Kama shabiki wa Yanga SC: Natamani Simba awe bingwa msimu 2016/17

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Salaam wana Jamvi,

Najua wengi wenu mmeshtuka na kustaajabu kwanini nimetamani iwe hivyo. Kwanza kabisa ningependa Ubingwa wa msimu huu uende kwa mtani wangu....si kwa sababu ana uwezo wa kuwa bingwa, au si kwa sababu Yanga SC hatuna uwezo wa kuwa bingwa ila ni matamanio yangu binafsi ya kuona watani zangu wakikata kiu yao ya takriban miaka 5(Bila Ubingwa wa LigiKuu).

Nasema hivyo kwa kuwa nina Jamaa zangu wa karibu sana ambao ni mashabiki wa MiKiA FC ambao walijawa na simanzi na hali ya kukata tamaa kabisa na timu yao baada ya Matokeo ya Kagera ambayo yaliwaonyesha kuwa wana nafasi ndogo kabisa ya kukata Kiu ua Ubingwa klabuni mwao.

Mimi kama shabiki mwenye huruma nikaona iwe bora tu wawe mabingwa wa msimu huu, ili tu kukata kiu yao na pia kutengeneza mazingira mazuri ya kuwa na msimu wa ushindani zaidi wa mwaka 2017/18.

Lakini kuna kitu kimoja kikanijia akilini.

Ni jina la mchezaji "Ramadhan Hassani KESSY'' ..Nikaaona haiwezekani huyu dogo hayafuate mafanikio Yanga SC halafu apishane nayo. Ghafla nikapungukiwa na huruma niliyokuwa nayo dhidi ya wale jamaa zangu wa MIKIA FC na kuona potelea mbali Kombe ni lazima lije Jangwani ili huyu dogo KESSY asijutie uamuzi wa kuja Jangwani.

Lengo la uhitaji wangu wa Ubingwa Jangwani ni kuona tamaduni yetu ikiendelea kudumu ...Tamaduni ya kuwa klabu ya kimbilio kwa wachezaji wenye nia na mafanikio ya mataji na kupata nafasi ya kushindana na vidume wengine wa bara la afrika.. sioni sababu ya kuwataja baadhi ya wachezaji waliokuja Yanga SC kwa lengo la mataji kwa kuwa kila mtu anawatambuaa. na msimu huu nataka uwe zawadi tosha kwa Hassan Ramadhani KESSY atakapo nyanyua ndoo kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake ya soka, Nadhani itakuwa fundisho kwa mastaa wengine wanaopoteza muda wao na kufikiria kuwa wanaweza kutwaa mataji wakiwa na vilabu vingine tofauti na Yanga SC.

Acha Kessy abebe ndoo kwanza, halafu mengine baadaye.

nawasilisha-
 
Mkuu sijakuelewa bado. Unataka wachukue au wasichukue ?, mwishoni ndiyo umeharibu
 
Simba anastahili kuwa bingwa kwa msimu huu kwa sababu;-

1. Ubora wa Yanga waliokuwa nao kwa misimu 2-3 hivi na hasa msimu uliokwisha umeporomoka kwa kiwango kikubwa.
2. Azam imeporomoka pia, na kimsingi wameshapotea , kwa sababu matokeo yao ni kama homa za vipindi
3. Ubora wa Simba umeongezeka sana tofauti na Simba ya misimu 2 iliyopita
4. Kwa maana ya mwendelezo wa ubora tangu msimu uanze, ndio timu bora ktk Ligi Kuu ya VPL

Kwa faida ya mpira wa nchi, ni mbaya sana kuwa na timu iliyoshuka kiwango na haina morari halafu bado inaendelea kuwa bingwa
 
timu haina morari na imeshuka kiwango then anakupita?maana yake na nyie mna timu mbovu,tena Sana...mnataka tujifungishe ili muwe mabingwa?acheni lawama form is temporary but class is permanent.....hakuna msimu niliowadharau kama huu.tungekuwa fiti nathani tungekuwa tumeshatangaza ubingwa kitambo Tu ...mikia loosers
 
Mashudu ya kiwango cha juu
 
Nadhani hapa umekubali kuwa Yanga haiko fit kwa sasa. Watu wote wenye akili hata Lwandamina wanalijua hili. Mashabiki oyaoya ni ngumu kuliona hili.

Na huu ni ukweli mchungu kwa Simba kujitathmini upya. Ikishindwa kuchukua ubingwa mwaka huu itakuwa ni the biggest failure kama ile ya msimu wa 2010/2011 au ile ya Liverpool ya 2014/2015
 
Te

uko sahihi mkuu majeruhi kibao,timu haina economic stability ...
 
Simba anastahili kuwa bingwa kwa msimu huu kwa sababu;-

1. Ubora wa Yanga waliokuwa nao kwa misimu 2-3 hivi na hasa msimu uliokwisha umeporomoka kwa kiwango kikubwa.
2. Azam imeporomoka pia, na kimsingi wameshapotea , kwa sababu matokeo yao ni kama homa za vipindi
3. Ubora wa Simba umeongezeka sana tofauti na Simba ya misimu 2 iliyopita
4. Kwa maana ya mwendelezo wa ubora tangu msimu uanze, ndio timu bora ktk Ligi Kuu ya VPL

Kwa faida ya mpira wa nchi, ni mbaya sana kuwa na timu iliyoshuka kiwango na haina morari halafu bado inaendelea kuwa bingwa
simba Tim yang ila wanazingua
 
Back
Top Bottom