Kama Taifa nashauri tukubaliane kwa kauli moja kwamba majadiliano ya katiba mpya yaanze rasmi baada ya uchaguzi mkuu 2025

Kama Taifa nashauri tukubaliane kwa kauli moja kwamba majadiliano ya katiba mpya yaanze rasmi baada ya uchaguzi mkuu 2025

Nafikiri mleta mada ,akubaliane na familia yake na machawa ila sio watz wenye kujitambua
sio mbaya,
ila hayo ndio maoni, mtazamo na ushauri wangu wa kizalendo sana kwa waTanzania wenzangu wenye mapenzi mema na amani na utulivu wa huyu MAMA TANZANIA..

nasalia kuyaheshimu sana maoni yako ya kinyonge, gentleman:pedroP:
 
Hata tukianza mwaka 2030.maana Watanzania ukiwasikiliza vizuri huku mitaani shida yao na kiu yao na mahitaji yao wala siyo habari za katiba.watanzania wanahitaji kuona yake afanyayo Rais Samia yanaendelea.mambo hayo ni kama vile uboreshwaji wa huduma za afya,elimu,usambazaji wa maji safi na salama,ajira kwa vijana, upatikanaji wa pembejeo hususani mbolea kwa wakati kwa wakulima pamoja na bei nzuri kwa mazao yao.

Wanasiasa walioshindwa kuwashawishi wananchi kwa hoja ndio wanahisi katiba itawasaidia kupata madaraka ya ubunge na udiwani.

Watanzania wanahitaji sera nzuri na wezeshi pamoja na uhakika wa kupata milo mitatu mezani pao.
Inawezekana kabisa nyie chawa ndio mnamwaribia raisi sifa zake.
 
Kwel kila kitu unakijua mkuu hongera sana mheshimiwa.
hapana,
sijui na sifahamu kila kitu,
ila angalau nina uelewa kiasi fulani juu ya masuala mbalimbali kwa namna nyingi, kwa sababu nimeishi katika hali hizo nilipokua najitafuata kimaisha....

ila kuna madini mengi sana ya muhimu na ya maana najifunza na kuyaelewa vyema kwa manufaa ya maisha yangu binafsi kiroho na kimwili, kitaaluma, kisiasa, kiuchumi, kijamii, kitaifa na kimataifa zaidi kutoka kwa familia hii kubwa na pana sana na ninayo iheshimu, kuipenda na kuijali ya JF:pedroP:
 
Safi sana kiongozi , nimeikubali hiyo .
 
Naunga mkono hoja, tubadilishe tumuongezee miaka mingine , atake asitake tumlazimishe
hapana,
katiba ya wananchi ninayoipendekeza mimi tuanze mchakato wake baada ya uchaguzi mkuu wa 2025, sio kwaajili ya kumuongezea muda au miaka ya kuongoza mtu fulani au chama fulani, la hashaaa, ni kwaajili ya haki, usawa, uhuru, uwajibikaji na uwazi katuka ugawaji rasilimali za nchi kwa manufaa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa wa Tanzania wote:pulpTRAVOLTA:
 
Katiba Mpya inaweza isichukue hata zaidi ya mwezi kupatikana kama kuna dhamira njema!
Kwa kuwa hakuna dhamira njema ya Watawala hata baada ya 2025 hakutawepo na mchakato wa kupata Katiba Mpya!
katiba mpya isiyochukua zaidi ya mwezi kuundwa, hata za kwenye vikoba na makundi mbalimbali ya kijamii huku mitaani, zinasumbua sana,

na makundi yenye aina hizo za katiba ya mwezi moja, hawana amani wala utulivu kwenye vikundi vyao, kwasababu ya ubovu wa katiba zao....

Tanzania yafaa kutengeza katiba itakayoishi miongo na miongo bila kusababisha mgogoro miongoni mwa waTanzania wenyewe. Tutumie muda mrefu na wa kutosha kujadiliana, tutumie rasilimali na tunu za wataalamu mbalimbali tullionao ili kufikia muafaka wa pamoja, tukiwa wamoja na wenye uelekeo moja miongoni mwa waTanzania wote:pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom