Soma hadi mwisho uone kama una swali uniulize...
Mungu anayetajwa katika wimbo wa Taifa na pale katika sala za Bungeni ni Mungu wetu wa Pamoja. Nina hakika wewe unajua kwamba sisi binadamu tunaye Mungu wa Pamoja?
Mungu wa Pamoja ndiye yupi huyu? Mungu wa Pamoja ndiye yule ambaye dini zoooote zinamtaja kuwa aliumba ulimwengu. Huyu ndiye Mungu wa pamoja. Ujue dini zetu wanadamu zimeletwa na tafsiri tofauti-tofauti za huyu Mungu wa Pamoja.
Wanoabudu mizimu, wanamwomba Mungu kwa njia ya roho za babu zao. Yaani daraja lao kumfikia Mungu ni roho za mababu.
Wanaomwabudu Mohammad wanamwomba Mungu kwa njia ya roho ya Muhammad (ambaye kwa kweli naye ni Mzimu tu kama ile mizimu ya mababu)
Wanaomwabudu Yesu Kristo wanamwomba Mungu kwa njia ya roho ya Yesu Kristo (ambaye naye ni Mzimu tu kama ileile mizimu ya mababu zetu)
Freemason wanamwomba Mungu kupitia kwa Mtume wao Hiram Abith (nadhani ni Hiram Abith huyu; jina limenitoka kidogo kwa sabu mi si freemaon), naye huyu ni Mzimu tu kama ile mizimu mingine ya mababu, ambayo tunaitumia kama ngazi ya kumfikia Mungu--kila mtu akiwa na mzimu wake anayemwamini zaidi. Wengine Muhammad, Wengine Yesu, Wengine Hiram Abith, wengine babu aliyekufa 1945, na kadhalika na kadhalika.
Kwa hiyo ukiangalia vizuri unakuta wanadamu tunaunganishwa na Mungu wa Pamoja, ambaye tunadhani atatusikia vizuri wakati tukimwomba huruma na misaada kama tukimwomba kupitia kwa mizimu--kila mtu na mzimu wake anayemwamini zaidi.
Sasa nije kwenye Serikali. Serikali inakusanya watu hawa wote na mizimu yao yote hiyo. Ili kuleta Umoja na Mshikamano, Serikali inalazimika kutokufungamana na mzimu hata mmoja katika huo utitiri wa mizimu. Lakini inajua Mungu yupo. Hivyo Dawa imekuwa kumtaja tu huyo Mungu moja kwa Moja kwa sababu ni wa kila mmoja wetu.
Serikali inamtaja huyu Mungu wetu wa pamoja bila mizimu ili kujenga mshikamano wa kitaifa. Lakini kwa kutoa idhini hiyo mizimu kila mmoja wetu akaitaje kwenye nyumba yake ya ibada. Kwa hiyo anayetajwa katika Wimbo wa Taifa ni huyu Mungu wa Pamoja.
Una swali?