Nasisi tukazane kusoma ili tuwe na sifa za kuteuliwa maana miaka ya hapo nyuma tuliwekeza sana kwenye mdrasa wakati wenzetu wakipiga elimu dunia; mpaka sasa wenzetu wanavyuo vikuu lukuki, shule za msingi na secondary wanaongoza, hospitali nyingi tena zingine za rufaa nazo pia wanamiliki. Ila na sisi awamu iliyopita tulishika ngazi nyingi hasa zile za juu kuanzia mkuu wa nchi na makamu wake na mawaziri sehemu nyeti mfano fedha, ulinzi, Elimu.
Ushauri tu; ukidhani kuwa utachaguliwa kwa sababu ya dini yako, labda uende ukaishi nchi kama Iran, Iraq, Pakistan, Afghanistan, Uzubegjistan, Libya, Somalia, North Sudan, Oman, Indonesia, Malysia, Takijstan na makao makuu ya dini yetu huko Saudia. Katika nchi hizi ukisikika unataja kwamba "Jesus is the LORD and Savior" adhabu yake ni kunyang'anywa kabisa kichwa chako.
Nchi kama Zambia, UK, USA, German, Franch na nyinginezo za Ulaya zina alama ya Ukristo lakini muislam ana uhuru wa kutamka dini yake, ana uhuru wa kugombea uongozi, ana uhuru wa kujenga na kuupamba msikiti kadri awezavyo na hakuna mtu wa kumlipua bomu wala kumshambulia. Kizuri zaidi ni kuwa mtu yeyote anaruhusiwa kubadili dini kwa mda wowote tena hata akijitangaza hadharani ni sawa tu na jamii itaendelea kumpenda tu. Lakini kwa nilizotaja hapo juu, daaa! kesema tu Yesu anaokoa, kakichwa kangu kanatenganishwa na mwili wangu. Sasa unaweza kujua ipi ni dini ya aman kata ya hizi mbili, yenye kuwalazimisha watu kujiunga nayo au ile inayowaacha waamue wenyewe na bado ikabaki kuwapenda hata wale wasioikubali?
Kwa taarifa ni kwamba ukiwa unatafuta huyu na yule wameteuliwa kwa sababu ya dini yako, basi mawazo yako hayatofautiani na ya wale wanaokesha kwenye vikao vingi usiku na mchana wakitafuta ni namna gani eti sheria za dini yao ziwe sehemu ya katiba ya Tanzania kwa mpango mkakati kuwa eti siku moja dini yao itatawala na kuitangaza Tanzania ni dola ya dini yao. Jambo hilo ni ndoto za mtu anayeota anakojoa porini na kumbe anakojorea godoro alilolalia na mara aamkapo usingizini hutambua waziwazi kuwa ndoto yake ilikuwa ya uongo, tena kibaya zaidi amekojolea kitandani kwake. Ndivyo itakavyokuwa kwa wenye ndoto za dini yao kutawala Tz.