Kama Taifa hatupaswi kujutia kumpata mtu aina ya Hayati Magufuli

Kama Taifa hatupaswi kujutia kumpata mtu aina ya Hayati Magufuli

Siku moja nilikuwa Kahama. Magufuli akiwa Waziri. Tukawa tunajadili nani anafaa kuwa Rais.

Kwa kuangalia ule utendaji kazi wa Magufuli, mimi nikalitaja jina la Magufuli. Mzee mmoja ambaye alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, akamaka, akasema, ' tema mate chini, balaa hilo lisitokee'. Alielezea sana, na ilionekana anamfahamu sana, kuliko wote tuliokuwepo pale.

Alipoteuliwa tu kuwa mgombea, niliyakumbuka maneno ya yule mjumbe wa NEC. Nikiwa Dar, tayari Magu akiwa ameteuliwa na kuzindua kampeni, mzee mmoja aliyekuwa ofisi ya Waziri
Mkuu, akasema, 'sijui, yaani John awe Rais, hii nchi itawaka moto. Magonjwa ya akili huwa hayaponi moja kwa moja'.

Nikayaweka maneno ya hawa wawili moyoni. Magufuli alivyoanza uongozi, hakika nikakubali kuwa wale watu wawili walikuwa wanamfahamu vizuri. Walikuwa sahihi sana.

Lakini kwa vyovyote, wanaostahili kulaumiwa sana ni Kamati Kuu ya CCM. Wao walikuwa wanamfahamu vizuri kuliko sisi sote. Nadhani alistahili kuishia kwenye utendaji na siyo kuwa kiongozi mkuu, nafasi inayohitaji mchanganyiko wa karama, na zaidi hekima.
Duh
 
Back
Top Bottom