#COVID19 Kama Taifa limekubali chanjo ndio maslahi ya Taifa, Viongozi wote wanakuwa Bind na A Collective Responsibility Clause. Must support, Shut up or quit!

Ameongea akiwa kanisani sio bungeni Wala mahala pengine popote kwaio lile swala Ni la kiimani na alikua anaongea na waumini wake Kama wewe sio muumini wake haikuhusu mkuu.
 
Nashauri waziri wa afya ajibu hoja za Gwajima kwanza

Na aje public kama waziri wa afya wa Zanzibar mbona ameeleza kwa umakini umuhimu wa hiyo chanjo?

Wachanjwe kwanza wenyewe wote baraza la mawaziri waliopitisha hii chanjo

Wanachi tutafuata.
Hapa wanaweza wakaweka maji wakatupiga Changa la macho.
 
Hii issue Ina walakini na itakuja kutugharimu tusipokua makini.
 
Watu wa CCM ndo wanatakiwa wakubali Kila kitu hata Kama ni ujinga.uhuru wa kutoa maoni ni kwa Kila raia wa nchii hii kwaio muacheni atoe hoja zake wananchi wanasikiliza then wataamua zipi kipi Ni Bora kwao wachanjwe au hapana.
 
Kwa hiyo unataka kusema Gwajima yuko sahihi?

Anyway kama umechagua kuishi kwa maombi ya walokole it's okay. Ila nakushauri fuata sayansi
Kwenye sayansi Kuna biashara sometimes kwaio umakini unahitajika nafikiri wakuu viongozi wa nchi Ni watu muhimu kwa ustawi wa Taifa letu walitakiwa wakae mbele kwenye foleni wapate chanjo sisi tutafuata mbona barabarani huwa tunasimama wapite Kwanza.
 
Hata kabla ya Gwajima kujitokeza hadharani kupinga hiyo corona akiwa kanisani, aliipinga pia akiwa bungeni

Licha ya hivyo, tunao kina Gwajima wengi ambao hawana uwezo wa kuonekana mitandaoni ambao wanaendelea kuipinga hiyo chanjo licha ya kutoonekana

Kwanza, kwa nini Serikali haitawajibika kwa tatizo ambalo linaweza kumpata mtu atayechanjwa chanjo? Hauoni kwamba hii pia inatia mashaka kwa wananchi kutaka kuhoji endapo hizo chanjo kama ni salama?

Gwajima anawakilisha maelfu ya watu ambao hawana mahali pa kusemea ila wanasema kama Gwajima, Nyie mnaoogopa kutaka kufahamu hatima ya uhai wenu, nyamazeni kimya!
 
Nimecheka!!! ...yaani sina mbavu.
 
Uko sahihi kabisa!
Lakini pia wala Pascal Mayalla hajataka wewe "uisapoti" Serikali. Mtazamo wa Pascal niliouelewa ni kuwa wewe, mimi ama yeye, sote tuko free kutoa ushawishi tunaoutaka. Alichoandika Pascal ni Gwajima na utumishi wa umma wa ngazi yake. Wao ndiyo wanaounda Serikali na niserikali yao imekuja na msimamo fulani. Hoja ya Pascal iko simple sana, haijajikita kwenye kuzuia mawazo mbadala, isipokuwa kwa utumishi wa Gwajima na Serikali yao. Anapaswa atoke ili kuweza kupingana nayo hadharani
 
Taifa lipi limeikubali Paschal ilhali wapigia chepuo wenyewe wanatuambia ni HIARI?
 
Kwa Mkristu yeyote anayeyajua maandiko matakatifu hasa "Ufunuo", wa Yohana hawezi kuchanjwa chanjo hiyo.
Hii ni chapa ya mnyama(Ufunuo 13: 1~18). Kipindi hiki viongozi wa kikristu wa kweli wanajua hilo na sasa dunia inagawanyika makundi mwili, waliochanjwa na wasiochanjwa. Gwajima askofu yuko sahihi, lakini Gwajima mbunge hayuko sahihi.
Mamlaka za juu yake wataamua cha kufanya, ingawa kwa Tanzania hii naamini kila kitu kitabakia kama kilivyofanyika.
 
Wewe ndo huna hoja. hujui chochote kuhusu hiyo chanjo. ushahidi unaonesha kuwa hata waliochanjwa hupata corona kama kawaida. so this is bullshit. haina maana yoyote zaidi ya mipango yao ya kishetwani tu
 
I got mine wrong sure! Upo sahihi
 
mnashawishi watu wachanjwe kuhalalisha tripu zenu za kwenda kwa bwana zenu ulaya na marekani
 
Awahishwe Mirembe
Your browser is not able to display this video.
 
Kwani hana uhuru wa kuongea?

Je kuna sheria yoyote ya nchi amevunja?

Kama jibu ndiyo basi mpelekeni anapostahili kwa kitendo cha kuvunja sheria.

Kama jibu hapana basi muacheni aongee au apaze sauti kwa niaba yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…