kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Baada ya Ikulu zote nchini Kisiwandui, Magogoni na Chamwino kukaliwa na Watanzania visiwani ndiyo nikaona umuhimu wa kuwa na serikali tatu au moja tu. Serikali tatu itasaidia kutunza siri na nyaraka za serikali ya Zanzibar na siri na nyaraka za serikali ya Tanganyika.
Serikali moja inasaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano iliyeko madarakani kuzifikia, kuzijua na kuzitunza siri za Zanzibar na Tanganyika kwa wakati mmoja tofauti na sasa ambavyo siri na nyaraka za wazanzibar ziko chini ya wazanzibar wenyewe lakini zile za Tanganyika ziko wazi kwa watanganyika na wazanzibar pia.
CCM imetufikisha hapa tulipo sana. CCM bara wako kwa maslahi binafsi ya matumbo yao, lakini CCM Zanzibar wako kwa ajili ya maslahi mapana ya Zanzibar.
Kama serikali ya Zanzibar lazima iwepo litoke jua inyeshe mvua basi kuirudisha Tanganyika hakuepukiki sasa ili kuweka mambo sawa.