Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Lowassa asingekwenda CHADEMA Dr. Slaa asingetoka CHADEMA. Slaa kutoka CHADEMA kukatoa njia kwa Lissu kuwa mrithi wake kwenye siasa za CHADEMA.Tumefika hapa kwa kosa la kumkata Lowassa 2015
Watu wengi akiwamo Nyani Ngabu wanashangaa mambo mengi waliyokuwa wanayasema zamani, leo yanaonekana kama mapya!
Nadhani kama taifa tukifanya uchunguzi wa kina tutagundua imekuwaje tumefika hapa tulipo. Kwa mtazamo wangu hali tuliyo nayo leo, inatokana na Tanzania kuwa na mtu anayeitwa Tundu Antipas Lissu.
Ukiachana na harakati zake za kutetea watu mbali mbali kisheria, Lissu alipoingia kwenye siasa, alibadili aina ya siasa zetu kutoka siasa za kinafiki kwenda kwenye siasa za kusimamia kweli kuhusu masuala muhimu wa kitaifa.
Inasemwa kuwa alipogombea ubunge mwaka 2010, aliyekuwa mgombea Urais kupitia CCM wakati huo Jakaya Kikwete,alipofikia kwenye Jimbo la Singida magharibi, aliwaambia wapiga kura wa Jimbo hilo kuwa ni heri wasimchague yeye kuwa Rais kuliko kumchagua Lissu kuwa mbunge.
Kumbe Lissu hakutakiwa kuwa mwanasiasa na wanasiasa wa Tanzania. Alipoingia bungeni akawa ni mwanasiasa msema kweli bila ya kuzunguka.
Sasa Lissu katufikishaje hapa. Lissu kupigwa kwake risasi hakukuwa nje ya misimamo yake kisiasa. Lissu kupingwa kwake asiwe Mwenyekiti wa CHADEMA hakukuwa nje ya mitizamo yake jinsi siasa za CHADEMA zinavyotakiwa kuwa.
Leo Lissu asingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, CHADEMA isingegomea uchaguzi bila ya marekebisho ya Sheria za uchaguzi na hivyo hata hawa kina Josephat Gwajima na Humphrey Polepole hoja zao zisingekuwa na uzito ilizonazo sasa.
kwa ivo Lissu alianza kujenga aina Mpya ya siasa za nchi hii bila ya wanasiasa wa Tanzania kujua kuwa mfumo wa aina ya siasa zao umeingiliwa na kirusi.
Leo wanasiasa wanapotaka kupambana na Lissu wanakutana na upinzani mkali kwa kuwa aina ya siasa alizoziasisi Lissu ndizo zinazokubalika kwa sasa.
Lissu ni kama taswira ya Dr. Wilbroad Slaa kabla hajakengeuka. Tofauti kati ya Lissu na slaa, ni kwamba Lissu ana muendelezo wakati Slaa alionesha kukata tamaa baada ya Lowassa kukaribishwa CHADEMA mwaka 2015.
Bro wapi UPO nikununulia Nyama choma na sharubati ijumaa hiiWatu wengi akiwamo Nyani Ngabu wanashangaa mambo mengi waliyokuwa wanayasema zamani, leo yanaonekana kama mapya!
Nadhani kama taifa tukifanya uchunguzi wa kina tutagundua imekuwaje tumefika hapa tulipo. Kwa mtazamo wangu hali tuliyo nayo leo, inatokana na Tanzania kuwa na mtu anayeitwa Tundu Antipas Lissu.
Ukiachana na harakati zake za kutetea watu mbali mbali kisheria, Lissu alipoingia kwenye siasa, alibadili aina ya siasa zetu kutoka siasa za kinafiki kwenda kwenye siasa za kusimamia kweli kuhusu masuala muhimu ya kitaifa.
Inasemwa kuwa alipogombea ubunge mwaka 2010, aliyekuwa mgombea Urais kupitia CCM wakati huo Jakaya Kikwete,alipofikia kwenye Jimbo la Singida magharibi, aliwaambia wapiga kura wa Jimbo hilo kuwa ni heri wasimchague yeye kuwa Rais kuliko kumchagua Lissu kuwa mbunge.
Kumbe Lissu hakutakiwa kuwa mwanasiasa na wanasiasa wa Tanzania. Alipoingia bungeni akawa ni mwanasiasa msema kweli bila ya kuzunguka.
Sasa Lissu katufikishaje hapa. Lissu kupigwa kwake risasi hakukuwa nje ya misimamo yake kisiasa. Lissu kupingwa kwake asiwe Mwenyekiti wa CHADEMA hakukuwa nje ya mitizamo yake jinsi siasa za CHADEMA zinavyotakiwa kuwa.
Leo Lissu asingekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, CHADEMA isingegomea uchaguzi bila ya marekebisho ya Sheria za uchaguzi na hivyo hata hawa kina Josephat Gwajima na Humphrey Polepole hoja zao zisingekuwa na uzito ilizonazo sasa.
kwa ivo Lissu alianza kujenga aina Mpya ya siasa za nchi hii bila ya wanasiasa wa Tanzania kujua kuwa mfumo wa aina ya siasa zao umeingiliwa na kirusi.
Leo wanasiasa wanapotaka kupambana na Lissu wanakutana na upinzani mkali kwa kuwa aina ya siasa alizoziasisi Lissu ndizo zinazokubalika kwa sasa.
Lissu ni kama taswira ya Dr. Wilbroad Slaa kabla hajakengeuka. Tofauti kati ya Lissu na slaa, ni kwamba Lissu ana muendelezo wakati Slaa alionesha kukata tamaa baada ya Lowassa kukaribishwa CHADEMA mwaka 2015.
Mwambie asogee hapa 361 hapa kunae yule mdudu mtamu kabisaaBro wapi UPO nikununulia Nyama choma na sharubati ijumaa hii