Mzee Nyerere
JF-Expert Member
- Jun 24, 2024
- 219
- 279
Kufanya Uchaguzi Mkuu tarehe 25|10|2025 kwenye nafasi ya Urais wa JMT ni matumizi mabovu na mabaya ya pesa za walipa kodi hawa wachache na masikini kabisa.
Kama Fedha ya Uchaguzi ni zaidi ya TZS 700BL, Pesa hii ingesaidia zaidi kutuletea Maji safi na Salama pamoja na kukamilisha reli yetu ya SGR hasa kwa Vipande Vya Tabora Kigoma na Tabora Mpanda ambavyo havijaanza kabisa.
Kwa Mambo aliyoyafanya na anayoyafanya Rais Samia kwa miaka hii mitatu kugombea nae kama mpinzani ni kutaka kujifedhehesha tu mbele ya Watanzania kwa kupata vikura kiduchu sana.
Najua Kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa lakini unachaguliwaje mbele ya Rais Samia? hata kama wafuasi wako wanakudanganya utashinda lakini nafsi yako itendee haki pia.
CHADEMA jiimarisheni kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani, hii ya Urais mtajidhalilisha na huenda mkapoteza kabisa mvuto wenu kidogo mliosalia nao kwa sasa huku mitaani.