Kama Taifa, huu ndio wakati wa kuweka siasa kando. Ni wakati wa kuchukua maamuzi sahihi

Kama Taifa, huu ndio wakati wa kuweka siasa kando. Ni wakati wa kuchukua maamuzi sahihi

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Wantanzania kama taifa tupo katika kipindi kigumu sana.Maambukizi ya huu ugonjwa yameongezeka kwa kasi (Covid -19).

Kama taifa inatupasa tuweke siasa kando. Tushikamane ili kupambana na hili janga. Kama jamaa zetu kule China wana namna ya kupambana na huu ugonjwa basi tuwanonog'eze watuambie ni hatua zipi za haraka tuchukue.

Mpaka sasa total reported cases ni kama 170.Ila waliopona ni wachache sana ukilinganisha na maambukizi, maana wamepona watu 11. Hii inaonyesha wanaopona ukilinganisha na maambukizi ni ratio ndogo sana.

Nina hakika kabisa kabisa huduma za afya hapa Tanzania ni duni ukilinganisha na mataifa kama Usa,Italy, Spain au Italy. Hivyo kama wagonjwa wakiongezeka itakuwa balaa kubwa.

Nashangaa sana kuna watu ati kisa ni wafuasi wa vyama vya upinzani basi wao wanafurahia hili janga liliwaue watanzania kwa wingi. Kisa tu serikali iliyopo madarakani ionekane imefeli kukabiliana na hili janga.

Hii haijakaa vizuri kabisa.
Kama taifa tuonyeshe umoja kwa kila namna ili kila mtu atoe mchango wake wa kila namna ili kukabiliana na hili janga. Tuache siasa za kupotosha au kupunguza morale ya kupambana na hili janga.
 
Hili bandiko lako ni la kuwachafua wapinzani wala hukuwa na haja yoyote ya kuanzisha uzi, bali ungechangia humo humo ulipoona huo upotoshaji. Nilidhani una suluhisho la huu ugonjwa, kumbe unaonyesha hisia zako hasi dhidi ya upinzani. Hakuna asiyepambana na huu ugonjwa, ila kupambana na huu ugonjwa kwa maombi, ni usanii maana sio tatizo la kiroho bali la kisayansi.
 
Ndio matatizo yenyewe haya... Huna imani kwamba Mungu anaepusha majanga?
 
Si kweli kuwa wapinzani wanafurahia huu ugonjwa kuongezeka isipokuwa wanaisuta serikali kwakuwa ili kataa kila ushauri iliyopewa na wapinzani kukabiliana na ugonjwa huu.

Waliishauri serikali izuie wageni kutoka nje ika kataa na kuendelea kupokea wageni na hasa watalii kutoka China.

Ugonjwa ulipoingia walioanza siasa ni CCM. Polepole alisema wapinzani ni kama korona. Makonda akamshukuru Mungu kwa mtoto wa Mbowe kuugua korona.

Serikali imefunga shule na vyuo lakini wanashauriwa wazuie mikusanyiko yote isiyo ya lazima ikiwemo ya ibada wamekuwa wabishi mpaka imefikia hatua baadhi ya viongozi wa dini wameamua kusitisha baadhi ya huduma na wengine kufuta ibada/misa kabisa.

Kwahiyo aliyeingiza siasa katika vita dhidi ya korona ni CCM siyo wapinzani. Ila sasa mambo yamegeuka mnaanza kutapa tapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio matatizo yenyewe haya... Huna imani kwamba Mungu anaepusha majanga?

Nina imani na Mungu ila sina imani na mbwembwe za kisiasa kwenye ibada. Hilo gonjwa tulianza kuomba kabla ya kuingia hapa, lakini limeingia. Kwahiyo hilo gonjwa suluhisho lake sio maombi bali kupambana nalo kwa kufuata taratibu za kiafya. Ukiona kiongozi anasema watu wasali ili corona iondoke ujue huyo ni tapeli.
 
M

Mungu anatupa maarifa tupambane na majanga kama haya. Hivyo si suala la kupuuza.
 
Ninyi CCM mnaweza na Mungu yupo upande wenu
Sisi wapinzani ni dhaifu tena Mungu hatupendi maana tunaropoka na kutetea mabeberu
Tena ni lengo la Ccm kuua upinzani ili ibaki pekee yake

Sasa mnataka tushirikiane ili iweje?
Sisi ni dhaifu hatuwezi kushindana na kitu ninyi mnaoweza kujenga maSGR pekee ndio mnaweza ondoa Corona
 
chagu wa malunde mjibu huyu jamaa
Si kweli kuwa wapinzani wanafurahia huu ugonjwa kuongezeka isipokuwa wanaisuta serikali kwakuwa ili kataa kila ushauri iliyopewa na wapinzani kukabiliana na ugonjwa huu.

Waliishauri serikali izuie wageni kutoka nje ika kataa na kuendelea kupokea wageni na hasa watalii kutoka China.

Ugonjwa ulipoingia walioanza siasa ni CCM. Polepole alisema wapinzani ni kama korona. Makonda akamshukuru Mungu kwa mtoto wa Mbowe kuugua korona.

Serikali imefunga shule na vyuo lakini wanashauriwa wazuie mikusanyiko yote isiyo ya lazima ikiwemo ya ibada wamekuwa wabishi mpaka imefikia hatua baadhi ya viongozi wa dini wameamua kusitisha baadhi ya huduma na wengine kufuta ibada/misa kabisa.

Kwahiyo aliyeingiza siasa katika vita dhidi ya korona ni CCM siyo wapinzani. Ila sasa mambo yamegeuka mnaanza kutapa tapa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida kubwa yenu CCM na wafuasi wake mnadhani kila anaewashauri Ni mpinzani wenu na badala mfikirie mnachoshauriwa mnakuja juu kwa mbwembwe kuonesha kila wanachosema wapinzani au wasio Wana CCM Ni makosa. Hapa ndio huwa mnakosea sana alafu mkiona kushindwa mnakuja kusema tushirikiane Kama Taifa. Na hii si Mara moja Wala Mara mbili. Ni kuanzia kwenye mashindano ya mipira kimataifa Hadi majanga mbali mbali.

Hamkuwa na haja kufananisha wapinzani Kama corona na kusema mtaishinda tu Ni kaugonjwa kadogo. Ilitakiwa pale pale mwanzo tungeshauriana Kama Taifa sio baada ya kutumia mabavu na kuona mnashindwa.

Mlifurahia mtoto wa Mbowe kuugua Corona mkasahau ndio kwanza janga lilikuwa linaanza. Sijui kusimama Kama Taifa kulikuwa wapi kipindi mtoto wa Mbowe anaumwa Corona!

Hakika mnatumia siasa vibaya Sana. Kuna Mambo ya kufanya siasa na yakipita maisha ya Taifa, undugu, uTanzania lazima uendelee. Haiwezekani kila wanachoshauri wapinzani na watu wasio CCM mnatupilia mbali na kuwaona wao ni waTanzania nusu na nyie ndio wenye haki kuwa waTanzania kamili simply because mmeshika dola!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wantanzania kama taifa tupo katika kipindi kigumu sana.Maambukizi ya huu ugonjwa yameongezeka kwa kasi (Covid -19).
Kama taifa inatupasa tuweke siasa kando. Tushikamane ili kupambana na hili janga. Kama jamaa zetu kule China wana namna ya kupambana na huu ugonjwa basi tuwanonog'eze watuambie ni hatua zipi za haraka tuchukue.
Mpaka sasa total reported cases ni kama 170.Ila waliopona ni wachache sana ukilinganisha na maambukizi, maana wamepona watu 11. Hii inaonyesha wanaopona ukilinganisha na maambukizi ni ratio ndogo sana.
Nina hakika kabisa kabisa huduma za afya hapa Tanzania ni duni ukilinganisha na mataifa kama Usa,Italy, Spain au Italy. Hivyo kama wagonjwa wakiongezeka itakuwa balaa kubwa.
Nashangaa sana kuna watu ati kisa ni wafuasi wa vyama vya upinzani basi wao wanafurahia hili janga liliwaue watanzania kwa wingi. Kisa tu serikali iliyopo madarakani ionekane imefeli kukabiliana na hili janga. Hii haijakaa vizuri kabisa.
Kama taifa tuonyeshe umoja kwa kila namna ili kila mtu atoe mchango wake wa kila namna ili kukabiliana na hili janga. Tuache siasa za kupotosha au kupunguza morale ya kupambana na hili janga.
Pole sana ndugu yangu! Leo unaona wapinzani kuwa ndo tatizo katika mapambano dhidi ya korona wakati wao si watendaji na hawana mamlaka yoyote! Kumbuka wao walishatimiza wajibu wa kuishauri serikali ichukue hatua gani dhidi ya tishio la mlipuko huu lakini je ni ushauri gani ulizingatiwa zaidi ya kubezwa.

Lakini kama kweli unataka watu waache siasa unadhani ni upande upi unatakiwa ubadilike; watawala au wapinzani? Unadhani zaidi ya kutoa ushauri ni jambo gani lingine ambalo wapinzani wanaweza kufanya kuonesha huo mshikamano?

Unamjua Freema Mbowe? Mtu huyu ndo "gear changer" wa siasa za Tanzania. Binafsi naamkataa kwasababu kitendo chake cha "kubadili gia angani" ndio chanzo cha siasa za hovyo tunazopitia hivi sasa. Hata hivyo natambua na kumtaja kuwa alishaomba na hadi sasa anapigia kelele pawepo na mwafaka wa kitaifa. Je, Mbowe alionanini mbele? Aliiona korona ambayo leo wewe unataka pawepo na mshikamano wa kitaifa? Makada wenzio wa CCM walipokeaje wito wa Mbowe? Je, kwa akili yako unadhani kuna tofauti kati ya wito wako wa "shikamano wa kitaifa" na ule wa "Prof. Mbowe" wa Maridhiano ya kitaifa?

Na unaposema wapinzani wanaombea hali iwe mbaya unaweza kuthibitisha hicho unachokisema kwamaana binafsi sijawahi na sitarajii kuwepo na "mpinzani" ambaye hana akili kiasi hicho.

Kama kweli unaumizwa na "siasa" juu ya gonjwa hili basi ingefaa uwakemee hawa wafuatao kwa kauli zao au vinginevyo useme kauli zao sio siasa (mzaha) dhidi korona.
1. Polepole (Katibu Mwenezi CCM) aliposema wapinzani ni maadui sawa sawa na korona.
2. Makonda (RC-Dar) aliposema "watu hawatoki ndani wanasubiri korona, kwani korona kitu gani"
3. Bulembo (Mbumge wa CCM) aliyesema "njia sahihi ya kupambana na korona tumchague Maguli aendelee kutuongaza". Alisema hivyo tena wakati huyo Magufuli ndo aliyeko madarakani.

Ukweli ni kwamba, anayetoa onyo siku zote anakuwa na maono/ufahamu juu ya hatari iliyopo. Bali anayepewa onyo na akashindwa kuzingatia maana yake ni mjinga au mzembe. Kinachotokea sasa kinafanana na ule msemo "mtoto akilia wembe mpe" kwa maana akijikata ndo atajua kumbe kiwembe sio "mdoli" bali umetengenezwa kwa ajili ya kukata. Hii ni namna dulani ya kutoa somo kwa vitendo. Humu JF kuna msemo maarufu wa "time will tell" na ule "muda" ndio sasa somo la wapinzani linaingia kwa vitendo kwenye vichwa zero vya watu sampuli ya Jiwe and Co. Lakini si kwamba anayeonya anatamani kutokee jambo baya.

Kiufupi ni kwamba serikali imedhihirisha UJINGA na UZEMBE iliposhindwa kuzingatia walichoonywa na wapinzani. Pole sana!
 
Hii maneno inanichanganya sana, yaani sijaona maombi ya kuombea mafuriko yasiendelee kuwasumbua ndugu zetu waliojenga mabondeni huko Rufiji na kwingineko, ila maombi dhidi ya Corona, comedy show, tunayoi'handle' kizembe zaidi yanaendelea .....!
💀💀💀☠😅😅😅🤡
 
Wewe ni mmoja wa watu wanaoongoza kuandika mada za kuchochea chuki kati ya CCM na wapinzani,na hata kwenye uzi huu umeendelea kutoa tuhuma za kipumbavu kabisa kuwa Wapinzani wanafurahia kuendelea kwa maafa haya ya Corona ili kuikomoa Serikali. Jitafakari, hata mods niliwahi kuwaomba kuwa kipindi hiki wasiruhusu mada zinazochochea chuki kwani kama Taifa inabidi tuwe kitu kimoja kwani vyama vitapita lakini mwisho wa siku Taifa litabaki lakini naona mods wanafurahia malumbano ya kipumbavu badala ya kuwa hili ni jukwaa la kuelimishana na kupashana habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani watu kama wewe mnaoliombea mabaya taifa letu. Si mnaonekana kwa macho na mnatukana watu hovyo.
 
Wantanzania kama taifa tupo katika kipindi kigumu sana.Maambukizi ya huu ugonjwa yameongezeka kwa kasi (Covid -19).
Kama taifa inatupasa tuweke siasa kando. Tushikamane ili kupambana na hili janga. Kama jamaa zetu kule China wana namna ya kupambana na huu ugonjwa basi tuwanonog'eze watuambie ni hatua zipi za haraka tuchukue.
Mpaka sasa total reported cases ni kama 170.Ila waliopona ni wachache sana ukilinganisha na maambukizi, maana wamepona watu 11. Hii inaonyesha wanaopona ukilinganisha na maambukizi ni ratio ndogo sana.
Nina hakika kabisa kabisa huduma za afya hapa Tanzania ni duni ukilinganisha na mataifa kama Usa,Italy, Spain au Italy. Hivyo kama wagonjwa wakiongezeka itakuwa balaa kubwa.
Nashangaa sana kuna watu ati kisa ni wafuasi wa vyama vya upinzani basi wao wanafurahia hili janga liliwaue watanzania kwa wingi. Kisa tu serikali iliyopo madarakani ionekane imefeli kukabiliana na hili janga. Hii haijakaa vizuri kabisa.
Kama taifa tuonyeshe umoja kwa kila namna ili kila mtu atoe mchango wake wa kila namna ili kukabiliana na hili janga. Tuache siasa za kupotosha au kupunguza morale ya kupambana na hili janga.
Umeandika kwa kutumia kichaa au kitu gani??
Hivi aliyeleta kejeli ni nani? Nani akiyewaita Wapinzani ni Corona? Nani akiyeidhalikisha Familia ya Mbowe? Nani aliyesema hatua zichukuliwe mapema kule bungeni wabunge wa CCM wakagoma?? Sasa hivi mlivyokuwa wanafiki mmeona mambo yanawazidi mnakataa kuwa accountable! I hate you guys aiseee
 
Back
Top Bottom