Kama taifa linaongozwa na 60% ya viongozi wasio na Upeo, maana yake hata Raisi yumo?

Kama taifa linaongozwa na 60% ya viongozi wasio na Upeo, maana yake hata Raisi yumo?

Rais niliyemaanisha hapo ni yule ni yule aliye tutoka siku za karibuni. Simzungumzii huyu wa sasa! Huyu mama tutamtathmini mwakani! Inshallah!!
....... Tume ambiwa mwekezaji anakuja , na kukuta hatuna watu wenye huo uwezo, sasa chukulia sisi wananchi wa Tanzania, kama sisi ndio watekelezaji wenyewe, ili tupate watu wazuri wa kutawala/manage rasilimali zetu ili zitulete tija na unafuu wa maisha. Huoni hapo tunahitaji watu wengine wa nje
 
Inahuzunisha sana kuona taifa kubwa Africa mashariki linashindwa kusonga mbele kisa ya kukosa watu wenye weledi kuliongoza taifa hili. Kwa majibu wa Pro. Mussa Assad, 60% ya viongozi wetu hawana ujuzi wa kutosha, hii inaonekana kuwa nikweli kwa maana ya khari ilivyo. Sasa Kama ndiyo hivyo, maana yake hata Raisi yumo. Tutaepukaje hili, inaonekana kuna sehemu tunakosea kama taifa, nani atalisaidia taifa hili?
  • katiba mpya?
  • chuo cha viongozi?
  • Bunge imara?

Mungu isaidie Tanzania
Tuna katiba ya hovyo sn ya kutukuza Rais, hapo ndipo shida inaanzia
 
Back
Top Bottom