Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,008
- 17,480
Rejea kichwa cha somo hapo juu chausika.
Wakati mwingine si vibaya kushirikishana uzoefu katika maisha tuliyopitia. Kwa umri wangu nimeona mengi na ninajua ninachokisema na walio wa kweli watanielewa. Misingi ambayo familia zoote za Kiafrica, zimejengwa katika kitu kinachoitwa mila na desturi za ukoo wetu. Hiki kitu kinachoitwa mila na desturi ni maagano ya matambiko ya mizimu na mashetani ya kuitolea kafara kila msimu waliokubaliana nayo ambayo yameridhishwa kutoka uzao hadi uzao.
Hayo maagano ni kwa ajili ya nia njema ya kulinda usitawi wa familia katika nyanja za uchumi, kuoa na kuolewa, elimu, vyeo, kuwa kiongozi katika jamii, mamlaka, n.k, n.k.
We angalia wenzio uliosoma nao au kukua nao au kucheza nao au kuajiriwa nao pamoja, au kuanza nao biashara na angalia tofaouti yao na wewe. Kama umejikuta maisha yako yamekuwa mepesi katika nyanja nilizozitaja na nyingine ambazo sijazitaja lakini unaona kwa upande wako pamekuwepo wepesi wa kufikia mafanikio na malengo uliyofikia, NAKWAMBIA kamuulize mama, Baba, Babu!, Bibi (kama bado wapo).
Wee waendee kwa upole na busara na hekima (maana haya mambo ni siri). Wadadisi kuwa: Pamoja na juhudi ninazoziweka katika maisha ebu niambie siri za mafanikio yangu. Au kwanini nakwama kila ninachotia mkono kukifanya?
Nakumbuka familia moja (kapuni). Baba alikuwa mtu wa kanisani na wote katika familia walikuwa wanasisitizwa kwenda kanisani! Pia, na kuomba (familia nzima) kabla ya kulala! Miaka ikaenda mpaka watoto wakawa wakubwa wakamaliza kidato cha nne wakafaulu kwa kusuasua! Maisha ya kiuchumi ya familia hiyo yakaanza kwenda mrama. Ndipo mama wa familia hiyo akatafuta kondoo mweupe akamwambia kijana wake wa mwisho wa kiume na mfanyakazi wake wampeleke huyo kondoo kwao na mama! Walipofika huyo kondoo alichinjwa kwenye kijumba fulani cha nyasi kilichoko mita kama 30 kutoka nyumba kubwa na damu ya huyo kondoo ikatamkiwa maneno fulani wakati inachuruzika.
Alafu wakachukua maini yakiwa ya kwanza na kuyaweka kwenye chombo maalumu na kuyaacha hapo kwenye kinyumba. Nyama ya huyo kondoo ikachinjwa na kuwa kitoweo kama kawaida! Baada ya hapo huyo mtoto karudi kwao.
Baada ya wiki kaka yake aliyekuwa amefaulu kwa kusuasua akajitokeza mtu fulani mwenye cheo kikubwa serikalini kamchukua na kumtafutia kazi na kuanzia hapo maisha yakamnyokea na kuwa baraka na neema katika familia nzima! Hila cha ajabu alipatwa na ugonjwa wa maini (kumbuka yale maini ya kondoo wa kafara) na alipokwenda hospitali walimwambia ugonjwa huu kawaida hauponi isipokuwa itakubidi usile vyakula fulani na ameishi na ugonjwa huo mpaka sasa ila kwakweli maisha yake safi saaana na familia inajivunia.
Sasa anayejua siri ya kilichofanyika ni mama yake peke yake na familia iliendelea kukua katika imani ya dini ya baba yao! Huu ni mfano mmoja chanya lakini kwa upande mwingine ni matatizo makubwa ndani ya familia nyingi za kiafrica kama aliyeingia maagano ya kafara na mizimu na mashetani akifa bila kumuachia mtu wa kuendelea kuyatolea sadaka ya makafara hiyo mizimu na mashetani utaangaika weee utaomba na kufunga utasoma mpaka Ulaya utaanzisha kila aina ya biashara, utaajiriwa lakini usogei, utaoa na kuolewa (ikitokea) lakini shida tupu, au utapumbazwa na kipato cha kiaina lakini ukijitafakari unaona unapiga mark time, HUSOGEI.
Kwa kizazi cha leo ambacho hakiamini katika mila na desturi nadhani kiko kwenye hatari zaidi kikijitahidi kutafuta njia mbadala utasikia free mason, waganga wa kienyeji, n.k. Cha kufanya rudini kwenu kawaulize kwa busara wazee wenu kulikoni? Mbona nakwama?
Na uwaulize kwa busara maana haya mambo yanafanyika kwa siri! Bora umjue Adui yako alipo ili ujue umpigeje? If you can't defeat him, then join him!
Hii mada ni kwa wakubwa, vijana nyamazeni.