Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kutokana majukumu ya maandalizi mazito ya kazi za kikatiba kitaifa, kwa mfano ya uchaguzi wa serikali za mitaa nchini nzima, pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2025..
Mambo haya muhimu kwa taifa, yanahitaji muda mwingi wa kutosha kijipanga na kuyaandaa, yanahitaji umakini, utulivu, uangalifu na weledi mkubwa sana wa kusheria na kikanuni ili yafanyike kwa ufanisi, lakini pia yanahitaji fedha na rasilimali watu wa kutosha kusimamia utekelezaji wake, ili kuepuka utata na malalalamiko yasio na tija baadae....
Ni busara kama Taifa la wastaarabu, wenye kuheshimiana kulingana na mila, desturi na utamaduni wa kitanzania, lakini pia kama Taifa linaloongozwa katika misingi ya kisheria, kikatiba, uwajibikaji, uwazi, usawa, haki, utawala bora, utangamano wa kidugu, amani na utulivu wa nchi yetu,
Kwa maoni yangu, kama hamtojali ndugu wananchi na waTanzania wenzangu,
Nashauri na kuwarai nyote kama Taifa, tuipe nafasi na muda wa kutosha serikali hii sikivu sana ya wananchi, na tuiache na kuipa fursa tulivu, ifanye maandalizi haya mazito na ya msingi sana kwa kipindi hiki, ili kwa wakati muafaka haya yanayoendelea kuhusu chaguzi yatakapotamatika, tuanze sasa mchakato wa katiba mpya tukiwa huru, wamoja na wenye nia, muda wa kutosha, dhamira na uelekeo moja kwa mustakabali mwema wa umoja, mshikamano na amani ya MAMA TANZANIA
nawatakia nyote mapumziko mema ya wiki enda...
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE AIMEN..