Kama sio mama yako, basi ni baba, bibi au babu yako ndo wanajua siri ya hali yako ya maisha

Kama sio mama yako, basi ni baba, bibi au babu yako ndo wanajua siri ya hali yako ya maisha

Kuna ile mtoto akiwa mdogo anakua ananenewa maneno, mengine yanakua ni baraka na mengine ni laana, hayo maneno huambatana saa zingine na mila ikiwa ni pamoja na kutoa sadaka.
Mara nyingi hizo sadaka huwa ni pombe ina miminiwa sehemu za matambiko au mnyama ana chinjwa na damu ina mwagwa pale.
TUMAINI LIPO KATIKA JINA LA YESU, unaweza fanya maombi ya kuvunja maneno na matambiko yote uliofanyiwa ukiwa mtoto mchanga ili usifanikiwe au kurithi malaana ya ukoo.
Una safisha kwa DAMU YA YESU.
 
Msahada pekee wa kuondokana na maagano ya wazazi wetu na mababu wa mababu zetu katika familia na koo zetu ni NENO la MUNGU! Tatizo wa kutufundisha ni nani? Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu! Tatizo nani wa kutufundisha neno la Mungu ili tupate imani ya kuondokana na maagano ya matambiko ya makafara ambayo koo zetu na familia zetu waliingia na kutukwamisha kimaisha au kuonekana tumefanikiwa lakini tumebeba mizigo ya magonjwa (kama kuharibika ini kwa huyo jamaa) au mashambulizi mwisho wa siku kuwapata watoto na uzao wetu mbeleni!!
 
Wapo watumishi wa MUNGU, wanafundisha inatokea tuu kwenye ibada mtumishi anaamua kufundisha ilo somo, au wewe unamfata na kumuambia unachotaka...maagano mengine ni lazima ufanye maombi ya kufunga.
 
Haya Mambo ya wazee huwa ni Magumu kuyajua na yanachukua Muda mrefu kuyathibitisha.

Kuna Babu yetu alikua akitembelea Familia yetu mara chache sana katika miaka mingi. Alikua na Uwezo wa ajabu wa kutabiri mtoto huyu atakuaje na huyu atakuaje kadri ya tabia asilia za huyo mtoto.

Wakati huo mimi nilikua mdogo miaka nane au tisa hivi, basi alikua akija nyumbani mimi ndio nakua mwenyeji wake wa kumtembeza tembeza na kumpeleka maeneo mbalimbali.

Kuna siku nimemtembeza na kumdadisidadisi ile ya kitotokitoto basi tukarudi home mida ya jioni ndipo Babu akamwambia Mama yangu, Mkamwana wake sasa kwamba huyu kijana ni mkarimu sana kuliko wajukuu zangu wote na atakua na Maisha mazuri na atasaidia Familia hata Ukoo mzima, hana hira moyoni mwake. Babu aliendelea kurudiarudia maneno hayo mara nyingi sana.

Hata wazazi wetu au mtu yeyote alieenda kumsalimia au kumtembelea babu huko kijijini kwao alipewa salamu maalumu za kwangu mimi tofauti na mjukuu yeyote. Babu alinielezea hata kwa ndugu wengine maeneo mengine.

Ilichukuliwa kama kawaida wakati huo, japo nilimsikia mama mara chache chache akielezea utabiri huu wa babu kwa ndugu na jamaa wengine.

Miaka imeenda mpaka habari hii ikasaulika kwani Babu alifaliki na mama pia akafariki watu ambao waliujua utabiri huu. Mimi niliujua utabiri huu na nikawa wakati mwingine nadhani ilikua ni maneno tu ya Babu kwani sikuona hata vidalilidalili ya hayo kutokea japo wakati mwingine nilona viashilia kadhaa hasa niliposhinda changamoto kadhaa ambazo kwa hakika bila nguvu za Mungu isingewezekana.

Leo hii Nimeona neno alilonitabiria Babu miaka mingi limetimia kwa ukamilifu kabisa. Napoandika habari hii mimi leo kwenye Familia na hata koo mbili zote yaani upande wa Baba na upande wa Mama mimi ndio mtu mwenye uwezo mkubwa kimafanikio.
Wanakadiria hata Mali za Familia au koo zote mbili zikijumlishwa huenda zisifikie mali nilizonazo na zinazoendelea kuja.

Na pia nimekua msaada mkubwa sana kwa Familia na hata koo zote mbili. Katika mambo mengi lazima nihusike ndio yaende vizuri. Sio kwa pesa tu hata maamuzi mengi ninayoshauri yamekua na busara nyingi kwa Familia na Ukoo. Hili limetimia baada ya miaka mingi tena wakati Babu na Mama watu walioliteta hili mimi nikiwa darasa la kwanza hawapo.

Pia Babu aliwahi kumtabiria Dada yangu mmoja kua yeye atakua na Familia kubwa na kwamba ndio atakua kama mama yetu miaka mingi. Na kweli hili lilikuja kutokea baada ya Mama yetu kufariki, huyu dada ndio akawa msingi wa Familia yetu, yaani katika Watoto kumi na moja wa Familia yetu hakuna hata mmoja wetu ambaye hakupita kwa huyu Dada yetu, ili ajistili au kusaidiwa kwa namna moja au nyingine tena bila Kinyongo cha Dada yetu au hata Shemeji yetu, na kwa asilimia nyingi ametulea na amelea hata Dada zake waliomtangulia.

Kifupi ni kwamba Wazee wetu hasa Mababu zetu walipewa siri nyingi kwa uwezo waliopewa na mungu. Babu yetu alikua Msabato Mtiifu sana.
 
Utakuwa umetumwa na Lusufer wewe.

Watu tulisha ondokana nayo na kuwa huru wewe unatusihi turudi utumwani,ni Nani anataka kuwa chini ya?
Na Mambo yanaenda Mimi nilitoa tamko nipo tayari kufa siyo kukosa utajiri tu.

Mungu ni mwema maisha ni mzuri waliobaki upande ule nimewaacha kilomita nyingi tu.mimi siyo tajiri ila naridhika nilipofikia naona ninachokifanya .

Mwisho niulize swali ukishapata hayo maisha mazuri alafu? Utaondoka na nao ? Nafsi yako itatulia?
Wito wangu vunjeni hayo maagano bila kurudi nyuma au kuangalia nyuma hakuna baya litakalo kupata

Sent using Jamii Forums mobile app
ndo nyie mkianza kuomba amtaki kuuliza, amtaki kujua mwanzo wala mwisho nyie ni kuvunja na kuteketaza nakuangamiza tu!

unamjua adui yako?
unajua sababu ya wewe kuishi hivyo ulivyo sasa?
nduo maana ya kuwakalisha wazee uwaulize kwa busara, kilikoni?? mbona mambo yangu meusi? daily

sio pepo tokaaa tokaaa alafu hata ujui pepo mwenyew aliingilia wapi
 
Mwendee Mungu atakufunulia kila kitu. Maisha nayoishi niliyaonyeshwa tangy 2014, bila Mungu kuwa ameshanionyesha, huenda ningeshakufa kwa stress, lakini sasa napunguza mawazo kwa vile kila mipango ya kuzimu inawekwa kwangu kabla.
 
ndo nyie mkianza kuomba amtaki kuuliza, amtaki kujua mwanzo wala mwisho nyie ni kuvunja na kuteketaza nakuangamiza tu!

unamjua adui yako?
unajua sababu ya wewe kuishi hivyo ulivyo sasa?
nduo maana ya kuwakalisha wazee uwaulize kwa busara, kilikoni?? mbona mambo yangu meusi? daily

sio pepo tokaaa tokaaa alafu hata ujui pepo mwenyew aliingilia wapi
Kama wazee wameingia maagano hawatakuambia asilani. Fikiria mzazi awe mchawi na huko uchawini alazimishwe kuharibu mambo yako kwa faida ya wachawi, atakuambia hata ukimwendea kwa upole?

Hakuna siri iliyositirika mbele za Mungu, mwendee Mungu.
 
Umejichanganya katika maelezo! Hatusupport mambo hayo pia! Tunaongelea hali halisi ya familia zetu! Kuvunja na kuachana na hayo maagano kunawezekana ila uwe umejipanga na silaha nzito kuliko adui!
Anakwambia yeye hatishwi na kukosa utajiri, maana yupo tayari hata kufa ,kuliko kushiriki Mambo hayo.
Kujikana, kujikubali na kujiamini, Ni silaha kubwa na nzito kuliko silaha yoyote katika mapambano ya mwanadamu na maisha yake.
Mbona mleta mada nae kajichanganya?
Eti yule aliemtolea mfano Mambo yake mazuri ila anaumwa maini!!!!!!
Uzuri wa maisha upo wapi hapa?
 
Hadi ukwame ndiyo urudi?
Wenzio Kila mwisho wamwaka Wana timiza Yao.
 
Back
Top Bottom