Kama Taifa tukubali kuna makosa yalifanyika, tujirekebishe yasijirudie, japokuwa ni ngumu kuondoa makovu yaliyopatikana

Kama Taifa tukubali kuna makosa yalifanyika, tujirekebishe yasijirudie, japokuwa ni ngumu kuondoa makovu yaliyopatikana

Iundwe kamati haraka sana ya maridhiano ya kitaifa ili kuponya makovu Haya. Chuki iliyopo nchini ni zaidi ya ile ya apartheid kule Africa ya kusini kipindi cha Makaburu.
Watanzania wako milioni 60 waleta chokochoko hawafiki 10 unataka maridhiano ya kitaifa? kila mtu abebe mzigo wake

Mleta chokochoko kimpate cha kumpata na wengine waendelee na maisha yao
 
Naamini ni ngumu kupata suluhu, kwa kuwa chonzo ni uchaguzi, je, watakuwa tayari kukiri walipora kura na ushindi? Watakubari kuwa hawata pora tena kura na ushindi? Kuacha uonevu kufuata katiba.
Tatizo lingine ni kuongea vitu visivyo kuwepo kama uchaguzi ulikuwa huru na amani, ushindi wa kishindo, wananchi mmetupa kura nyingi hapa, wakiwa wanajuwa wengi wamewakataa!
Kiongozi kwenda sehemu na watu kujaa si kipimo cha kupendwa, watu hawana kazi hivyo ni kwenda kushangaa tu, na ukimuuliza kila mmoja aliyeudhuria mikutano anasema watu walikuwa wengi, sio tulikuwa wengi, yaani yeye anajiondoa!
 
Kuendelea kushupaza shingo kuwa hakuna makosa yaliyofanyika juu ya uvunjifu wa haki za binadamu hapa nchini kwetu ni kupoteza muda. Maana ni kutaka kujenga taswira isiyofaa kuwa mauaji, ukatili na uvunjifu wa sheria ni jambo la kawaida.

Tukubali kuwa kuna makosa makubwa yalifanywa na vyombo vya dola na yanaendelea kufanywa na vyombo vya dola. Maana mbali ya watu wanaojulikana kama Lissu, Saanane, Alphonse Mawazo bado kuna malalamiko makubwa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola. Mbaya zaidi viongozi wanajua na wanafumba macho.

Tusishupaze shingo, tukubali makosa yalifanyika na tujirekebishe maana kukosolewa au kupata mawazo kinzani ni sehemu ya maisha. Hii nchi ni ya kwetu sote.

Lakini je nani atayafuta makovu yaliyopatikana na udhalimu waliofanyiwa akina Alphonse Mawazo, Tundu Lissu, Ben Saanane na wengine wengi ambao hawajulikani?
Hakuna makosa yoyote makubwa yaliyofanyika katika nchi Hii Kama unavyojaribu kujenga hoja hapa...na Wala hakuna ukiukwaji au uvunjifu wa haki za binadamu hapa...ila wapo wakorofi, wavunja sheria, miongozo na kanuni na waliozoea kufanya maovu na ambao Sasa wamebanwa na wanashindwa 'kupumua'...Na Hawa wataendelea kubanwa mpaka washike adabu na kuomba po...cleansing is taking place in our society...
 
Inabidi tuunde truth and reconciliation committee kama ile iliyoundwa South Africa
Haihitajiki hapa tuna viongozi wachache wa upinzani wachochea shari wakiondoka nchi inatulia sababu hawana support kwanza tofauti na South Africa ndio maana unaona wakiitisha maandamano hawapati support na wao wenyewe ndani ya vyama hawana support mfano wanasema hatutambui uchaguzi akina Halima Mdee na wabunge kibao hao mbio bungeni!! sasa watu hawasikiliziki ndani ya chama chao na nje unataka reconciilition nao ya nini? Hata upinzani hauwa support walipinga serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar wazanzibari wakawapiga chini wakaingia serikali ya umoja wa kitaifa!!! Ndani kwao tu kunawaka moto they have support Hapa I mean Lisu,mbowe, Lema na Zitto Kabwe
 
Kuna uvunjifu wa haki za watu sana ndani nchi hii. Mf; wiki mbili zilizopita maeneo ya tengeru kuna trafik aligombana na bodaboda yule boda akatoroka pikipiki ikabaki.

Kesho yake wale askari wamekuja wanapiga kila mwendesha pikipiki awe boda hasiwe boda unajua hujui wakawashika na kuwapeleka mahakamani baada ya hapo magereza ya kisongo wiki mbili.

Kwa tabia kama hizi, wananchi hawezi kuvipenda hivi vyombo vya dola wala kuvipa ushirikiano wa maana.
Hii kudhibiti vyombo vya habari, lengo hasa ilikuwa ni ili unyama uwe unafanyika bila kutangazwa, na habari zikitangazwa ziwe ni zile wanazotaka hao waendesha unyama.
 
Kweli kabisa, huwezi kumimina risasi zaidi ya 33 kwa binadamu mwenzako
Hakuna aliyethibitisha hilo zaidi ya Lissu mwenyewe hakuna independent source yeyote iliyowahi kuthibitisha hilo zaidi ya Lissu kutamka .Alijibunia kuwa zilikuwa risasi 33 hakuna mtanzania aliyewahi ona ripoti ya daktari kuthibitisha hilo .Ni Lissu ndio huchonga mdomo kusema alipigwa risasi 33.Lakini kwa uzushi huo ndie aliongea na BBC nk kuwa Magufuli anaumwa bila ushahidi wa third party wa ripoti ya daktari nk

Mimi siamini kama Lissu alipigwa risasi sina ushahidi wa third party wa ripoti ya daktari yawezekana alipigwa marungu na mapanga alipofumaniwa na mke wa mtu ndio maana aligoma kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi
 
Watanzania wako milioni 60 waleta chokochoko hawafiki 10 unataka maridhiano ya kitaifa? kila mtu abebe mzigo wake

Mleta chokochoko kimpate cha kumpata na wengine waendelee na maisha yao

Wakati Gaddaf, Mugabe, Elbashir nk wanaua wasiokubaliana na mwenendo wao wa uongozi, walikuwa pia na watetezi kama ww, na walitumia maneno haya haya. Leo hii fuatilia viongozi hao waliondoka vipi madarakani, na wapambe wao kama ww walikuwa wapi wakati yanawakuta ya kuwakuta hao mabaradhuli.
 
Hakuna makosa yoyote makubwa yaliyofanyika katika nchi Hii Kama unavyojaribu kujenga hoja hapa...na Wala hakuna ukiukwaji au uvunjifu wa haki za binadamu hapa...ila wapo wakorofi, wavunja sheria, miongozo na kanuni na waliozoea kufanya maovu na ambao Sasa wamebanwa na wanashindwa 'kupumua'...Na Hawa wataendelea kubanwa mpaka washike adabu na kuomba po...cleansing is taking place in our society...

Ww ni mfaidika wa huu udhalimu wa awamu hii, hivyo lazima utoe mrejesho chanya kuendana na wanaowezesha familia yako kwenda chooni.
 
Wakati Gaddaf, Mugabe, Elbashir nk wanaua wasiokubaliana na mwenendo wao wa uongozi, walikuwa pia na watetezi kama ww, na walitumia maneno haya haya. Leo hii fuatilia viongozi hao waliondoka vipi madarakani, na wapambe wao kama ww walikuwa wapi wakati yanawakuta ya kuwakuta hao mabaradhuli.
Sawa waliondoka lakini waliokamata hakuna anayewataka kutwa wanatembea wakijificha kama digidigi walichoahidi hawajakitimiza wanawindwa kuuawa kila kona ya nchi hazitawaliki
 
Binafsi nimeogopa sana kushuhudia vigelegele na shangwe ya uvumi wa huyu ndugu kupatwa na tatizo. Imefunua kilichomo ndani ya mioyo ya watu wengi nchini. Hii haitawahi kushuhudiwa kwa siku za karibuni. Ila mimi mzee wa siku nyingi hali hii imenikumbusha jinsi tulivyofurahi na kusherehekea kufurushwa kwa Nduli Idd Amin Dada wa Uganda miaka ile ya 1978 hadi 1979 wakati wa vita kati ya Tanzania na Uganda. Ukweli ni kwamba ilikuwa vita kati ya Tanzania na Idd Amin. Kwanza tulisherehekea uvumi wa kwamba amekamatwa, akajitokeza kwamba yupo salama na hakuna wa kumkamata, tukapoa kidogo. Baadaye kidogo vijana wetu wakafanya kweli, wakaiteka nchi ya uganda na kuwa chini ya himaya yao. hapo hakuwa na ujanja. Akakimbilia Saudi Arabia. Tulisherehekea usiku na mchana kumshinda Nduli idd Amin, sawa sawa na inavyosherehekewa sasa. Watu walisherehekea sana uvumi, Kassimu atatuliza upepo kwamba jamaa yupo fiti. Sasa kama ikitokea kuwa kweli nafikiri kutakuwa na sherehe mara tatu ya ile ya mwanzo.
 
Ww ni mfaidika wa huu udhalimu wa awamu hii, hivyo lazima utoe mrejesho chanya kuendana na wanaowezesha familia yako kwenda chooni.
Wewe ni muathirika wa utawala huu kutokana na Lissu kukimbilia Ubelgiji familia yako haiendi chooni
 
Back
Top Bottom