Kama Taifa tukubali kuna makosa yalifanyika, tujirekebishe yasijirudie, japokuwa ni ngumu kuondoa makovu yaliyopatikana


Kuchekana ni kwa zamu subiri yakujie wewe tena yatakuja kwa staili ya tofauti kabisa na uzuri wake hautakumbuka.

Usiwahi kufurahia matatizo yanapompata mwingine ikiwa bado unapumua.

Kabla haujafa haujaumbika
 
Ww ni mfaidika wa huu udhalimu wa awamu hii, hivyo lazima utoe mrejesho chanya kuendana na wanaowezesha familia yako kwenda chooni.
Yaani watu wengine ni kinyaa ndugu yangu huyo mtu anatetea unyama wa awamu hii,ni sheria zipi zimefutwa basi wafute katiba ya nchi yetu na ya kwao danganya toto ya zidumu fikra sahihi, dhaifu na mfu za CCM.
 
Tuko milioni 60

Vigelegele vya wahuni wachache wasiozidi laki moja visikutishe
 
Wakati wanapanda miba badala ya mahindi wengi sana walionya kwa wema tu wakaishia kupotezwa, kupigwa risasi, kufilisiwa, kubambikwa jela, kutekwa, nk leo miba imekua awaitaki tena wanataka wavune mahindi.
 
Kuchekana ni kwa zamu subiri yakujie wewe tena yatakuja kwa staili ya tofauti kabisa na uzuri wake hautakumbuka.

Usiwahi kufurahia matatizo yanapompata mwingine ikiwa bado unapumua.

Kabla haujafa haujaumbika
Lissu si unamuona anavyofurahia kuzusha ohhh Magufuli anaumwa kwa nini nisisikie raha nikiona Lissu anatembea kwa kuchechemea kwa kukatwa mapanga na kupigwa marungu baada ya fumanizi?

Naambiwa hata yale mambo hawezi tena.Ni padre
 
Alphonce, Lissu, Ben ndo wakina nani hao?

Shida ukada ndio unawasumbua vijana wa Tanzania.


Ukiukaji wa Sheria haujaanza Leo hapa nchini.

Toka tunapata Uhuru wa kwenye makaratasi Sheria zinakiukwa hivyo kama mnataka kuleta hoja za kutetea haki kisheria leteni kiujumla wake.

Na sio kidini, kichama au kiukoo.
 

Wakati Iddy Amini anaua Waganda hakuna Mganda hata mmoja aliandamana, na hakuna aliyethubutu kumobilize watu waandamane kupinga unyama wake, maana angeishia kaburini. Kwa mtiririko wako huu wa utetezi, ni kuwa waganda walikubaliana na hayo mauji maana hakuna aliyeandamana, wala kudhubutu, na wote walionyesha kupinga utawala wake aliishia kuwaua. Kinachofanyika hapa kina picha hiyo hiyo hata kama kiko kwenye hatua ya awali.
 
Iundwe kamati haraka sana ya maridhiano ya kitaifa ili kuponya makovu Haya. Chuki iliyopo nchini ni zaidi ya ile ya apartheid kule Africa ya kusini kipindi cha Makaburu.
Ndo maana watu wanafurahi jiwe kufa maana yeye ndiye aliyejenga hio chuki
 
Sawa waliondoka lakini waliokamata hakuna anayewataka kutwa wanatembea wakijificha kama digidigi walichoahidi hawajakitimiza wanawindwa kuuawa kila kona ya nchi hazitawaliki

Kwasababu walitawala kama wao, wala hakukuweko na smooth transition, na hayo yanayoendelea kwenye nchi hizo kwa sasa, ni athari za kuwa na viongozi wenye viburi vya madaraka. The same applies right in our country at the moment.
 
Matukio uliyotaja kuhusishwa kwa vyombo vya Dola ilaleta ukakasi na haujawahi kutolewa ushahidi thabiti. Kufumbiwa macho pia si sahihi sababu taarifa zenye usaidizi zinapotolewa polisi husaidia kukamatwa watuhumiwa na kuhukumiwa. Tushirikiane na katika kutoa tip wa waliofanya makosa waweze kuchukuliwa hatua.
 
Huo ni mfano tu lakini kuna unyama mbaya sana unafanyika
Hili ni tatizo sugu kwa hapa TZ na kwa Africa kwa ujumla ukishakuwa askari tu basi tayari uko juu ya sheria ufanye unavotaka hii kitu kinachoitwa Polisi ni falier sana hapa TZ .Its very shame .
 
Kwasababu walitawala kama wao, wala hakukuweko na smooth transition, na hayo yanayoendelea kwenye nchi hizo kwa sasa, ni athari za kuwa na viongozi wenye viburi vya madaraka. The same applies right in our country at the moment.
Mfano Chadema ndani hakuna smooth Transition Hatuombi mabaya Mbowe akifa leo haieleweki nani atashika lakini si hivyo tu mbowe mwenyewe sauti hana hakuna smooth transition ya bunge viti maalum lilillopita na la sasa la akina Halima Mdee!!! akina halima mdee wamempindua Gadafi Mbowe na Elbashiri Tundu Lisu na Mugabe Godbless Lema na kuingia bungeni!!! upo hapo
 
Tuko milioni 60

Vigelegele vya wahuni wachache wasiozidi laki moja visikutishe
Kwa sisi tuliosoma uongozi na kufanya kazi serikalini hadi tumestaafu tunajua kwamba kwenye uongozi mtu mmoja tu miongoni mwa maelfu unaowaongoza akisimama kwenye mkutano akatoa hoja fulani inayokusuta au inayoponekana kutoridhishwa na jinsi unavyowaongoza huwa tunachukulia serious huo ujumbe. Ukianza kusubiri eti, hadi watu wote milioni 60 waseme utakuwa umechelewa sana na hujui uongozi kabisa kabisa.
 
Yaani mbunge anamiminiwa risasi 38 tena kwenye kota za serikali bado unasema ni mhalifu?
 
Sasa kwa umri wako wote mpaka umestaafu unategemea mtu apendwe na kila mtu kweli?

Muulize hata Lisu hapo chadema atakwambia si wote wanampenda
 

Utetezi uupeleke wapi na kwa nani, hapa ni kwenye majukwaa huru, watu wanaweka ukweli wa mambo hadharani, maana hatuna tena taasisi za kutoa haki zinazoaminika, kwani wanaaondesha unyama ndani ya nchi hii, ndio hao hao wanaosimamia taasisi za kutoa haki. Matokeo yake ni kuminywa kwa haki huku tukiwa tunaona kwa macho yetu, na wale wote wanaokemea wazi wazi unyama huo ndio wanashambuliwa hata kuuwawa, huku vyombo vya habari vikiwa vimezibwa mdomo.

Haya yanayoendelea ndani ya nchi hii ni matokeo ya kutawaliwa na mtu muovu, japo zinatumika njia nyingi za kinyama kufunika ukweli huo usionekana kwa wengi, na hata ukionekana kuwe na hofu ya kuusema.
 
Sasa kwa umri wako wote mpaka umestaafu unategemea mtu apendwe na kila mtu kweli?

Muulize hata Lisu hapo chadema atakwambia si wote wanampenda

Hakuna anayetaka kupendwa na wote acha upotoshaji, hoja ni unachukiwa kwa nini, na mifumo ya kutoa haki inafanyaje kazi chini yako. Mwenendo wa taasisi za kutoa haki tunaona kwa macho yetu ukiwa na hofu ya maamuzi ya mtu muovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…