tunaruhusiwa kuowa wake mpaka wanne kwahiyo hata ktk kuzaliana nadhani waislam wanazaa zaidi.
Na unapo tawala nchi kama hii yenye makabila na dini tofauti ni vyema ktk teuzi kuangalia cv, uwezo, kabila nahata dini .
kwamfano unahitaji wakuu wa mashirika 10 ya serikali nivyema watu 10 hao wakapatikana kutoka dini na kabila tofauti ili kuondoa hii misuguano isiyo ya lazima na zaidi kuleta umoja mshikamano na upendo ktk jamii zote za kitz.
Mm naamini wapo watz wa dini zote na makabila yote wenye cv na uwezo wa kuongoza.
 
Wagalatia wa Tanzania kwa unafiki bana leo hii tunaambiwa serikali haina dini wakati wa JK kila alimteua Muslim mlikuwa mnalalamika humu kuwa JK ni mdini.

Mwacheni Rais afanye kazi yake ................!!

Nyinyi ndiyo wapiga debe wakubwa wa Lumumba sijui mnalalamika nini? Kwa nini msizungumze haya kwenye chama kama ni kweli!!?
 
Unajua maana ya UADILIFU?
 
Hawa wote ni wana ushirika tunasali wote Kanisa la Mbezi na wengine wanasali Tegeta ni wana jumuiya hawana tatizo.

Ha ha ha ha

Mkuu ile Tanesco ni Dayosisi ya Tanesco usharika wa Ubungo Mkuu...

Ile ni kigango cha kanisa kabisa yanii

Ha ha ha

Christinization at its best level...

Mama yangu weeeeh....
 
Una uhakika gani kuwa hao wote ni wakristo ............ au unaangalia majina tu na kuconclude?
Mkuu unaingia ofisini unakuta watu wanaimba mapambio halafu unauliza jibu.
 
Mkuu heshima kwako, mkuu naomba nikushauri pamoja na kushauri wengine ya kuwa kupata cheo nafasi au utukufu wowote ule haupatikani ila mwenyeezi mungu apende, kwa hiyo kikubwa cha kufanya si kumlakamikia mr president na serikali yake kuwa hatuangalii waislam, cha kufanya sisi ni kumuelekea Allah kikweli, Allah anatuambia katika quran tukufu ya kuwa TUKIAMINI KIKWELI NA KUFANYA VITENDO VYEMA"ATATUFANYA KUWA NI MAKHALIFA KATIKA ARDHI KAMA ALIVYOWAFANYA KUWA MAKHALIFA WALIOKUWAPO KABLA YETU"
Kwa hiyo mkuu cha msingi ni kufuata zile sharti tulizopangiwa na Allah basi yote yatatufuata badala ya sisi kutumia jitihada binafsi, pia suala la elimu zote ni muhimu kulizingatia ili tujiweke katika mazingira mazuri ya kidunia hata kesho mbele ya Allah,
Inshaallah.
 
Kigezo cha dini na ukabila hakifai! angalia Record ya makosa, utaalam(usomi) umahiri wa kazi na nidhamu ya kazi. Mengine unatafuta kujiumiza kisaikolojia
 
Hii ilikuwa wakati ule uongozi ZAIFU.
 
Wewe hauwezi kuwa mkristo wewe ni muislam na ni moja kati ya waislam wa chache wenye fikra za ubaguz na kwakua wewe ni mbaguz utakacho kiona mbele yako ni kubaguliwa tu na sio vinginevyo
 
Nendeni shule na mfaulu manake ht shule zenu znaongoza kufelisha
 
Mfia Dini huna hoja
 
Mbona nyie wengi wenu mazezeta hivi huko msikitini mnaambiwaga nn icho mshindwe kuchuja mnakuja kuleta huku
 
Mkuu unaingia ofisini unakuta watu wanaimba mapambio halafu unauliza jibu.

Kwa hiyo hata hao waislam wachahche wanaimbishwa mapambio!!?

Ritz, nyinyi ndiyo huwa mnadai kuwa hao wagalatia wamepewa upendeleo kwenye elimu ......... labda mngeanzia huko kwanza. Mjikomboe kwenye elimu ndiyo mpiganie nafasi. Kulalamika kwa waislam kunadhibitisha kuwa hawana wasomi wa kutosha kupata hizo nafasi ............ unless mnataka tuje na kitu kama BEE kwa ajili ya Waislam!!
 
Mkuu, sio pattern inajirudia, ila ukweli ni kwamba tukiangaliwa huu upande wetu wa waislam, random selection ikifuatwa hatuwezi tukaingia wengi.. huo ndo ukweli. Historia inaonesha hawa wenzetu walisoma awali hivyo wana comparative advantge..pia huku bara wapo wengi sana kiasi kwamba probability of selecting randomly lazima wawepo wengi kutuzidi.. that is reality..tuhimize watu kusoma na kufanya kazi kwa bidii tuwe na sisi competitive in high position tuache kubebwa bebwa kila mara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…