demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Salaam wana Jamvi,
Najua wengi wenu mmeshtuka na kustaajabu kwanini nimetamani iwe hivyo. Kwanza kabisa ningependa Ubingwa wa msimu huu uende kwa mtani wangu....si kwa sababu ana uwezo wa kuwa bingwa, au si kwa sababu Yanga SC hatuna uwezo wa kuwa bingwa ila ni matamanio yangu binafsi ya kuona watani zangu wakikata kiu yao ya takriban miaka 5(Bila Ubingwa wa LigiKuu).
Nasema hivyo kwa kuwa nina Jamaa zangu wa karibu sana ambao ni mashabiki wa MiKiA FC ambao walijawa na simanzi na hali ya kukata tamaa kabisa na timu yao baada ya Matokeo ya Kagera ambayo yaliwaonyesha kuwa wana nafasi ndogo kabisa ya kukata Kiu ua Ubingwa klabuni mwao.
Mimi kama shabiki mwenye huruma nikaona iwe bora tu wawe mabingwa wa msimu huu, ili tu kukata kiu yao na pia kutengeneza mazingira mazuri ya kuwa na msimu wa ushindani zaidi wa mwaka 2017/18.
Lakini kuna kitu kimoja kikanijia akilini.
Ni jina la mchezaji "Ramadhan Hassani KESSY'' ..Nikaaona haiwezekani huyu dogo hayafuate mafanikio Yanga SC halafu apishane nayo. Ghafla nikapungukiwa na huruma niliyokuwa nayo dhidi ya wale jamaa zangu wa MIKIA FC na kuona potelea mbali Kombe ni lazima lije Jangwani ili huyu dogo KESSY asijutie uamuzi wa kuja Jangwani.
Lengo la uhitaji wangu wa Ubingwa Jangwani ni kuona tamaduni yetu ikiendelea kudumu ...Tamaduni ya kuwa klabu ya kimbilio kwa wachezaji wenye nia na mafanikio ya mataji na kupata nafasi ya kushindana na vidume wengine wa bara la afrika.. sioni sababu ya kuwataja baadhi ya wachezaji waliokuja Yanga SC kwa lengo la mataji kwa kuwa kila mtu anawatambuaa. na msimu huu nataka uwe zawadi tosha kwa Hassan Ramadhani KESSY atakapo nyanyua ndoo kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake ya soka, Nadhani itakuwa fundisho kwa mastaa wengine wanaopoteza muda wao na kufikiria kuwa wanaweza kutwaa mataji wakiwa na vilabu vingine tofauti na Yanga SC.
Acha Kessy abebe ndoo kwanza, halafu mengine baadaye.
nawasilisha-