Msaada wachambuzi :
Ngoja tuweke baraza la mawaziri awamu ya nne ya Mh. Jakaya Kikwete November 25, 2010 na wale wanaojadili dini wafanye uchambuzi wao yupi ni yupi na ni asilimia ngapi na pia labda tutaona Rais anapokuwa madarakani anatumia vigezo gani dini, CV, uswahiba, ukanda au nini :
Orodha kamili ya mawaziri na manaibu wao ni kama ifuatavyo:
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe;
2. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira;
3. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Hawa Ghasia;
4. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu;
5. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Luoga Hovisa;
6. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi;
7. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu;
8. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika;
9. Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo;
10. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha;
11. Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani;
12. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe;
13. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi;
14. Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David Mathayo;
15. Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa;
16. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka;
17. Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige;
18. Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja;
19. Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli;
20. Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu;
21. Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami;
22. Waziri ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa;
23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk. Haji Hussein Mpanda;
24. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka;
25. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba;
26. Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Emmanuel John Nchimbi;
27. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel John Sitta;
28. Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Prof. Jumanne Maghembe;
29. Waziri wa Maji; Prof. Mark Mwandosya
MANAIBU
1. Aggrey Mwanri;Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi),
2. Kassim Majaliwa;Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Elimu),
3. Gregory Teu;Naibu Waziri Wizara ya Fedha,
4. Pereira Ame Silima;Naibu Waziri Wizara ya Fedha,
5. Balozi Khamis Suedi Kagasheki;Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani,
6. Mahadhi Juma Mahadhi; Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje,
7. Uvuvi, Benedict Ole Nangoro; Naibu Waziri Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
8. Charles Kitwanga;Naibu Waziri Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
9. Goodluck Ole Madeye;Naibu Waziri Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
10. Adam Kigoma Malima;Naibu Waziri Wizara ya wa Nishati na Madini,
11. Dk. Harrison Mwakyembe; Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi,
12. Athumani Mfutakamba; Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi
13. Lazaro Nyalandu;Naibu Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara,
14. Philipo Mulugo;Naibu Waziri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
15. Dk. Lucy Nkya; Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
16. Makongoro Mahanga; Naibu Waziri Wizara ya Kazi na Ajira,
17. Umi Ali Mwalimu; Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,
18. Dk. Fenella Mukangara; Naibu Waziri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
19. Dk. Abdallah Juma Abdallah; Naibu Waziri Wizara ya Ushirikiano Afrika Mashariki,
20. Christopher Chiza; Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika,
21. Eng. Gerson Lwinge; Naibu Waziri Wizara ya Maji.
Wakongwe ambao wametupwa nje ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Seif Khatib Mohammed, ambaye amekuwa kwenye Baraza la Mawaziri tangu awamu ya pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Pia mkongwe mwingine aliyeachwa ni Profesa Juma Kapuya ambaye alikuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, akiwa amekaa kwenye Baraza tangu mwaka 1995 Rais Benjamin Mkapa alipoingia madarakani.
Mwingine ni Profesa Peter Msolla, aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, huyu aliingia na serikali ya Awamu ya nne, Januari 2006; Profesa David Mwakyusa aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia aliingia awamu ya nne.
Katika orodha ya walioachwa yumo pia John Chiligati, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, huyu alianza akiwa naibu tangu awamu ya tatu ya Rais Mkapa na Margaret Sitta, aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, aliingia na awamu ya nne.
Kundi hili linaungana na wale walioangushwa kwenye mchakato wa uchaguzi ambao ni Lawrence Masha (Mambo ya Ndani); Shamsa Mwangunga (Maliasili na Utalii); Diodorus Kamala (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Dk. Batilda Buriani (Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira) na Philp Marmo aliyekuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
Pia wapo manaibu walioachwa akiwamo mkongwe kwenye wadhifa huo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Dk. Maua Daftari ambaye amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu awamu ya Rais Mkapa; Hezekiah Chibulunje aliyekuwa Miundombinu naye alianza na awamu tatu na Jeremiah Sumari, aliyekuwa Naibu Fedha na Uchumi.
Source: IPPMEDIA
Home