Kama Slogan yako ni ya 'Kazi Iendelee' kwanini Wamachinga hawana imani nawe?

Mkuu umenichekesha [emoji23][emoji23][emoji23]. Uliona oooh hoooo. Hapa masela wamejaa watanipumzikia na hizi hasira walizonazo
 
Mwendazake alitaka wananchi wa tanzania wawe na thamani sawa na wageni kutoka nje. Kama ww unavoenda ulaya. Unakuta wazawa wanathamani na maisha mazuri kuliko ww. Sio foreigner anakuja ugenini anaishi vizuri masaki na mwenyeji haruhusiwi hata kukanyaga masaki na kufanya biashara
 

wakati ule Wamachinga na Wanyonge wakionyeshwa upendo na mwendazake pia kunawatu walilalamika kuwa mwendazake anaupendo nao,miongoni mwao walikuwa walimu, watumishi wa uma,matajiri na wanasiasa wapande zote mbili upinzani na chama tawala. Kwahiyo kila zama na kitabu chake...wanyonge wajinyonge tu hakuna namna....ila haki zao watazipata tu
 
JPM alipandikiza mzimu kwa hao jamaa msiwaonee,msiwadhulumu wala msiwanyanyase...
waelimishwe taratibu wataelewa....
 
Mama wala simuamini.
 
Naona Sukuma Gang kazini. Hamuamini Mwendazake keshaoza
 
Wangeachaje kumpenda wakati aligawa mahela barabarani.
Aliwapa barabara zilizojengwa kwa gharama na malengo maalumu kujaza vitu vyao.
Aliwagawia vitambulisho vya 20,000 kufanya biashara kwa uhuru
Aliwasemea aliobatiza wanyonge na kuwatetea huku akitumbua na kuteua jambo wanalopenda wanyonge.
Ok. Mengine yasingeweza kudumu mfano ikiwa kila siku wamachinga wanazaliwa ingefika siku barabara zote zingejaa.
Sasa ni wakati wa kurekebisha sio kijipendekeza
 
Eti ndio walimpa kura..akili sijui za wapi hizi
Labda za "Dom kama si Chattle!!"
Mtu unakaa chini unajiuliza hivi kizazi cha hawa waitwao na kujiita "wanyonge" wakikua wanawaona wazazi wao wakipanga bidhaa barabarani na kuziba maduka ya wenzao au malango ya hospitali wakikua tutakuwa na pa kupita kweli? Maana kizazi hicho kila watakapoona lami watajua ni eneo lao la kupanga biashara zao na kutupa uchafu...
Hili bomu liteguliwe mapema kabla madhara hayajazidi... Hivi watendaji wa mitaa, wakurugenzi, wakuu wa wilaya na mikoa wanakwama wapi?
 
Magufuli hapendi kufuata utaratibu na wamachinga hawapendi kufuata utaratibu ndo maana wamemmiss, wao kila eneo wanataka kupanga biashara, kutokufuata kwao utaratibu unakupa TRA wakati mgumu
 
Mwendazake hakuwahi kuwa na upendo na mtu yeyote. Kila kitu alifanya kwa unafiki. Na ukiwa na akili ndogo, ungeweza kuamini kuwa anawapebda maskini.
 
Utawala wa sheria ukifuatwa hakuna atakayekuja kulalama kuonewa, maana kila mtu anazingatia haki yake, sasa machinga wanaziba barabara na wanataka iwe hivyo hata hivyo hakuna kanuni zilizoruhusu haya, Mtu mmoja aliamka asubuhi aksena wekenni mahali popote na ikawa hivyo lakini hakuna sheria inayoruhusu machinga barabarani wana sehemu zao wametengewa kwanini wasiende huko? Rais Samia kama ana mpango wa kuwaondoa barabarani wala si yeye atakayesema waondoke, Kwani wakurugenzi na halmashauri kazi yake nini?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…