Mkuu unapotoka sana. Katiba ipo wazi kuwa wananchi wapo entitled to just renumeration. Maana yake ni kuwa wapate mshahara unaokidhi mahitaji yao kulingana na kazi wanazofanya. Hakuna mahala katiba inadai kuwa mshahara ukiwa mdogo uache kazi.
Kwanza kabisa naomba uelewe kwamba sitetei serikali kuwapa waajiriwa wake mishahara midogo. Hilo la kwanza.
But let's add some nuance here. Naomba tuchambue mambo kwa kina, si kwa juu juu tu.
Nakwambia hivi, suala la mishahara midogo linaweza kutatuliwa vizuri zaidi na kwa ufanisi mkubwa zaidi kiuchumi kuliko kisheria.
Kwa sababu, kisheria utaanzisha mzozo tu na serikali. Unasema habari za just renumeration wakati katiba haijatoa figure ya what is just renumeration. Uta argue vipi kwamba this is not just renumeration?
Serikali ikikuambia kwamba Watanzania wote wana haki ya kupata just renumeration, kwa sababu hakuna aliyelazimishwa kufanya kazi kwa mshahara anaoona ni mdogo, na anayeona mshahara wa serikali ni mdogo akatafute kazi private sector na NGOs. Rais Samia akakwambia na yeye alishawahi kufanya kazi serikalini,akaona mshahara mdogo, akajiongeza kwenda NGO, akapata mshahara mkubwa, akasoma, akarudi serikalini, akapanda ngazi mpaka kawa rais, utamjibu vipi?
Unaelewa kwamba kuna tofauti kati ya kusema everyone has a right to just renumeration na kusema everyone must get a salary over this amount?
Unaelewa kwamba ukilipwa mshahara mdogo serikalini, kama kiukweli serikali haina uwezo wa kulipa watu, na sekta binafsi ina mishahara mizuri na mikubwa iliyo just, wewe unayefanya kazi serikalini hujanyimwa right yako to just renumeration, kwa sababu hujanyimwa kuacha kazi serikalini na kwenda kufanya kazi private sector kwenye mshahara mkubwa?
Unaelewa kwamba haki nyingi hazipatikani automatically, kwa mfano, kila mtu mzima mwenye akili timamu ana haki ya kupiga kura, lakini ili kupiga kura inambidi ajiandikishe kupiga kura, hatakiwi kusema yeye atapiga kura tu kwa sababu katiba imesema ana haki ya kupiga kura?
Unelewa kwamba hiyo clause ya kila mtu ana haki ya just renumeration haina maana serikali ina wajibu wa kuajiri kila mtu na kumlipa mshahara fulani?
Unaelewa kwamba mtu ambaye katiba imesema ana haki ya kupiga kura, kama hajajiandikisha kupiga kura anaweza kuzuiwa kupiga kura bila haki yake ya kikatiba ya kupiga kura kuvunjwa, kwa sababu haki yake ya kupiga kura inaenda sambamba na wajibu wake wa kujiandikisha kupiga kura, asipotimiza wajibu wake hapati haki, bila katiba kuvunjwa?
Tatizo letu ni la kiuchumi.Litatuliwe kiuchumi. Kwa kuongeza uzalishaji na ufanisi.
Kwa sababu, unaweza kuilazimisha serikali ipandishe mishahara. Serikali ikakubali.
Ikasema kima cha chini ni milioni moja. Haya tunawapa right renumeration mnayotaka.
Huku uchumi haujapanda, uzalishaji haujapanda.
Matokeo yake serikali inachapisha hela bila kuongeza uzalishaji. Ili iwapatie mishahara yenu mnayodai.
Na kwa sababu hela zimeongezeka, bila uzalishaji kuongezeka, mfumuko wa bei unakuwa juu.
Hiyo mishahara yenu mipya inakuwa sawa na ya zamani tu, kwa sababu hela zimeongezeka zimekuwa nyingi, zinafukuza bidhaa chache ambazo hazijaongezeka. Kanuni za demand and supply zitafanya bei zipande.Economics 101.
Mtarudi tena kuililia serikali ipandishe mishahara tena.
Bila kujua inflation inawafanya mbaki pale pale!
Hakuna shortcut ya kuboresha maisha zaidi ya kuongeza uzalishaji na kupandisha uchumi.
Ukitegemea katiba na sheria tu kupandisha mishahara, hata ukipandishiwa mshahara, hutataua tatizo.
Utakuwa unaelekea kuwa kama Zimbabwe.Kwenda dukani kununua mkate unaenda na toroli la noti!